Ambacho sijafafanua ni kipi?
Unaelewakwamba sijasemakwamba kwenye polygon huwezi kupata pembe tatu, nimesema hakuna pembe tatu ambayohapohapo nipembe tatu na pembe sita?
Unaelewa tofauti?
Kwanza unaelewa kwamba silaumu, nakosoa kutokuwepo kwa logical consistency?
Unaelewa hilo?
Pili, unasema yote hayo ni matendo ya binadamu, Mungu alipokuwa anaumba ulimwengu, kabla binadamu hajaumbwa, alishindwa kuumba ulimwengu ambao binadamu hana matendo hayo na hawezi kuwa na matendo hayo?
Hujajibu swali hili, nimeshaliuliza kwakujua utakujana point hii. Hujajibu.
Unaweza kuthibitisha Mungu yupo?
Wewe leo una free will ya kurudi mwaka 1982?
Mnajichanganya, mara mnasema binadamu hajikomboi mwenyewe, ila kwa neema ya Mungu tu anakombolewa, mara mnasema binadamu ana uchaguzi mwenyewe.
Kipi ni kweli hapa? Ana freewill na ana contraol destiny au anapata kumjuaMungu na kwenda peponikwa neema ya Mungu tu?
Ambayo hujaijibu.
Kama mazuri ni ushahidi kwamba Mungu yupo, maovu ni ushahidi kwamba hayupo?
Unaweza kuthibitisha kwamba mazuri haya hayatokani na kingine chochote zaidi ya huyo Mungu?
Mimi naweza kusema angekuwepo, asingeweza kuruhusu mabaya yawepo, na mabaya yapo, kwa hiyo hayupo.
Wewe unaweza kuniambia imekuwaje Mungu huyoawepo halafu aumbe ulimwengu unaoruhusu mabaya, wakatialikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao hauruhusu mabaya?