1. Ukiristo ulileta habari za Utatu, Qur'an imekuja kunyoosha mafunzo hayo ya kipotevu na kuweka rekodi sawa kuwa Mungu ni mmoja na kwamba utatu ni imani ya kipotevu.
2. Wakiristu walidai Yesu kafa msalabani na kwa hilo eti ni ondoleo la dhambi, Qur'an inasema Yesu hakufa msalabani, na wala hakuna ondoleo la dhambi kwa mtu kufa kwa ajili ya mwingine bali kila mtu atabeba mzigo wake.
3. Wakiristu wana imani ya dhambi ya asili, Qur'an inasema Adamu alipokosa aliomba msamaha na akasamehewa.
Unaongea kirahisi sana ,binafsi nimekuwa muislamu nikaritad,
Uislamu ni dini Haina misingi thabiti ya kujisimamia ,ni dini imejengwa kwa propaganda sana
Biblia ni kitabu cha kale chenye uthibitisho mkubwa wa kihistoria. Kuna zaidi ya manuscript 5,800 za Kigiriki, 10,000 za Kilatini na maelfu mengine kwa lugha za zamani kama Coptic, Syriac, Armenian n.k. Mfano, Codex Sinaiticus ni nakala kamili ya Biblia ya karne ya 4 AD,
Codex Vaticanus ni ya karne ya 4 pia, na Dead Sea Scrolls zina sehemu za Agano la Kale zilizoandikwa kabla ya Kristo kuzaliwa, hadi karne ya 2 K.K.
Hizi zote zinafanana kiuhakika na Biblia tunayosoma leo.
Je, Qur’an ina wapi hata nakala moja ya kale ya karne ya 7 yenye kuthibitisha asili yake? Haipo,
isipokuwa Qur’an ya Uthman aliyeteketeza nakala zote tofauti ili kubaki na moja aliyochagua. ,cha ajabu hata hiyo ya Uthman Leo haipo popote pale ,Je unawezaje kumshawishi mtu kama Mimi awe muislamu?😂😂
Hii ni historia, si chuki.
Halafu iweje tuiamini Qur’an ambayo asilimia kubwa ya simulizi zake zimekopiwa kutoka vitabu vya Apokrifa vya Wayahudi na Wakristo waliokataliwa?
Mfano, hadithi za Yesu kuumba ndege kwa udongo zimo kwenye Injili ya Watoto ya Tomaso si sehemu ya Injili halali.
Hadithi za Abraham na Samawati saba, pia ni hadithi kutoka Talmudi ya Kiyahudi.
Qur’an haikuja na kitu kipya ilikusanya mapokeo yaliyokuwapo na kuyapachika katika mfumo wa Kiarabu.
Kuhusu Utatu, Biblia haifundishi Mungu watatu bali Mungu mmoja aliyejifunua kwa sura tatu Baba, Mwana na Roho Mtakatifu.
Hii haipingani na umoja wa Mungu. Yesu hakujibuni bali ametabiriwa.
Yeremia alitabiri Agano Jipya (Yeremia 31:31),
Danieli alitabiri muda wa kuja kwa Masihi na kuuawa kwake (Danieli 9:26),
Isaya alisema wazi kuwa Masihi atauawa kwa ajili ya makosa ya watu (Isaya 53),
na Daudi, miaka 1,000 kabla ya Kristo, alisema
“Walinichoma mikono yangu na miguu yangu” (Zaburi 22:16),
na pia alisema
“Hutakia nafsi yangu kuzimu; wala hutamwacha mtakatifu wako aone uharibifu” (Zaburi 16:10)
huu ni unabii wa kufufuka kwake.
UNAWEZAJE KUNISHAWISHI MTU KAMA MIMI NIMUAMINI MUHAMAD NA QURAN ?
Yesu kufa msalabani ni kiini cha injili. Biblia inasema
“Kwa maana alifanywa dhambi kwa ajili yetu yeye asiyejua dhambi, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika yeye” (2 Wakorintho 5:21).
Hii ni neema, si udhaifu. Kama kila mtu atabeba mzigo wake, basi hakuna haja ya rehema wala msamaha lakini kwa Yesu, Mungu mwenyewe alivaa mwili ili kutupatanisha naye.
Sasa ni haki kweli kuyaacha maneno ya manabii waliotabiri kwa karne nyingi kabla ya Yesu, kisha nimwamini mtu mmoja tu TAPELI mudy aliyejitangaza miaka 600 baadaye bila ushahidi wowote ?