Kuna mchangiaji mmoja amesema yote haya yanafanyika kwa juhudi na kukutana na watu sahihi!
Ndugu yangu mshukuru MUNGU sana umekutana na watu sahihi, nahisi hii inaweza kuwa ndo bahati. Yaani kuna watu unakutana nao maishani unajuta! kama huna mtu wa kukusemelea ofisni kwako, kila siku anayetakiwa kukusemelea kwa boss yeye ndo ana ji brand hata pale ambapo wewe umefanya usitegemee kutoboa wala kupewa cheo.
Mimi naamini kabisa bila watu sahihi ni ngumu kupiga hatua!!
Narudia Tena hiyo unaita kukutana nawatu sahihi mie kwangu naiita Bahati mkuu. Kumbuka huyo ni Boss wa watu wote. Lakini kipekee alinipigania kawaandikia HR barua kwamba huyu jamaa sio graduate lakini kazi zake mnaziona hapa. Napendekeza apandishe nafasi akataka na daraja.
Kitu nasisitiza, usikae tu au kutokufanya chochote kusubiria bahati, haiendi namna hiyo. Kwenye juhudi zako na kujituma kwako huko huko utakutana na bahati.
Nitoe mfano mwingine kunihusu.
Tukiwa kwenye mtihani wa mwisho O level, tulikua tunatengwa makundi wengine wanaingia kufanya mtihani wa vitendo kundi lingine mnasubiria wamalize ila hamtakiwi kuonana Kwa vile watavujisha maswali.
Siku hiyo tunafanya chemistry paper 2. Tulivyoingia chumba Cha mtihani, sikugusa chochote, nikaanza kusoma maswali kwanza na maelekezo, wakati naendelea kupitia hayo maswali na Nini Cha kufanya, nimefika mwisho nikaona mwalimu anapita haraka haraka kama anatafuna kitu. Alipofika kwangu akasema tumepata, kumbe Kuna jamaa alichelewa, ilikua lazima afanye huo mtihani muda huo ili mchana aingie kwenye mtihani mwingine. Sie tulikua na mtihani mmoja tu. Ikabidi niambiwe nisiguse chochote nimwachie jamaa afanye.
Sasa kwakuwa nilikua nimeshaona swali, sikutakiwa kuonana na watu wengine, ikabidi nipelekwe kwenye ofisi nikae peke yangu nikiwa nasubiria wamalize namimi niingie na kundi jingine. Hapo nilipowekwa ilikua ofisi ya mwalimu wa chemistry na kulikuwa na kitabu Cha Lambert mezani.
Nikachukua nikawa napitiapitia, nikakuta lile nililoliona kwenye mtihani lipo na maelezo yake kama wamelinakili wakalitoa kwenye mtihani. Kwa ufupi ilipofikia zamu yetu niliandika majibu Ile practical ilikua kutimiza wajibu tu.
Hapo hapo kwenye Chemistry, paper 1 Kuna yale mawali soil sijui organic na inorganic, wakati yanafundishwa nilipata changamoto sikwepo shule. Hii hali ikanitatiza sana. Nikachukua past paper nne kufanya swali la soil tu, mojawapo likaja kwenye mtihani na ndio nilianza nalo, hali kadhalika kwenye swali la Sulphur Kwa kuwa sikusoma hiyo topic nzima, usiku wa kuamkia mtihani ni kama kitu kilinisukuma kuamka nikachukua Lamber, nikaenda eneo Moja nikakutana na kipande kidogo tu kuhusu Sulphur na maelezo yake ndio yalikuwa kwenye swali lililotoka kwenye mtihani.
Matokeo kutoka, nna A ya chemistry lakini kiuhalisia sikuwa mzuri wala sikuwa na maandalizi ya kutosha kiasi Cha kufaulu daraja A, ni hayo mambo mie nayatafsiri kama Bahati.