Kama umezaliwa bila ulemavu wowote usiache kumshukuru Mungu hata mara moja kwa siku

Kama umezaliwa bila ulemavu wowote usiache kumshukuru Mungu hata mara moja kwa siku

Pole sana mdogo wangu kipenzi Leejay49 nina imani utaendele kukaa sawa na utaendelea na majukumu yako mengine😍

Yes, humu sometimes kuna watu wanakera sana, na bila kuangalia kwa umakini unaweza jikuta unagombana na kila mtu maana si kila mtu anapenda afanyacho mtu
.... halafu nikuibie siri, hakuna members wanafiki humu kama wanawake, tena wale wa karibu yako...chukua point hiyo!!!
Leo mnacheka vzr, kesho anaunda kigroup Pm na mmoja mmoja unaanza kuiona rangi yake, mifano ninayo na wanajijua.
Ila usiwaze, japo kila siku tunawalalamikia akina Paw na Fang na Cookie kuwa wabadilishe mfumo wa hata mtu uliyemu-ignore, asinione na nisimuone kwenye thread, kiufupi tusionane, ila naona hii kitu haiwezekani!!!😔

You're dada love you❤️
Kuna vi group visivyo rasmi humu, NOTED!
 
For sure,
Mimi sijawai kuugua au kuumwa umwa tangia niwezaliwa hichi kipind ndio nimepitia Maumivu Sanaa

Haya majanga yasikie TU kwa watu Ila yasikukute

Vp Unaendeleajee wewe kwa Sasa...........

Kikubwa tusikate tamaa mungu Ni mwema tutakaa sawa..
Hadi nimeandika na uzi jua naendelea vizuri,. Tunasubiri tu mda wa daktari kupita saa kumi naweza nikaruhusiwa wanasema
 
Wakuu habari za siku nyingi,..

Sikua najua how they feel, sikua najua ni kwa namna gani wanateseka mpaka mda huu ambapo Mungu ameamua anipitishe na mimi kidogo, huenda bila hivyo ningeendelea kuwachukulia kawaida…

Iko hivi,. Nimepatwa na uziwi wiki ya pili sasa ,. I don’t know the mechanism mpaka ilikua hivyo ila nachokumbuka ni kwamba nilipatwa na malaria makali pamoja na kichomi at once,. Nilikua to that point ambayo sikua naelewa chochote zaidi ya jina langu ambalo hata sikua nasikia kama naitwa,..

Namshukuru Mungu naendelea vizuri somehow,. Ila guys viziwi ni wanateseka sana,. Imagine masikio ni mazito, yameziba halafu mda wote unafeel like uko jirani na mtambo ambao unapiga kelele halafu huwezi kurealize ni kelele za kitu gani,,. Means hatakama unataka kuzungumza kitu unahisi wote wanasikia makelele inabidi uongee kwa sauti ya juu sanaaa,. Halafu wanakushangaa unapayuka , which is not easy 😌🥹… Yaani masikio mda wote yako na ganzi hata mtu akufinye husikii maumivu just imagine..

Nipo najiwazia hapa viziwi hii ndio hali wanaifeel for the rest of their lives 🤔, na je ikitokea na mimi nakua kiziwi ina maana ndio nitateseka hivi maisha yangu yote ??? ,.. Thanks Lord nimewahi treatment leo moja limeanza kusikia i hope yote yatasikia tena,. ( Mniombee wananzengo siko poa niko wodini bado,. Malaria nayo nayaniendesha ).


NB: Mtu kama upendezwi na mada za mtu au humuelewi hapa jukwaani ni better ukamuignore kuliko kureport kwa mods nao bila kufanya utafiti vizuri wanapigana ban,. Sio wote tuko humu just for fun,. Yaani wewe uliyenireport sijui hata nikufanye nini maana kuna watu nilikua nao seminar huko Pm na wametoka kunipa tu hela napigwa ban imagine😔😔.. Yaani naitwa tapeli kwasababu ya chuki zako binafsi,. SIJAPENDA
Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, angekuwepo, ulemavu usingewezekana kuwapo.

Ukiona tunaishi kwenye dunia inayoweza kuwa na ulemavu, huo ni ushahidi Mungu huyo hayupo.
 
Back
Top Bottom