Kama sio tajiri na huna asset, kusomesha watoto shule za gharama ni ujinga unaongeza umaskini kwenye ukoo

Kama sio tajiri na huna asset, kusomesha watoto shule za gharama ni ujinga unaongeza umaskini kwenye ukoo

Kuna Mtu namfahamu anauza zake tu Viazi mbatata Sokoni pamoja na bidhaa zingine ndogondogo ila yuko katika Vikundi vya Vicoba kama Saba hivi anawasomesha Watoto wake Shule za Gharama wakati Yeye bado amepanga na hana hata Uwanja na Kwao shida hazibanduki.

Na bahati mbaya aliyonayo sasa anawasomesha Watoto huko Shule za Gharama lakini Wote wawili hawana Akili na Kutwa Wanafeli tu na Jamaa anabakia Kuwapiga huku akiwaambia wanamtia Hasara Kipesa.
Huyo ndo wakumsaidia atoke humo
 
Mm. Imeanza sasa wako la tano na nne wana Ng’ombe wa Maziwa 7 na ndama 7 Maziwa kila siku 30lt
Mie ndio nimenunua shamba.. natarajia kuhamia.manispaa mpya.. nipate muda wa kuwachungia future yao nikiwa jirani kabisa.
 
Mkuu

Unaongea as if upo kwenye your own utopia

Wewe una akili,ulisoma ukafaulu vizuri tu bila hata kusumbuka

Cha ajabu una equate your brilliance na the rest of 60mil normal Tanzanians!

Tunazungumzia athari ya sisi kutokua na maarifa coded kwenye lugha yetu wenyewe kutoka generations and generations ago

Hatuna budi kumfata Mzungu ili tu-survive

Na yeye maarifa yake kaweka kwa Kingereza,hatuna budi kujifunza Kingereza kwanza kwa usahihi then ndio tuchimbe maarifa yake

Hata wewe hapo hizo A ulizopata za 81% ungekua unajua Kingereza kama native language ungepata 99%

Watoto wetu wa OLevel "wanakariri" definitions za vitu mbalimbali sababu tu hawaijui hii lugha...Watoto hawalali "wanakariri" definition ya Osmosis wakati wanatakiwa "waelewe" ambapo lugha ya Kingereza ni integral part yake!

Kwanini nchi zote zenye kutumia Kingereza zina maendeleo na elimu kubwa zaidi ya nchi ambazo hazitumii Kingereza?

Kwanini?

Sababu ni kwamba,dunia nzima elimu na maarifa yote yamevumbuliwa na English Speaking nations hivyo wana advantage ya lugha kuelewa haya maarifa kwa usahihi kuliko wewe Mswahili

Mfano mfupi ni nchi za Africa zinazoongoza kua na elimu bora na maendeleo bora ni zote zinazotumia Kingereza....sio South Africa,sio Nigeria,sio Egypt sio Kenya,etc....wengine wote Tanzania included ni mavi jumlisha mavi

Huna lugha,huna maarifa,huna maendeleo,huna chochote,unacheza makida makida tu...sijui lini mtaelewa na liCCM lenu la hovyo!

Nyerere new all these unfortunately alichoka mapema...Lee Kuan Yew new it and implemented it better than Nyerere...

Halafu leo anakuja pumbavu mwenzangu EllySkyWilly anabishana na Kingereza as if yeye ana maarifa aliyogundua yaliyoandikwa native kwa lugha yake ya Kiswahili

Na Kiswahili mna ki-overrate mno..ni lugha ya hovyo na haitumikia duniani zaidi ya TZ na Zanzibar...msije jidanganya....mnaotegemea wawasaidie kukiongea walao Wakenya nao ndio hawakitaki wanajua upumbavu wake...Mombasa tu ndio wanaongea kama lugha ya kienyeji..Uganda,Burundi,Rwanda,Kongo,etc ni some people....hii ni nonsense

Learn English or die doing nonsense here in TZ....hadi emails mnashindwa kuandika,upumbavu mtupu,bure kabisa...ndio maana Tanzania we will never be an international hub,never

Na mtaletewa Wakenya kila siku wawe maCEO wenu....maana ni majinga mno...kila siku mnaambiwa jifunzeni Kingereza,hatutaki,kuleni kiburi sasa...na mtaisoma vizuri maana Rwanda sasa hivi wameigeuza English speaking country bado kidogo Rwanda ita overtake everybody kama international hub...majinga nyie

Tatizo linaanza hata walimu hawajui kiingereza
If I was the Minister wa Education
Ningetafuta walimu waliostaafu from UK wanaotaka kujitolea kufundisha kiingereza (volunteers)
U jus have to provide them with good accommodation
Kama huelewi English huwezi kuelewa hata hiyo Historia ya Tanzania unless ifundishwe kwa kiswahili
 
Aisee ni sawa na kujenga msingi mbovu wa nyumba huku ukiwaza kuezeka kwa bati za gharama kubwa kama sio kuweka paa la vigae ama bati za South!

Kila hatua ya mtoto anayoipitia kielimu ina nafasi ktk mustakabari wa hatma yake!
Hivyo Kama una uwezo mpatie tu Elimu yenye msingi bora tangu awali/ mwanzo ili huko Elimu ya Juu awe fit kutokana na alichokipitia tangu akiwa mdogo!
Tatizo huko kwenye elimu ya juu .finally anataka kupata nini!? Kwa sababu kama ni ajira ndio lengo basi bora tuzitunze hela tumpe aamue kununua cheti au kufanya biashara.. kupoteza muda au kuingia akapambane!?

Imagine mtu anayeamua kuwa mkulima immediately baada ya kumaliza form four.. halafu nahuyu anayeamua kusoma Advance secondary education, there after chuo kikuu ili awe agronomist.. kwenye field aliye drop form four ana experience ya 6 by the time unaingia na ww kulima..

Huyo mtu pamoja na nadharia za chuo kikuu zako.. ana mengi ya kukufundisha.. leo mbunge wa KAHAMA ameiwekea vizuri sana.. elimu ya sasa ni biashara tu .. wanatangaza vikubwa na reality haiwezi hata kuachieve vidogo.

Na content ya hii elimu ndio much more questionable.. planner anasoma theory zilizotumika kutatua shida za ulaya mwaka 1890-1920... Leo mwaka 2021 akiwa anaandaliwa kutatua shida za Mtanzania.. such a waste of time and resources
 
True.. mtu analipa milioni 3 ama nne kwa mwaka ili mwanae ajue kiingereza tu. Huku sylabus anayofundishwa mwanae wa tusiime ni ile ile ambayo wa elimu bure anafundishwa. Tofauti ni lugha tu.

Tatizo la elimu yetu ni sylabus. Jaribu kuwaza hiyo milion 3 kila mwaka mnunulie kiwanja ndani ya miaka 7 atakuwa na asset kiasi gani huyo mtoto.

Mtoto atakuwa na uhakika wa kupata elimu ya juu ama basic need hata kama mzazi umefariki.

Haumjui mnachoongea nyie tuulizen sie santa kayumba tunavyopata shida leo....watu wangapi uwa mnawacheka umu wenye nyazifa ila lugha mbovu ?
 
Tatizo huko kwenye elimu ya juu .finally anataka kupata nini!? Kwa sababu kama ni ajira ndio lengo basi bora tuzitunze hela tumpe aamue kununua cheti au kufanya biashara.. kupoteza muda au kuingia akapambane!?

Imagine mtu anayeamua kuwa mkulima immediately baada ya kumaliza form four.. halafu nahuyu anayeamua kusoma Advance secondary education, there after chuo kikuu ili awe agronomist.. kwenye field aliye drop form four ana experience ya 6 by the time unaingia na ww kulima..

Huyo mtu pamoja na nadharia za chuo kikuu zako.. ana mengi ya kukufundisha.. leo mbunge wa KAHAMA ameiwekea vizuri sana.. elimu ya sasa ni biashara tu .. wanatangaza vikubwa na reality haiwezi hata kuachieve vidogo.

Na content ya hii elimu ndio much more questionable.. planner anasoma theory zilizotumika kutatua shida za ulaya mwaka 1890-1920... Leo mwaka 2021 akiwa anaandaliwa kutatua shida za Mtanzania.. such a waste of time and resources
Unavyoongea utafikiri kilimo ni rahisi kama unavyo type hapa.....eti atakua na 6 years expiriensi katika fildi of agrikacha baada ya kumaliza fom fooo.....motivesheno spikaz bwana
 
Unavyoongea utafikiri kilimo ni rahisi kama unavyo type hapa.....eti atakua na 6 years expiriensi katika fildi of agrikacha baada ya kumaliza fom fooo.....motivesheno spikaz bwana
Sijaelewa hoja yako ni nini!?
Kwamba hatakuwa na 6yrs experience!?
Au hakuna wanaowezalima kwa miaka 6?
Au kwenye Agrikacha ukisoma miraculously unakuwa na experience zaidi ya aliyelima miaka sita!?

Honestly sijaelewa ..kipi unaargue against.
 
Kilimo gani kinachozungumziwa hapa hikihiki kinacholimwa na wapigania uhuru hadi leo miaka zaidi ya 60 ,mkulima hana at nyumba ya bati yupo kwenye kibanda Cha nyasi ananyeshewa mvua?
Bado ata hawezi kuafford basic needs anatembea na nguo viraka Kama vyote!!
Hiki kilimo ambacho hakitoshi kumlisha mkulima hata mwaka mzima?
Asee elimu Ni muhimu acha kujidanganya
Kama unataka awe mkulima mpeleke SUA appate best education about agriculture,aweze kutumia elimu yake kuboresha na kuongeza agricultural production,embu niambie mkulima ambae hahasoma anajua Nini kuhusu kilimo Kama sio kupanda tu mbegu na kutdgemea mvua,mvua zisiponyesha ndio basi Tena anatangatanga njaa,kilimo kinahitaji uwekezaji mkubwa kwenye cost na experts,
Hicho kilimo Cha mazoea Ni kurithishana umasikini tu,
 
Hiyo expiriensi ya miaka 6 kwa kilimo hiki hiki ambacho tumekua tukikiona na hata wazazi hawako proud nacho kiasi kwamba wanasema "soma mwanangu usije kulima".
 
Kina dingi angu mkubwa alimsomesha mwanae Scotland BA in Accountacy akamaliza,ada alikuwa analipa almost 20ml per semister mungu sio John sins bwana akamaliza mzee wake akamuambia rudi nyumbni uje utulie

Kurudi bongo akaomba kazi akapata huko maswa halmashaurin salary 650000

Mshua ake akamuambia huwez fanya kazi salary ni hiyo ya kimaku temana nayo,

Uzuri alikuja pata kazi nyingine Norway ndio alipo mpaka sasa

Kibongo bongo unaweza msomesha mtoto kwa ela ndefu then anakuja kushikiwa chini na jiwe kwa mshahara wa 450000

Ila kila mtu aishi anayojua mwenywe tusiumizane akili
 
Kilimo gani kinachozungumziwa hapa hikihiki kinacholimwa na wapigania uhuru hadi leo miaka zaidi ya 60 ,mkulima hana at nyumba ya bati yupo kwenye kibanda Cha nyasi ananyeshewa mvua?
Bado ata hawezi kuafford basic needs anatembea na nguo viraka Kama vyote!!
Hiki kilimo ambacho hakitoshi kumlisha mkulima hata mwaka mzima?
Asee elimu Ni muhimu acha kujidanganya
Kama unataka awe mkulima mpeleke SUA appate best education about agriculture,aweze kutumia elimu yake kuboresha na kuongeza agricultural production,embu niambie mkulima ambae hahasoma anajua Nini kuhusu kilimo Kama sio kupanda tu mbegu na kutdgemea mvua,mvua zisiponyesha ndio basi Tena anatangatanga njaa,kilimo kinahitaji uwekezaji mkubwa kwenye cost na experts,
Hicho kilimo Cha mazoea Ni kurithishana umasikini tu,
Hakuna anayekataa elimu. Shida ni aina ya elimu.. hiitegemezi haina maana.. sua wanamaliza maelfu kwa maelfu.. ila wakulima siwaoni wakiongezeka kwa maelfu.. tena to be honest ndio kwanza wanapungua.

Na hao akina Sumry waliofanikiwa ka large scale farmers hawakusoma sua.

Ni sawa na engineering ya UDSM wakitoka unajikuta kiutendaji ni bora mtu wa DIT au VETA maana alichojifunza hakikumuandaa kufanya..

Aina ya elimu tuliyonayo haiwezi kutuondoa kwenye umasikini. Unaandaa wwatu wengi wa kwenda kusimamia vilivyoanzishwa tayari Mameneja. Sasa nani aanzishe!?
 
Hiyo expiriensi ya miaka 6 kwa kilimo hiki hiki ambacho tumekua tukikiona na hata wazazi hawako proud nacho kiasi kwamba wanasema "soma mwanangu usije kulima".
Shida ni kwasababu wamerubuniwa. Elimu ilipaswa kuna na lengo la kuwanelighten watu. Na ilipaswa kuwa lengo la state kuhakikisha watu wake wamekuwa enlightened enough.

Thana ya kufanya elimu biashara ni dhana waliyouziwa african countries kuwadidimiza kwenye umasikini wa milele, bila kutumia nguvu.

Tanzania bado inahitaji wasomi, ili kuusaidia kuwa na jumuiya yenye uelewa wa kutosha. Kuanza kuuza elimu kwa muda huu ni kudiscourage azma ya kufikia state yenye uelewa mkubwa..

Kwanini wazazi wanataka tukasome, wakati wa elimu ya kujitegemea, kipindi cha mwalimu.. hata graduate wa darasa la saba alikuwa sisi well equipped kufanya kilimo.bora.

Shule watu wakisoma basics za uongozi, sayansi ya kilimo ( namna bora ya kufanya kilimo kwa maeneo tofauti tofauti, sayansi ya kujikimu, namna bora ya kuboresha mlo wake, afya na unadhifu wa mavazi na mazingira, katika hesabu walijifunza hesabu za fedha, kuandaa budget na kuandaa wazo la biashara kwa vitendo. Alijifunza mambo mengine kama michezo, sanaa na ufundi)

Haya yote yalimdhihirisha mbele ya watu wasiosoma alionekana bora zaidi. Lakini leo unatoka unajua definition na kutaka kazi kwa mhindi.. hiyo elimu inamsaidia nn mzazi!? Tukiendelea hivi wengi hawatawapeleka watoto vyuo vikuu katika generation hii tunayoishi ya ukosefu wa ajira.
 
Me naona tatizo kubwa ni umaskini. Tutafute hela alafu tusipangiane maisha.
 
Kuna Mtu namfahamu anauza zake tu Viazi mbatata Sokoni pamoja na bidhaa zingine ndogondogo ila yuko katika Vikundi vya Vicoba kama Saba hivi anawasomesha Watoto wake Shule za Gharama wakati Yeye bado amepanga na hana hata Uwanja na Kwao shida hazibanduki.

Na bahati mbaya aliyonayo sasa anawasomesha Watoto huko Shule za Gharama lakini Wote wawili hawana Akili na Kutwa Wanafeli tu na Jamaa anabakia Kuwapiga huku akiwaambia wanamtia Hasara Kipesa.
HAPANA huwezi sema hawana akili na wanafeli, iko siku wakirudi hapo mtaani hamuwezi shindana nao hata na watoto wenu wa mitaani wakioenda kanumba
kila binadamu ana akili ndio maana mzazi atachagua akasomee masomo gani km mchanganyiko na masomo ya ziada ya Dini ya kiislam au Kikristo mzazi atalenga,
Kama atampeleka zenye masomo ya Kichina, kifaransa, au kuogelea yote yamafundishwa huko,
sio mtoto akitoka shule anapitia vibanda umiza vya mipira, kung fu au sex wewe unarudi jioni unasema utasahihisha home work zake
usisomeshe mtoto kwa ajili aje aajiriwe na Serikali mpe mradi wako baada ya kumaliza, sio umuwekee ng'ombe wa maziwa leo, je ukija wala hao mg'ombe au ukaongeza watoto wengine wadogo zake km 6 hizo ng'ombe zitatosha

FRESHMAN

usimbanie mtoto elimu, mlipie km una uwezo wala kwa Ulimwengu wa leo usitarajie kuajiriwa na Serikali ila Elimu uliyompa atabuni biashara za kileo na hata Serikali itamchukua akionesha vyetivyake
IMG-20210214-WA0018.jpg
 
Asante sana mleta mda.

Kusoma huu uzi nimegundua machache.
-Wengi tunafarijiana na kudanganyana (ni wachache kama wapo) wenye uwezo lakini wakaamua kuwapeleka watoto wao shule zetu za Kayumba. wengi wetu (30s na kuendelea naamini tulipita hizi shule. We know what we are talking about).
-Si kweli kwamba mtoto ukimpeleka Kayumba, utafanya savings za kumnunulia assets. Na waliosoma academies hawatakuwa na assets.....at the end of the day wengi waliosoma Kayumba..ndo hao utakuta ni semi illiterate..kiingereza hawajui..kiswahili hawajui..ilmradi maisha yanakwenda. Hata maofisini wanaweza kuja na vyeti vya first class lakini kujieleza ni shida!
-infact wanaosoma shule za academies ndo unakuta wengi wazazi wamewaandalia mazingira mazuri...
-Elimu ya Tanzania inatutayarisha kuajiriwa (blue collar jobs. Haimuandai mwanafunzi kuwa innovative na kutengeneza utajiri. Ndo maana unakuta humu wengi tunapambana kuwanunulia viwanja, kuwajengea nyumba nk watoto wetu all in the name of "assets".
-Ndo maana ukiangalia wengi waliobahatika kufanya kazi serikalini most ni wezi wezi na wajanja wajanja. unakuta mtu ana viwanja 5, nyumba za kupangisha laki mbili au tatu na frame kadhaa....na ndo atakwambia ana assets.
-Humu I can bet my last coin wengi wanaoandika wakiponda hizi academies..watoto wao wanasoma hizo shule.....ukweli ni kwamba kwa Tanzania ya leo Kayumba au shule za kata ni za watoto wa wasiokuwa nacho. ( ndo maana utakuta Mwigulu anakwambia Kiswahili lugha ya taifa ndo itumike kila sehemu…..yet mwanae anasoma Feza! Zako changanya na za kuambiwa!
-Ni kama gari huwezi kuwa na uwezo wa kununua V8 au Prado ukaenda kuchukua Vitz au IST..kisa kwamba yote ni usafiri….….very few will do that.
-Mwisho wa siku mafanikio ni juhudi binafsi na baraka za mwenyezi Mungu. Kuna waliosoma Kayumba na wametusua kweli kweli..ingawa wengi wanapigika. na kuna waliopita kwenye hizi academies ambao wametusua na wengine wako mjini na kiingereza kingi. Ingawa hili group la academies..hata kama maisha yamewapiga..wana survival skills (wanajua kujieleza na wana exposure). Unaweza hata kumkuta customer care Tigo au DSTV! Huko kiingereza kimetamalaki!
-Mimi nasomesha mwanangu shule ambayo nina uwezo nayo. Siwezi kumpeleka Kayumba nilikosoma mimi eti naogoa maneno ya waja! Ngoja akapambane...Mimi natimiza wajibu wangu. Aijuaye kesho ni Mungu pekee.
-Dunia ya leo ni Kijiji. lazima ujue lugha za watu. Uwe confident. Ujue dunia na walimwengu wanataka nini….you have to position yourself! Ujue kupambana kweli kweli..na katika hilo utahitaji silaha zote. Ukisikiliza maneno ya wanasiasa...utaishia kugombania ajira za Magufuli ambazo hazipo…..hata ukizipata mshahara ndo laki tano (dola 200!)..hapo kwa nini usichanganyikiwe?
-Ushauri wangu: Usisikilize mtu humu. mpeleke mwanao shule ambayo una uwezo nayo. Mengine ni porojo tuu za waja.
 
Na bahati mbaya aliyonayo sasa anawasomesha Watoto huko Shule za Gharama lakini Wote wawili hawana Akili
Eti hawana akili! Hebu kazae wako wenye akili!

Wachawi mna shida sana ninyi!

Mtoto anawezaje kuwa hana akili?
 
Unavyoongea utafikiri kilimo ni rahisi kama unavyo type hapa.....eti atakua na 6 years expiriensi katika fildi of agrikacha baada ya kumaliza fom fooo.....motivesheno spikaz bwana
Hahahahhaaa

Nimecheka sana.
 
Hawana exposure..na kujiamini.
Kujua lugha hakukufanyi smart... Au kujua kabla ya mwingine hakukufanyi uwe na akili zaidi yake.. mtoto anatakiwa ajue hilo mapema maishani.

Elimu ni kutafsiri maarifa uliyopewa au kupata katika maisha yako ya kila siku. Mtoto anajua kiingereza hajui kufunga kamba za viatu inamsaidia nini!?
Mtoto anajua kiingereza hawezi kwenda sokoni mwenyewe na kurudi itamfaanini!?

Logic and Reasoning ndio muhimu. Kwa level za chini watoto wanatakiwa kuwa curious... Mid ages waweze kuleta connection na theory na uhalisia katika maisha yao.. mtoto awe huru atleast saa 9 saa kumi aende akacheza apumzike kutoka shule ... Ukizidisha hapo unaua curiousity mtoto anakuwa duster ananyonya kila kitu kama kilivyo without Reasoning
Umemaliza mkuu japo wapo watakaochelewa kukuelewa, ahsante kwa elimu.
 
Hivi huu msemo Wa eti watoto wanaosoma shule za academies sijui private school eti wanaishia kujua lugha tu, mi natofautiana na wewe mkuu, Kijana wangu yuko std seven hizo shule, sikifichi anawa challenge hata majamaa waliosoma hizo ma A level za kata na wanamkubali mbaya.
Bosi huyo anakipaji hata angekuwa st kayumba angekuwa juu tu mimi nina mdogo wangu yupo form Three Now Ilboru anawakimbiza mbaya hao wa sijui international school na dogo kasoma st kayumba
 
Back
Top Bottom