Kama Wizara ya Maliasili na Serikali hawana mkakati wa kutokomeza kunguru weusi, tuwape tenda wachina

Kama Wizara ya Maliasili na Serikali hawana mkakati wa kutokomeza kunguru weusi, tuwape tenda wachina

Ogopa sana kunguru wanamagonjwa mengi ..coz wanasafiri umbali mrefu na kula kila Aina ya uchafu
Mariposa ana mapenzi sana na hawa ndege sijui kwa nini ila sio ndege wastarabu kabisa hata ukiwaheshimu hawakueshimu sana sana watakuaibisha kama vile mtoto mwenye malezi mabovu
 
Kuna mshkaji wangu anaishi karibu na maeneo yadampo nyumbani kwake amepanda miti Basi kunguru wakiokota mizoga dampo wanakuja kuangushia nyumbani kwake. kilasiku anakazi yakutafuta mizoga ilio achwa na kunguru aifukie isinuke
 
Ninapoishi kuna Minazi mingi ndio wamefanya makazi yao, nimewawekea maji kwenye chombo maalum baada ya hapo awali kua wanafungua bomba la nje wanakunywa maji na kuacha yanamwagika.

Mabaki ya chakula hua nawawekea sehemu maalum na wakishaniona naelekea hiyo sehemu wanakuja kwa kelele kali hua natafsiri wanafurahi na kuitana, wanabeba na kula kwenye nyumba zao,

Watu wengine wanaona kero makelele yao nikagundua kinachowasumbua ni kiu cha maji.

Watilie sumu humo. Unga mkono jitihada za kupunguza hawa ndege waharibifu.
 
Kama nchi ningeshauri tujifunze kushughulika na kero hata kama hazina madhara ya moja kwa moja!
Huko ulaya wenzetu huwa wanafanya oparesheni ya kuondoa paka, mbwa na ndege wasio natija!

Hata hapa kwetu sioni kama inashindikana kuwaondoa kitaalam hawa kunguru weusi!

Historia inasemekana wazo la kuleta mbegu ya hawa kunguru weusi lilifanyika katika utawala wa CCM chini ya waziri mkuu wa zamani EDWARD LOWASSA ambapo liligharimu bilion 7.5 Wakiwa na lengo kwamba Kunguru hawa weusi wangesaidia kula uchafu huko mahospitali!

Bahati mbaya maamuzi hayo yalifanyika pasipo utafiti wa kitaalam!
Kundi la kwanza lilimwagwa Zanzibar! Na baadae wakazaliana na wengine walisafili kuja Tanzania bara kwa kudandia meli na majahazi baharini!

Hivi sasa kunguru hawa ni kero kubwa sana kwa taifa na wananchi!
1. Wanapiga makelele baadhi ya makundi mahospitalini
2. Wanachafua mazingira ya miti na kujisaidia ovyo.
3. Wanaharibu miundombinu ya umeme na kusababisha ukosefu wa umeme kwa dharula (wanabeba vipande vya waya wanapotua kwenye nyaya za tanesco wanagonganisha waya transfoma zinazima-KERO)
4. Wanachafua nguo za wananchi zilizoanikwa juani!
5. Wanawasumbua sana walevi na wapenda nyama choma huko bar
6. Wana wanyea mav hasa wanapoona mtu kavaa vizuri hususan MTU akivaa nguo nyeupe au ya kung'aa
7. Wanapokonya chakula watoto wadogo
8. Wanaipua mboga jikoni na kula hata kama ilifunikwa
9. Wakifa Hawaozi haraka
10. Ni hatari kwenye baadhi ya injini hasa maeneo ya uwanja wa ndege

Kiufupi hawa kunguru weusi wana kero nyingi ambazo lazima serikali ifanye mpango mkakati kuwatokomeza kabla hawajaongezeka!

Kama serikali itashindwa basi tenda wapewe wachina watuondolee huu upuuzi unaozidi kuzaliana!

WATU WAZURI HUSHUGHULIKIA KERO ZA WATU ILI WAKUMBUKWE KWA MAZURI NA SI KWA MABAYA
Yani ulivomalizia hapo chini🤣🤣🤣😂
 
Nipo tayari kulipa tozo KUNGURU waondoshwe. Kwa Bahati mbaya sana tukiendelea kuwachekea wakafikia kwenye Mbunga zetu za wanyama watakula ndege wote huko maaana watashambulia Viota vyao na hatimaye tutapoteza Urithi.
Dar es salaam tayari ndege wengine wooooote kunguru ashatafuna na hata akionekana mmoja mmoja atafukuzwa hadi uvunguni akamatwe aliwe. Kwa kifupi hawa Kunguru ni FISI WANAORUKA
 
Wanakula kweli vifaranga wa ndege wenzao! Serikali hill nalo wakalitazame! Wizara husika ilete mpango wa kutokomeza hawa kunguru
 
Ninapoishi kuna Minazi mingi ndio wamefanya makazi yao, nimewawekea maji kwenye chombo maalum baada ya hapo awali kua wanafungua bomba la nje wanakunywa maji na kuacha yanamwagika.

Mabaki ya chakula hua nawawekea sehemu maalum na wakishaniona naelekea hiyo sehemu wanakuja kwa kelele kali hua natafsiri wanafurahi na kuitana, wanabeba na kula kwenye nyumba zao,

Watu wengine wanaona kero makelele yao nikagundua kinachowasumbua ni kiu cha maji.
Aahaaaaaa
 
Wanakula kweli vifaranga wa ndege wenzao! Serikali hill nalo wakalitazame! Wizara husika ilete mpango wa kutokomeza hawa kunguru
Hapo Kwenye vifaranga dah! wanakula vifaranga vya kuku mpaka nakata tamaa kufuga. Wanabeba mpaka vyombo vya plastic ukiacha kwenye karo njee. Sabuni pia wanabeba. Ni kero kwa kweli .
 
Hawa kunguru waliletwa Toka Zanzibar, walisema wanasaidia kufanya usafi. Kumbe walikuwa wanatuletea tatizo kubwa, SI kweli waliletwa wakati Lowassa yupo madarakani kwani walikuja mapema zaidi.
Kilikuwa na kunguru wenye ufito mweupe lakini Sasa hivi wametoweka kabisa.
 
Umeongea kitu muhimu sana mkuu, ni lazima tulinde uasili wetu ndio maana kuingia NZ au Australia wapo makini mno, kuanzia uhamiaji haramu mpaka vitu vya kuathiri uasili wao,pendekezo hizi borders zetu tuunde chombo kimoja cha kuratibu sio sasa kila mtu anafanya kazi independent,

utafiti wa kunguru hawa ulishafanyika miaka kibao nyuma huku na mpaka kukawa na mitego eti wategwe na zawadi kutolewa hasa kwa kiota chenye mayai!pale makumbusho ya taifa watu wakala pesa tu,tuingize eagles 🦅 ambao ni natural enemy wa kunguru,

Hawa watakomesha kabisa tatizo hili, hawa kunguru wametupotezea mno ndege wetu wa asili, Dar vitonga sasa ni adimu mno, shore hamna kabisa
Wanakera sana
 
Hawa kunguru waliletwa Toka Zanzibar, walisema wanasaidia kufanya usafi. Kumbe walikuwa wanatuletea tatizo kubwa, SI kweli waliletwa wakati Lowassa yupo madarakani kwani walikuja mapema zaidi.
Kilikuwa na kunguru wenye ufito mweupe lakini Sasa hivi wametoweka kabisa.
Wanazidi kuhama kuelekea Magharibi ya Tanzania kuwakimbia kunguru weusi
 
Back
Top Bottom