Kama Wizara ya Maliasili na Serikali hawana mkakati wa kutokomeza kunguru weusi, tuwape tenda wachina

Ogopa sana kunguru wanamagonjwa mengi ..coz wanasafiri umbali mrefu na kula kila Aina ya uchafu
Mariposa ana mapenzi sana na hawa ndege sijui kwa nini ila sio ndege wastarabu kabisa hata ukiwaheshimu hawakueshimu sana sana watakuaibisha kama vile mtoto mwenye malezi mabovu
 
Wazo la kuwashughulikia kunguru weusi limenivuta nisome.Baada ya kusoma historia ya uongo kuhusu kunguru hao nasimama hapa hapa mbele siendi.
Hapa siyo urus
 
Kuna mshkaji wangu anaishi karibu na maeneo yadampo nyumbani kwake amepanda miti Basi kunguru wakiokota mizoga dampo wanakuja kuangushia nyumbani kwake. kilasiku anakazi yakutafuta mizoga ilio achwa na kunguru aifukie isinuke
 

Watilie sumu humo. Unga mkono jitihada za kupunguza hawa ndege waharibifu.
 
Yani ulivomalizia hapo chini🤣🤣🤣😂
 
Nipo tayari kulipa tozo KUNGURU waondoshwe. Kwa Bahati mbaya sana tukiendelea kuwachekea wakafikia kwenye Mbunga zetu za wanyama watakula ndege wote huko maaana watashambulia Viota vyao na hatimaye tutapoteza Urithi.
Dar es salaam tayari ndege wengine wooooote kunguru ashatafuna na hata akionekana mmoja mmoja atafukuzwa hadi uvunguni akamatwe aliwe. Kwa kifupi hawa Kunguru ni FISI WANAORUKA
 
Wanakula kweli vifaranga wa ndege wenzao! Serikali hill nalo wakalitazame! Wizara husika ilete mpango wa kutokomeza hawa kunguru
 
Aahaaaaaa
 
Wanakula kweli vifaranga wa ndege wenzao! Serikali hill nalo wakalitazame! Wizara husika ilete mpango wa kutokomeza hawa kunguru
Hapo Kwenye vifaranga dah! wanakula vifaranga vya kuku mpaka nakata tamaa kufuga. Wanabeba mpaka vyombo vya plastic ukiacha kwenye karo njee. Sabuni pia wanabeba. Ni kero kwa kweli .
 
Hawa kunguru waliletwa Toka Zanzibar, walisema wanasaidia kufanya usafi. Kumbe walikuwa wanatuletea tatizo kubwa, SI kweli waliletwa wakati Lowassa yupo madarakani kwani walikuja mapema zaidi.
Kilikuwa na kunguru wenye ufito mweupe lakini Sasa hivi wametoweka kabisa.
 
Wanakera sana
 
Wanazidi kuhama kuelekea Magharibi ya Tanzania kuwakimbia kunguru weusi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…