Nimejaribu, kupiga hesabu, wastani miezi sita ya kukaa kila nchi hizo 125, mara umri wake 34, nikatoa miaka 14 ya shule, msingi na Sekondari, nikabaki na miaka 20, ambayo hii ndiyo ameitumia kutembea nchi 125, akikaa watani wa miezi sita kila nchi nikagundu inabidi tumuongezee miezi kama 60, ili iendane umri wake ukitoa miaka 14, ya shule kwenye umri wake 34.
Mimi naamini inawezeka kwa kutembea nchi 125 ila kila nchi ukikaa miezi sita basi itabidi tukuongezee miaka mitano, na ukitoa miaka mitano kwenye miaka ya shule, utabaki na miaka 9 ya shule. Inawezekana ama pia haiwezekani.