Kama una ndoto ya kwenda Ulaya, Marekani, Canada n.k, pitia uzi huu


Sasa diamond alienda kabla ya pesa au baada ya pesa?? Sio Diamond wa Mbagaalaaaaa, Yemi alade amenyimwa Canadian visa kwakua aliomba akiwa hajulikani

Kama una pesa kuingia n kutoka kwao ni pesa na ndio wanapenda hao watu sana ndio maana wamewapa kipaumbele nchi za Asia kwakua wana hizo pesa za kuingia nakutoka

Nitakufunza hadi uelewe, nitaacha ukirusha mtu wa 4m pale YYZ
 
Acha uongo, wamarekani wengi wanakuja Afrika kutafuta ajira za uhakika.

🤣 🤣 kwa kazi gani zilizopo Afrika? Wamarekani hata siku moja hawaondoki US kwa kusema wanaenda kutafuta kazi nje ya nchi. Kazi nimejaa tele hapa. Ila hizo nchi zingine ndo wanajazana hapa from China, Russians to Europeans.

Kuna more that 11M open positions in the US right now.
 
Yani wewe unaona Canada hatari? Mshamba sana Wewe jamaa, hapo Montreal Quebec city Watoto wa Tandika wamejaa kibao wamemwagwa na meli na hata mia hawakuwa nayo, hao Wacanada walikuwa wapi?

Jinga sana wewe jamaa.
Story za kunwaga na meli za miaka ya 90 hazifanyi kazi kwa sasa

Mm nachotaka ww urushe mtu YYZ kwa 4m hapo nitaacha kukupa somo
 
Wamarekani wanajazana hapa bongo kutoa huduma ya kuendesha Bodaboda.
 
Nashukuru sana kwa maelezo mazuri
 
Labda anachanganya na volunteers wa peace corps.
 
Ila wakuu tuwe serious kidogo, hzo USD 25000 Mimi kijana nnayemakemake ntaifikisha lini kwa mkupuo niweze kwende huko majuu! Ni kweli wote wanaoenda huko wanakua na hyo hela? Sitaki kubisha sababu sijawah kufika nikashuhudia lakin kiuhalisia hapana haiwezekani maisha yetu kibongobongo tunayajua majority kushika milioni moja tu kwa mkupuo ni kasheshe. Sasa zifike kumi ishirini mpaka hamsini sijui sitini hapana,
Naamini kutakua na namna nyingne inatumiwa licha ya kuwepo hzo taratibu za USD 25000, tuambiane njia nyingne tufuate hzo hela nyingi sana jamani na mbele tunataka kwenda
 

$25,000 si wamesema ukiwa nayo huna haja ya kuondoka TZ inakufanya kuwa Mo Dewj au Azam.

Wasichojua ni kuwa $25,000 kwa kupiga kazi unaipata ndani ya miezi 6 wengine miezi 4 tu wakati kwa TZ ni miaka 5
 
WEZIO WANA TUMIYA DAWA KWENDA USA NA HAWAONEKANI NA HAWALIPI NAULI MJINI SHULE

Sent from my SM-G965F using JamiiForums mobile app
 
Hivi kwani hii taarifa ya kwamba ukishinda green card unalipiwa kila kitu nauli sijui na makazi ukifika US huwa mnaitoa wapi

Mkuu ukishinda green card kuna gharama za hapa na pale zinakusubiri kama medical fee, visa fee utalipia pale ubalozini ukienda kwenye interview, nauli, green card yenyewe, pamoja na gharama za kujikimu kimaisha US huku ukiwa unajitafutia kazi

Hizi fursa hazitufai watoto wa wakulima ndugu yangu labda wazazi wetu wauze mashamba
 

UNITED STATES OF AMERICA NDIO NCHI INAYOONGOZA KWA UBORA

Mimi nimeshangaa pia anavyozipamba nchi za pembezoni badala ya USA the SuperPower.

Ukiona nchi inalinganishwa kimaisha a kibiashara kama uswshilini Kariakoo basi yajieleza halisi ilivyo.

Nchi ambayo ni ngumu sana kupata visa ni Marekani, hii ni kutokana na udhibiti wa wahamiaji kutokana ns wimbi.la wahamiaji kuwa chaguo la kwanza kabisa kwa wahamiaji.

Marekani ni nchi ambayo pamoja na uthibiti mkali wa idara ya uhamiaji, lakini mtu akishaingia kwenye territory yake hasumbuliwi tena kama zilivyo nchi za Ulaya na Asia.

Naijadili kipana nchi hii nchi na ukitaka kuuliza cho chote niulize maana ninapoandika hivi nipo safarini nchini Marekani, na nilishasoma na kufanya kazi sana huku, hivyo hakuna wa kunidanganya.

Upatikanaji wa kazi bila security of life sipendekezi sababu mtu anakuwa anaishi kwa kujifichaficha na uoga jambo ambalo kwa Marekani halipo.
 

Preach. Security of life is the key word. Acha waende huko vichochoroni kuwa watumwa.
 
Pesa itumikayo kupima thamani ya uchumi duniani ni dollar, na pesa mama itumikayo to convert thamani ya Sarafu duniani ni dollar.

Soko kuu la pesa lipo New York, hata pesa za bongo zinapobadilishwa na kuhamishiwa kwa bank nyingine hupitia financial institute ya New York , Marekani.

Pesa pekee ambayo hupokelea kila nchi duniani ni dollar.

Kwa hoja hizo chache kati ya nyingi ambazo sijazitaja kiuchumi nchi bora duniani ni Marekani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…