Acha wavune utajiri kadri watakavyo kwenye taifa la wajinga kisha waishi maisha ya anasa ambayo watanganyika wengi kamwe hawatakuja kuyaishi.
Binafsi mimi imefika stage mpaka akili yangu imeozea kabisa kuona hii familia ikitapanya kodi za watanzania na wala sishtuki wala kuumia.
Kinachoniumiza na kunichukiza zaidi ni kuona watanganyika wenzangu wanaitetea hii familia kila aina ya ushenzi na ushetani inaoufanya, kwanzia ufisadi mpaka mauaji kwenye taifa letu la tanganyika.
Hapa ilipaswa watanganyike wote kwa moyo wa dhati kabisa tuungane na kuwakemea hawa majizi wanaoishi maisha ya anasa kwa kuwaumiza wanainchi, pengine wangeona aibu na kupunguza huu ufisadi wanaoufanya...
.. Ila sasa badala yake watanganyika baadhi yetu ndio kwanza wanashinda mitandaoni kuwatetea hii familia ya majizi na watesi wetu kwa sababu tu za kufanana nao kiimani au kwa ujira mdogo usiotosha hata kununua bando.
Nafikiri hata Abdul mwenyewe akionaga jinsi anavyotetewa na watu huku mitandaoni anakuwa na moyo mweupe kabisa na wala hajioni ni mwenye hatia, kwa ufupi tu hasumbuliwi kabisa na guilty conscience.