Mpaka sasa bado sijaona Wachezaji bora na mahiri ndani ya Simba SC kwa Msimu huu wa kufikia Viwango vya Wachezaji ninaowapenda na kuwakubali wa Yanga SC kama Yanick GENTAMYCINE Bangala, Khalid GENTAMYCINE Aucho na Fiston GENTAMYCINE Mayele.
Kama Simba SC katika Draw ya Leo (Jumamne) tutapangwa na Magwiji na Majabali akina TP Mazembe na Orlando Pirates nashauri / napendekeza tuachane na Utani wetu wa Simba na Yanga au kuona Aibu na tuwaombe Yanga SC watupe hawa Wachezaji wao Watatu tajwa ili Watusaidie kwani kwa hawa tulionao naona zile Goli Tano Tano za Kufungwa zinaenda Kurejea tena Msimbazi.
Kwa wale Mazuzu, Washamba na Mapopoma ambao huenda miaka ya mwishoni mwa Tisini bado mlikuwa katika Zipu za Baba zenu ni kwamba hata Yanga SC nao walivyofika hatua fulani ya Michuano hii ya Kimataifa walituomba Simba SC Wachezaji wetu ambao walikuwa Mahiri kipundi hiko akina Alphonce Modest ( Beki ), Shaaban Ramadhan ( Kiungo ) na Monja Liseki ( Mshambuliaji ) ambapo waliwasaicia vizuri tu Yanga SC sema bahati haikuwa Kwao.
Ukweli unauma ila ni dawa iponyayo.