Kwenye 1998 hivi tulikuwa na morali wa kwenda mbele, ikawa ukitaka kuandika emails za kuomba chuo unaenda posta kariakoo na mbarua wako unampa mhudumu wa pale posta unalipa shs 800 ana-type na kuituma kupitia Africa online, wewe unakaa nyumbani kusubiri prospectus yako kupitia S.L.P.
About 1998-1999 tukawa tunaenda UD-ardhi na mshikaji wangu ambaye sister wake alikuwa anasoma pale, anatupeleka computer room kulikuwa na internet connection lakini mouse hamna tunakomaa na keyboard tu (ilikuwa ngumu sana).
About 2000-2001 nilikuwa naenda IFM kwa mshikaji wangu aliyekuwa anasoma pale,Kila mwanafunzi alikuwa na password yake, akawa ananiachia natumia na mpaka sasa ninayo address niliyofungua pale (
jinalangu2001@yahoo.co.uk).
Internet cafe yetu maarufu ilikuwa Richmond pale kariakoo karibia na round-about. Japo zilikuwepo zingine ndogo mdogo mitaani.
Sasa kati ya 2002 na 2003 nikapata Compaq pc Pentium ya windows 98 lakini ilikuwa inatumia floppy disks tu. Mwanangu mmoja akitoka bongo records na cd yenye ngoma zake za album anataka tuziingize kwenye computer lakini ndo hivyo tena haiwezekani. Mungu si Mayele nikapata HP Pentium II tower yenye windows ME na CD-ROM, then windows XP, hapo sasa nikaanza kuhifadhi mangoma ya Wana. Then nikanunua CD writer (kazi ikaanza). Flashdisk ya Kwanza ya MB 128 niliinunua KVD kwa shs 35,000.
Baadae Zantel wakatuletea dial-up connection (simu za mezani) kwa shs 96,000, unaweka vocha ya elfu 5 au 10 unapata network Safi.
Sasa kilchoendelea baadae, Sote tunaona. Bado kugusana tu kupitia mtandao.