Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tatizo lenu mnachati sana.Hii ndio Taarifa mpya kwa sasa .
Taarifa zaidi zitaendelea kutiririka.
Magaidi wanaachwa kuandamana kweli? Sawa umuache MULLAH OMAR kuandamana.Wangeacha waandamane kuondoa ghadhabu.. au wanataka yale ya MKIRU?!
Huwezi kuchemsha maji huku umeziba kabisa kuzuia mvuke kutoka, afu ww ubaki salama.
Wananchi walio wengi Wana hasira juu ya matendo ya watawala waovu hawa.
Jiulize wewe hilo swali. Kelele nyingi sana mitandaoni afu vitendo zero kabisa. Mambo Sasa kafanya kwa vitendo, nyinyi vitendo vyenu vipo wapi?. Mnadaganya watoto wa wenzenu akati wewe,wenzako na watoto wenu mmejificha ndani. Shenzi kabisa.Hivi Mambosasa ana akili timamu?
Wanastahili kabisa kwa sababu walikuwa wanahamasisha uvunjaj wa amani nchini.UPDATE
View attachment 1617804
"Mbowe na wenzake watashtakiwa kwa makosa ya ugaidi kwa sababu kuna mtu ametupa ushahidi kuwa walipanga kulipua vituo vya mafuta jijini Dar na kuleta maafa makubwa," Lazaro Mambosasasa, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya DSM.
=====
Kamanda wa Polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam ACP Lazaro Mambosasa amesema wanawashikilia watu kadhaa wakiwemo viongozi watatu wa CHADEMA.
Viongozi wa CHADEMA wanaowashikilia ni pamoja na Freeman Mbowe ambaye ni mwenyekiti wa CHADEMA taifa, Godbless Lema na Boniface Jacob.
Amesema wanawashikilia viongozi hao kwa kuwa wanahatarisha usalama wa Raia na mali zao kwa kuwa Novemba 2 walipanga kuwatumia vijana kuchoma moto miundominu na vituo vya mafuta.
Aidha kwa usiku huu wanaendelea kuwatafuta watu ambao wanawashawishi vijana kushiriki maandamano ambayo Polisi wamesema ni ya Vurugu na si amani kwa kuwa wanaoshawishiwa ni vijana wavuta bangi.
Amesema hayo katika kipindi mubashara kilichorushwa na ITV.
PIA SOMA
= > Uchaguzi 2020 - Dar es Salaam: Watu watatu zaidi wakamatwa kuzuia maandamano
Mnakera sana, kelele nyingi sana humu. Shida ni nini, si uende ukaandamane.Eti vijana wavuta bangi! Imenikumbusha Gaddafi ndivyo alivyokuwa akisema wakati Libya inaanza kuanguka! Alisema ni vijana wamepewa madawa ya kulevya wafanye fujo na maandamano!
Hivi kwa mfano, ukawa umedhamiria kufanya kitu ambacho wakati mwingine (na si wakati wote), kinachukuliwa kuwa ni kinyume cha sheria, ikitokea ukashindwa kukitekeleza kwa sababu tu ya kuwekewa mazingira pingamizi, kisheria unakuwa huna hatia? Mfano ulidhamiria kwenda kuiba nyumbani kwa A, bahati mbaya ukakuta mazingira hayaruhusu, ukashidwa kuiba, je unakuwa huna hatia katika mazingira hayo, assuming umejulikana?Wamevunja sheria gani?
Njooni mtakutana na pira mpapaso.Mimi nimeshajiandaa na vijana wenzangu kama 70 hivi. Mabali na sisi Coaster kumi na mbili toka maeneo mengine ikiwemo Arusha ziko njiani muda huu.
Waendee kwenye majimbo yao wakaone walipokosea waache kuja kutusumbua huku kama ndio tulipo wachaguachadema acheni wananchi wapuuzi wa nchi hii waisome namba, mnajitoa kwa ajili yao ila hakuna support yeyote. kiufupi huwezi kumpigania mtumwa ambaye aliyozea utumwani.
Mambosasa ni SACP, sio ACP.UPDATE
View attachment 1617804
"Mbowe na wenzake watashtakiwa kwa makosa ya ugaidi kwa sababu kuna mtu ametupa ushahidi kuwa walipanga kulipua vituo vya mafuta jijini Dar na kuleta maafa makubwa," Lazaro Mambosasasa, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya DSM.
=====
Kamanda wa Polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam ACP Lazaro Mambosasa amesema wanawashikilia watu kadhaa wakiwemo viongozi watatu wa CHADEMA.
Viongozi wa CHADEMA wanaowashikilia ni pamoja na Freeman Mbowe ambaye ni mwenyekiti wa CHADEMA taifa, Godbless Lema na Boniface Jacob.
Amesema wanawashikilia viongozi hao kwa kuwa wanahatarisha usalama wa Raia na mali zao kwa kuwa Novemba 2 walipanga kuwatumia vijana kuchoma moto miundominu na vituo vya mafuta.
Aidha kwa usiku huu wanaendelea kuwatafuta watu ambao wanawashawishi vijana kushiriki maandamano ambayo Polisi wamesema ni ya Vurugu na si amani kwa kuwa wanaoshawishiwa ni vijana wavuta bangi.
Amesema hayo katika kipindi mubashara kilichorushwa na ITV.
PIA SOMA
= > Uchaguzi 2020 - Dar es Salaam: Watu watatu zaidi wakamatwa kuzuia maandamano
Magufuli ameaibika?Watu wa Bengazi aliwaita mende au panya. Magufuli anaenda kuabika kuanzia kesho.
Kesho tena? Kwa nini isiwe leo?Kesho tutawatoa kwa maandamano
Hawa wapinzani fake vibaraka ni wakubinya kabisa wakaishi cages huko wajinga sanaHicho wanchofanya ni more dangerous zaidi, Bora wangewakamata wakati wa maandamano.
Inanikumbusha story moja " Kuna baunsa mmoja alikua ananyanyasa wanakijiji. Siku moja akatokea kijana mdogo tu akamwambia kesho saa Saba mchana nitazibinya pumbu zako mpaka ulie" Sasa Yule baunsa akaanza kumkimbiza Yule kijana.
Kijana akakimbilia nyumbani kwa babu yake " babu akamuliza baunsa kulikoni unakimbizana na mtoto" Baunsa akajibu mjukuu wako kasema kesho atanibinya pumbu" Babu akamuliza kwani kesho imefika? Kwa ameshakubana pumbu? Baunsa akamjibu hapana.
Babu akamwambia Baunsa subiri kesho akikushika Kama alivyoahidi ndio umkamate umtie bakora.
Hadhithi inatufundisha tusiwe tunaweza mechanically/ robotically, na Kuna wakati subira huvuta heri.
Hatukujifunza wakati wa Maandamano ya Mange Kimambi?
Hauandamani tena?Yana mwisho hayo.
Twendeni tu.