Mungu ni stories tu, hakuna anayeweza kuthibitisha yupo.
Kiranga wewe ukiandiko hivo wala heart beat zangu haziathiriki nakujua, ingawa najua siku zinazonga, sasa hivi wewe possibly age yako ni 45+,kuna sehemu wote tunaelekea.
Acha ziwe story ,ndugu yangu ni bora usingesoma, kama hiyo elimu imekufanya useme hakuna Mungu haya. Kitu kimoja nikuambia kama Mungu ana mpango na wewe kuna siku utakiri ya kuwa yupo, ila kwa jinsi unavyoendelea kuukana uwepo wa Mungu ndungu yangu kuwa makini asije akakukataa.
Rehema ya Mungu ikufunike umjue yeye na kumtumikia. Maswali yako hayabadiliki nilishakujibu ila hutaki kukubali majibu labda nijubu swali lako leo kwa manufaa ya wengine ambao hawakuwa kuona swali lako na jibu langu.
Mara nyingi umekuwa unataka prove kwamba Mungu yupo
1. Moja ya jibu langu nilikwambia upepo upo, na hata wewe unajua upepo upo,je kuna mwansayansi amefanya experiment ya kuprove uwepo wa upepo?Upepo upo,hatuwezi kuuona ila tunaweza kuona uwepo wake kutokana na madhara yake mazuri na mabaya kwa mfano upepo unapovuma you can feel it, utaona matawi ya miti yanatikisika ila hutaweza kuuona upepo na kuprove kwamba upo zaidi ya kutumia kazi zake na kunufaika nao kama kutengeneza umeme.
Mungu yupo,haonekani kwa macho ya nyama,kama ni mtu mzima kiroho unaweza ukafeel uwepo wake ila kwa watu wazima wa umri ila wachanga kiroho kama wewe huwezi na ndiyo sababu kwa sababu hamuwezi mnapinga.
Mungu ni roho sasa wewe unataka kufanya experiment ukiwa mwilini kuprove kwamba roho inaexist, utangojea sana. Labda kwa elimu yako na ufahamu wako kuna wanasayansi walishawahi kuiona roho ya mwanadamu au kuishika?
Kwanza unaanzaje kumuweka Mungu maabara,unjua aliposema " I am that I am"/"Mimi ni niko ambaye niko" maana yake Mungu anaweza akawa katika form yeyote atakayotaka,sasa unaanzaje kumfanyia experiment.Dunia hii kazi tunayo.
2.Kuhusu kuprove uwepo wa Mungu niliwahi kujibu kwamba siku robot zilizotengenezwa na wanadamu zikiweza kufanya experiment ya kuprove kwamba "mwanadamu" aliyezitengeneza roboti yupo basi uje utuombe tunaoamini kwamba Mungu yupo nasi tufanye experiment.Point yangu hapa ni kwamba robot inafanya au inamfanana mwanadamu kwa sehemu tu,the same level ya ufahamu ya Mungu iko juu sana kuliko wanadamu, kwa hiyo hakuna mwanadamu atakayeweza kufanya experiment ya kuprove kwamba Mungu yupo kama nilivyosema robot haiwezi kuprove kuna mwanadamu.
Ila tunasema Mungu yupo kwa sababu tunafeel uwepo wake(watu wazima kiroho) na tunaona kazi zake,kama wagonjwa kuponywa,mapepo kutoka,na menginen mengi.
Wewe na wenzako majapokuwa na elimu ya juu sana ya mambo ya dunia, lakini mmekosa kumjua Mungu that is why nikasema ndugu yangu, kama elimu yako imekufanya useme hakuna Mungu ni bora usingesoma.Unaweza usinielewe kwa sasa ila siku nafsi yako ikitengana na mwili utajuta na hautakuwa na muda wa kurekebisha makosa yako.
Mungu akusaidie ,macho yako ya rohoni yatiwe nuru uweze kuona.