Kama Wanasimba tunajiamini tuna timu imara, kwa nini tunaombea tukutane na Al Ahly Tripoli, siyo TP Mazembe au Orlando Pirates?

Acha dharau. Timu imeingia robo fainali misimu mitatu, wewe unadhani tunashindwa kuingia nusu fainali?.
 
Hakuna anaemkumbuka mtesekaji bora anakumbukwa yule aliepata ubingwa na haijalishi umepitia wapi kuupata.
 
Kwani liver sio timu imara? Mbona walikuwa wanaomba wakutane na benfica na sio real madrid?
 
Malengo ya Simba Sc ni robo fainali okay nakubali, nyinyi Yanga mna ndani ya hii miaka mitano mlikuwa na malengo gani?
 
Mpaka sasa bado sijaona Wachezaji bora na mahiri ndani ya Simba SC kwa Msimu huu wa kufikia Viwango vya Wachezaji ninaowapenda na kuwakubali wa Yanga SC kama Yanick GENTAMYCINE Bangala, Khalid GENTAMYCINE Aucho na Fiston GENTAMYCINE Mayele.

Kama Simba SC katika Draw ya Leo (Jumamne) tutapangwa na Magwiji na Majabali akina TP Mazembe na Orlando Pirates nashauri / napendekeza tuachane na Utani wetu wa Simba na Yanga au kuona Aibu na tuwaombe Yanga SC watupe hawa Wachezaji wao Watatu tajwa ili Watusaidie kwani kwa hawa tulionao naona zile Goli Tano Tano za Kufungwa zinaenda Kurejea tena Msimbazi.

Kwa wale Mazuzu, Washamba na Mapopoma ambao huenda miaka ya mwishoni mwa Tisini bado mlikuwa katika Zipu za Baba zenu ni kwamba hata Yanga SC nao walivyofika hatua fulani ya Michuano hii ya Kimataifa walituomba Simba SC Wachezaji wetu ambao walikuwa Mahiri kipundi hiko akina Alphonce Modest ( Beki ), Shaaban Ramadhan ( Kiungo ) na Monja Liseki ( Mshambuliaji ) ambapo waliwasaicia vizuri tu Yanga SC sema bahati haikuwa Kwao.

Ukweli unauma ila ni dawa iponyayo.
 
GENTAMYCINE nitawalaumu sana CAF na hata nitakuwa tayari kukata 'Rufaa' Kwao kama katika 'Draw' ya leo watatupanga na Timu 'Dhaifu' ya Al Ahly Tripoli ya Libya kwani nataka Kuuona Uwezo wa Simba SC ambayo inasifiwa 'Kipuuzi' Mitandaoni kwa Kupangwa na Majabali / Magwiji wa TP Mazembe ( Congo DR ) au Orlando Pirates ( South Africa )

Si tunajiamini? Basi tuwe Wavumilivu!!!!!
 
Aisee!
Mbona wewe Genta mwenyewe huwa unatudanganya kuwa Simba inashindaga kwa nguvu ya ndumba mnazozifanya kwenye kamati yenu ya kimafia?. Halafu leo unatamani kuona uwezo wa Simba ikicheza kwa uwezo wake wa uwanjani?.

Kumbe huwa ni mikwara tu
 
Malengo ya Simba Sc ni robo fainali okay nakubali, nyinyi Yanga mna ndani ya hii miaka mitano mlikuwa na malengo gani?
Hopeless nani kakuambia kuwa Malengo ya Simba SC ni kufika Robo Fainali?

Fuatilia Kauli za CEO Barbara Gonzalez, Mwenyekiti wa Bodi Salim Abdallah na Mwenyekiti wa Wanachama Mustafa Mangungu walipokuwa Wakimtambulisha huyu Kocha wa sasa wa Simba SC Pablo Franco Martin.

Halafu GENTAMYCINE nikiwadharau kuwa hamna Akili mnanikasirikia na kuona kuwa Ninawatusi.
 
Dah ila Popoma viongozi wa simba waliumiza sana EGO yako ulipowashauri wakate kucheza saaa nne wakakupuuza....Mimi kiukweli naombea sana simba tupoteze robo fainali ili maneno yako yatimie uje kujisifu kwamba wewe ni talented fella..ANYWAY ILA KAMA TUTAPITA KWENDA NUSU BASI MKUU USISITE KUJA NA ZILE ID ZAKO FEKI KAMA 40 ZA ZIADA KUJA KUSHANGILIA MANA HUNAGA AIBU WEWE ..USHA MTUKANAGA SAN AJAMES KOTEI UKAJISAHAU BAADAYE UKAANZA KUMSIFIA UKIDAI ULIMKUBALIGI SANA..JINGA MKUBWA WEWE
 
Majini yako yatatusaidia.
Na 'Nitaroga' tufungwe hadi mniombe Radhi. Naanzia na Mechi ya Keshokutwa na Coastal Union FC kule Tanga ambako nitachezesha 'Kiuchawi' ili tutoke tu 'Sare' huku nikifikiria je, Mechi yetu na Police Tanzania nayo 'niichezeshe' ili tutoke 'Sare' au 'tufungwe' tu kabisa?

Endeleeni Kunitukana mtanitambua Ok?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…