Kama Wanasimba tunajiamini tuna timu imara, kwa nini tunaombea tukutane na Al Ahly Tripoli, siyo TP Mazembe au Orlando Pirates?

Kama Wanasimba tunajiamini tuna timu imara, kwa nini tunaombea tukutane na Al Ahly Tripoli, siyo TP Mazembe au Orlando Pirates?

Acha dharau. Timu imeingia robo fainali misimu mitatu, wewe unadhani tunashindwa kuingia nusu fainali?.
 
Hakuna anaemkumbuka mtesekaji bora anakumbukwa yule aliepata ubingwa na haijalishi umepitia wapi kuupata.
 
Si tunajiamini kuwa Simba SC ni Timu Bora kabisa na tumepita CAFCC Jana kwa uwezo wetu na tuna Jeuri ya Kucheza na Timu yoyote Afrika sasa kwanini karibia 99% ya Wanasimba wanaombea wakutane na Al Ahly Tripoli ya nchini Libya na kamwe siyo TP Mazembe ya Congo DR au Orlando Pirates ya South Africa?

Tukisema ukweli kuwa kwa Kiwango cha Simba SC kwa sasa na kwa aina ya Wachezaji tulionao pamoja na Uwekezaji wetu mchanga kwa hizi Timu Tatu ambazo moja wapo tutacheza nao Simba SC 'hatutotoboa' kwenda Nusu Fainali ya Shirikisho mnanitukana na mnatutukana tuliowazidi Upeo, Maono na Jicho Kali la Uchambuzi wa Michezo ( hasa Mpira wa Miguu wa Tanzania ) na Masuala mengine.

Ninasisitiza hapo ndiyo mwisho Wetu!!!!
Kwani liver sio timu imara? Mbona walikuwa wanaomba wakutane na benfica na sio real madrid?
 
Ukiitwa mpumbavu uone unatukanwa na kumbe unastahili.

Level ya Simba ni robo fainali, huko kwengine ni majaliwa tu. Si lengo.

Taratibu inavyoenda na kushiriki mara kwa mara ndivyo watazidi kutanua malengo yao.

Hivi unasikilizaga hata press za afisa wa habari wa Simba au umekalia kijiweni na wenzio wa darasa la saba?

Kwa mujibu wake, Simba iliazimia kufika robo fainali na ndo' kitu walichokuwa wanaota na kukiimba kwa wachezaji.

Lengo limetimia.

Au hujui malengo huwa yanawekwaje?

Timu inajipima kwa mabavu yake ya budget na uzoefu. Timu kama Simba haiwezi ikaweka malengo sawa na Al Ahly au Mamelodi.

Hao wakiishia robo ni dhihaka wakati kwetu ni fahari.

Kusema hii Simba imelenga kubeba ubingwa ni kuwa na funza kichwani, labda kama michezo yote itachezwa Benjamin Mkapa.

Umfukuze Pablo kwa kutokufika nusu fainali kwa uwekezaji gani huo? Bajeti ya timu nzima ya Simba kwa mwaka, wakina Pyramid wanasajilia mchezaji mmoja.

Achilia mbali uhakika wa kushinda game away ni kutiatia maji, ukifanikiwa ni draw against teams like USGN.

Hiyo Robo au nusu unapita kimiujiza?


Pathetic.
Malengo ya Simba Sc ni robo fainali okay nakubali, nyinyi Yanga mna ndani ya hii miaka mitano mlikuwa na malengo gani?
 
Mpaka sasa bado sijaona Wachezaji bora na mahiri ndani ya Simba SC kwa Msimu huu wa kufikia Viwango vya Wachezaji ninaowapenda na kuwakubali wa Yanga SC kama Yanick GENTAMYCINE Bangala, Khalid GENTAMYCINE Aucho na Fiston GENTAMYCINE Mayele.

Kama Simba SC katika Draw ya Leo (Jumamne) tutapangwa na Magwiji na Majabali akina TP Mazembe na Orlando Pirates nashauri / napendekeza tuachane na Utani wetu wa Simba na Yanga au kuona Aibu na tuwaombe Yanga SC watupe hawa Wachezaji wao Watatu tajwa ili Watusaidie kwani kwa hawa tulionao naona zile Goli Tano Tano za Kufungwa zinaenda Kurejea tena Msimbazi.

Kwa wale Mazuzu, Washamba na Mapopoma ambao huenda miaka ya mwishoni mwa Tisini bado mlikuwa katika Zipu za Baba zenu ni kwamba hata Yanga SC nao walivyofika hatua fulani ya Michuano hii ya Kimataifa walituomba Simba SC Wachezaji wetu ambao walikuwa Mahiri kipundi hiko akina Alphonce Modest ( Beki ), Shaaban Ramadhan ( Kiungo ) na Monja Liseki ( Mshambuliaji ) ambapo waliwasaicia vizuri tu Yanga SC sema bahati haikuwa Kwao.

Ukweli unauma ila ni dawa iponyayo.
 
GENTAMYCINE nitawalaumu sana CAF na hata nitakuwa tayari kukata 'Rufaa' Kwao kama katika 'Draw' ya leo watatupanga na Timu 'Dhaifu' ya Al Ahly Tripoli ya Libya kwani nataka Kuuona Uwezo wa Simba SC ambayo inasifiwa 'Kipuuzi' Mitandaoni kwa Kupangwa na Majabali / Magwiji wa TP Mazembe ( Congo DR ) au Orlando Pirates ( South Africa )

Si tunajiamini? Basi tuwe Wavumilivu!!!!!
 
Aisee!
Mbona wewe Genta mwenyewe huwa unatudanganya kuwa Simba inashindaga kwa nguvu ya ndumba mnazozifanya kwenye kamati yenu ya kimafia?. Halafu leo unatamani kuona uwezo wa Simba ikicheza kwa uwezo wake wa uwanjani?.

Kumbe huwa ni mikwara tu
 
Malengo ya Simba Sc ni robo fainali okay nakubali, nyinyi Yanga mna ndani ya hii miaka mitano mlikuwa na malengo gani?
Hopeless nani kakuambia kuwa Malengo ya Simba SC ni kufika Robo Fainali?

Fuatilia Kauli za CEO Barbara Gonzalez, Mwenyekiti wa Bodi Salim Abdallah na Mwenyekiti wa Wanachama Mustafa Mangungu walipokuwa Wakimtambulisha huyu Kocha wa sasa wa Simba SC Pablo Franco Martin.

Halafu GENTAMYCINE nikiwadharau kuwa hamna Akili mnanikasirikia na kuona kuwa Ninawatusi.
 
Dah ila Popoma viongozi wa simba waliumiza sana EGO yako ulipowashauri wakate kucheza saaa nne wakakupuuza....Mimi kiukweli naombea sana simba tupoteze robo fainali ili maneno yako yatimie uje kujisifu kwamba wewe ni talented fella..ANYWAY ILA KAMA TUTAPITA KWENDA NUSU BASI MKUU USISITE KUJA NA ZILE ID ZAKO FEKI KAMA 40 ZA ZIADA KUJA KUSHANGILIA MANA HUNAGA AIBU WEWE ..USHA MTUKANAGA SAN AJAMES KOTEI UKAJISAHAU BAADAYE UKAANZA KUMSIFIA UKIDAI ULIMKUBALIGI SANA..JINGA MKUBWA WEWE
 
Majini yako yatatusaidia.
Na 'Nitaroga' tufungwe hadi mniombe Radhi. Naanzia na Mechi ya Keshokutwa na Coastal Union FC kule Tanga ambako nitachezesha 'Kiuchawi' ili tutoke tu 'Sare' huku nikifikiria je, Mechi yetu na Police Tanzania nayo 'niichezeshe' ili tutoke 'Sare' au 'tufungwe' tu kabisa?

Endeleeni Kunitukana mtanitambua Ok?
 
Back
Top Bottom