SEHEMU YA PILI.
Namna kufika Germany na UAE na shughuli za kufanya.
Germany- Kwanza kwa asiyefahamu, Ujerumani ni nchi inayoongozwa na maneno ya Paulo Mtume aliyowaandikia Wathesalonike katika barua ya 2; 3:10. “Asiyefanya kazi na asile”.
Ukiwa Germany ni mwiko kuishi bila kufanyakazi yoyote. Sijui kama sera imeshabadilika lakini wakati naenda kupiga kazi wakati wa kiangazi, ilikuwa mhamiaji akikamatwa anazurula....anakamatwa na kupewa kazi yoyote ili ale chakula kwa kukifanyia kazi. Kuombaomba na kupewa bure katika nchi hii ni dhambi. Napendekeza mtu kwenda katika nchi hii kwani kupata kazi ni rahisi.
Kwa Ulaya au nje ya nchi hakuna kitu cha muhimu Kama kuwa na kazi. Hii ndo sababu nashauri sana kuangalia nchi ambazo itakuwa rahisi kupata kazi.
-Namna ya kufika Germany. Nchi hii ni mojawapo ya nchi zinazounda Umoja wa Ulaya(European Union).
-Kwa hiyo ukiweza kupenya mojawapo ya taifa linalounda umoja huu basi inakuwa rahisi sana kuingia Germany.
-Unaweza kwenda kama mtalii wa nchi mojawapo ya taifa la EU kisha ukazamia Germany kusaka sega la asali.
NB: Ukikamatwa Germany na passport lazima urudishwe nchini mwako mara moja kwa gharama zao. Sera hii ipo pia Switzerland and Netherlands.
-Kwa hiyo cha kufanya, ukifika nenda Ubalozi wa Tanzania nchini Ujerumani, wapatie passport yako halafu utakapoamua kurejea nchini tena itakubidi kuifuata ubalozini.
-Germany pia inatoa nafasi za masomo kwa hiyo unaweza kujaribu bahati yako kuomba udhamini.
-Kiingereza kinaongelewa lakini ukifahamu Kijerumani utakuwa katika nafasi nzuri sana.
(Nakumbuka namna nilivyopata chance ya kuwa naenda kupiga kazi Germany, ni baada ya siku moja kuwa na mazungumzo na Mjerumani mmoja ambaye alikuwa ni visiting lecturer chuoni kwetu. Aliponiuliza natokea wapi nikamjibu Tanzania halafu nikaongezea, moja ya nchi iliyotawaliwa na babu yako...nilifanya hivyo in an amazing casual way kiasi kwamba aliniona mtu cheerful nisiye na resentments. Tulitokea kuwa mabest sana na hata kuwa ananifanyia michongo ya kazi zenye malipo matamu).
Mwisho ukiwa Ujerumani-fanya kosa lolote lakini siyo kuchelewa chelewa. Uchelewaji ni kitu Mjerumani hawezi kuvumilia. “Be obedient to Kantian punctuality”.
UAE [emoji1256] (United Arab Emirates)
Kwa asiyefahamu, unaposema [emoji1256] una maanisha muunganiko wa vinchi saba ambavyo makao makuu yake yapo Abu Dhabi. Kiongozi Mkuu pia yupo Abu Dhabi huku msaidizi wake akiishi Dubai.
Abu Dhabi ndiyo imeshikilia uchumi mkubwa kwa sasa ikifuatiwa na Dubai kisha Sharjah.
Umoja huu, mbali na Abu Dhabi, Dubai na Sharjah, unajumuisha pia Ajman, Umm Al Quwain, Fujairah na Ras Al Khaimah.
-Wale vijana wa Ilala wanaofuata spea za magari Dubai, chimbo lao lipo Sharjah.
Namna ya kufika- Wepesi wa kufika Dubai ni kwamba kama unatokea Tanzania unaweza kwenda bila visa na ukakata visa on arrival. Kwa maana hii Mtanzania yeyote anaweza kutinga Dubai bila shida yoyote.
-Unaweza kwenda kama mtalii kwa kukata visa ya miezi3 au 6 na kishafika kule ukaprocess working na resident permit. Visa hii utahitajika kukata ticket mbili yaani go and return lakini kwa sasa technology itakusaidia kwa kukata ticket moja ya go na return unaweza kupata “DUMMY TICKET”.
-Pamoja na kuwa [emoji1256] una vinchi saba, binafsi napendekeza Dubai kwa sababu zifuatazo;
- Mchanganyiko wa watu wa mataifa mengi
- Ni mji ambao ni very westernized
- Uchumi ni mzuri na kazi bado zipo japo competition ni kubwa sana kutokana na kuzungukwa na labor-zone states yaani Africa, India, Pakistan, Afghanistan, Srilanka, Bangladesh, Lebanon, n.k.
- Gharama ya maisha ipo chini sana ukilinganisha na nchi nyingi zilizoendelea
- Thamani ya pesa ni nzuri sana (1AED=630Tsh)
- Ni karibu sana hivyo panafikika(nauli inafika hadi chini ya laki5 za Kitanzania)
- Ni rahisi sana kutuma pesa nyumbani kutokea Dubai
- Kuna sehemu za kuabudi za wahindi ambapo wanatoa breakfast, lunch na dinner bure kabisa hivyo kwa mzamiaji unaweza kuishi kwa kuvizia mlo sehemu hizo.
-Ukiwa Dubai unaweza kufanya kazi za kuajiliwa kama vile Ulinzi, Usafi, Ujenzi n.k au unaweza kujiajili mwenyewe kwa kufanya shughuli zifuatazo
-Unaweza kuingia mjini kati yaani Deira City Centre na ukapiga kazi ya kupakia na mizigo kwenye magari.
-Unaweza kufanya kazi ya kusukuma toroli la mizigo katikati ya mji hasa hasa Deira
-Unaweza pia kujiajili kuuza nguo, mikoba ya wanawake, Viatu nk, ambapo itakubidi ujue machimbo ya wachina unapoweza kupata mzigo kwa bei nafuu...sehemu kama Baniyan Square shughuli hii inapigwa sana na waafrica.
-Kuna wa Wabongo wengi pia maeneo kama Etisalat wanapiga shughuli ya kuuza mishikaki, vitumbua nk.
-Kama wewe ni risk taker unaweza pia kupiga deal la kuuza pombe; kikubwa ni kujua chimbo la kupata mzigo zaidi Sharjah na sehemu ya kuuzia. Hii kazi inalipa sana.
Mwisho kwa mtu anayewaza kutoka nje ya nchi Dubai ni sehemu ya kufikiria kuanzia kabla ya kuwaza kwenda kuishi katika taifa kubwa kama [emoji631].
Maisha ya Dubai na Bongo binafsi sikuuona utofauti mkubwa sana.
Next time nitakuelezeeni namna ya kufika USA na naamini kila mtu anapenda sana. Kwa kila mwaka huwa nasaidia walau watu 2 kufika USA na huu ni mwaka wa 3 nafanya hivyo.
“Aquila non capit muscas”