Kama ulianza kutumia Internet mapema miaka ya 1990 na 2000 njoo hapa tukumbushane Internet Cafe tulizoenda, Vimbwanga, Kero na Kumbukumbu

ukijua kuzima computer tayari we ni mtalamu nakumbuka kulikua na program moja ivi nimeisahau jina ilikua yakufundisha jinsi ya kuweka vidole kwa mpangilio kwenye kybod na kuandia kwa mikono miwili
 
Huo mwaka nilinunua computer kichwakichwa nikapigwa kwa 350,000/= ila nilipotezea kwa sababu mpigaji hakuwa MSUKUMA.
 
wakuu huu uzi utabadilika uwe wa games sasa [emoji23] [emoji23]

ikipendeza zaidi moja wenu afungue uzi maalum wa games tbt, nami ntakuwa mchangiaji maana nilikuwa mdau si haba


Emaili yangu ya kwanza ni YAHOO
Ila Hotmail mwaka 2001 baada ya kuja na mfumo charting papo kwa papo kama mwezio yupo
ONLINE wote tukahamia HOTMAIL

ilikuwa tukitoka kucheza mpira jion CBE ndani pembezoni mwa kiwanja cha BASKETBALL kwa ndani mule Halafu Uzio wa CBE kulikuwa na nyumba kuna TAUSI ndege wakubwawakubwa tunacheza mpila huku TAUSI wakitutazama tunacheza KANDANDA

Basi jioni haooo tunaelekea zetu mitaa ya UPANGA internetCAFE kucheck email zetu na kucheza game ONLINE
 
Moshi mjini, Cafe ya Kahawa house ground floor kama unalizunguka hilo jengo, Kicheko pale opposite na stand na kuna cafe ilikuwa ya container mtaa ilipo Malindi na ofisi ya Tanesco kama unaelekea kwa Arusha road.

Hawa jamaa wamekula sana buku zangu tkwa robo saa kabla ya kushuka jero robo saa baadae jero nusu saa!! Baadae zikatoweka kabisa kwa kukosa wateja
 
Sisi Tulioanza Tumia Internet 2010-2011 Tena Kwenye Smartphone Tunacomment Wapi wajameni?
Whatsapp Isiyo Na Notification(Push Notification) Mpaka Ufungue Whatsapp Ndo Unaona New Messages.
Android Ice Cream Sandwich 4.0,Android Honey Comb
 
Enzi hizo naambiwa kuhusu net cafe na bro mmoja kwamba ana E-mail sijui ana uwezo wa kuingia facebook na mambo mengine. Muda wote ananitambia mimi nanote pembeni.

Wiki hyo hyo nikajitafuta huyo mpaka cafe nikafungua zangu email yangu pale ya Rocketmail enzi hizo ndio inasikika sana na Facebook nikajiunga zangu.

Baada ya hapo nkamtumia friend request, kesho yake ameenda net cafe alivyotoka ananitafuta dogo nani amekufundisha. Nikajitamba nilikua najua kumbe nimeyajua kwa kuunganisha dots[emoji28]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…