Uchaguzi 2020 Kamanda Mambosasa: Mbowe na wenzake kushtakiwa kwa makosa ya ugaidi, walipanga kulipua vituo vya mafuta

Uchaguzi 2020 Kamanda Mambosasa: Mbowe na wenzake kushtakiwa kwa makosa ya ugaidi, walipanga kulipua vituo vya mafuta

Wewe uliuona uchaguzi tar 28? Tuache kuwa wanafiki. Demokrasia nchi hii imeshafutika angalau kidogo labda tokea uchaguzi wa 2015 labda lkn mwaka huu ni aibu sana. Kama unanufaika na yanayofanyika nchinu kwasasa nakutakia kila la kheri nyie ndio mmeshika makali. Nchi yenu hii fanyeni mtakavyo.
Niliona na mimi nilishiriki na pia nilimsikia Lissu saa tisa mchana na yeye akisifu kama mimi kuwa ulikuwa mzuri ila masaa 4 baadae uchaguzi ukawa mbaya nahisi CDM wanapelekeshwa,kwani hawakuwasiliana na Mdee kuwa wamekamata kura zipo nje ya kituo hapo ndipo napata mashaka ni nini kilichowabadilisha wakati walituaminisha uchaguzi ni mzuri na wakati wa Kampeni walisema hakuna kuiba tutazilinda kura kivyovyote watazilinda kwenye majumuisho yanapotangazwa wakagoma kuwa hukuwa na huru.

Changamoto zipo sikatai na sipingi hilo ila ukumbuke namba zako zilinakiliwa pale ulipokuwa unapiga kura karatasi ilipochanwa ,tunahakika gani kama hizo karatasi zilizokutwa nje zilikuwa zinafanana vipi kwann walichoma ushahidi .

Moja ya karatasi nilipoingalia niligundua haina tick chumba chochote ila aliekuwa anaongea alisema inakura ya Magufuli karatasi hiyo nyuma ilikuwa na mistari mieupe tofauti na nilizoziona za Raisi nilizopiga mimi zilikuwa na rangi ya bluu nyuma,ndugu tafuta ukweli kuna watu wanajua kupika vitu.

Kama matokeo walikuwa nayo basi kulikuwa hakuna haja ya kuwazuia mawakala kuingia ndani ,nina imani kura zilipigiwa ndani nakuhesabiwa kituoni kama wizi kuna watu walikuwa wanafosi katika ngazi ya majimbo ila sio Tume hiyo lazima ilikuwepo ila huku sikuona nilipo mimi.

Huwezi kusema tume sio Huru wakati na yeye anapokea matokeo kutoka kwenye vituo kimeo kipo kwa wakurungenzi ,hata CAG anapata ripoti kwa wengine yeye ni sahihi tu ndio ilivyo.

Mwaka huu Lissu hakuwepo hivyo hajui mengi ndani ya nchi hii ni mtu aliyesikia kama walivyo wengine huo ughaibuni kuwa Magufuli ni Dikteta lakini kiuhalisia Magufuli kasaidia wengi kupata haki kasemehe wengine waliomkosea na hakuonesha chuki kuwachagua tena kugombea Ubunge ,

Hivyo kutokumjua Magufuli na wananchi wake wana mapenzi gani nae na wanapenda nini ,Lissu ilimwaminisha anaweza kumtoa madarakani Magufuli kitu ambacho kimemuumiza hakutarajia.

Demokrasia sio wapinzani kwenda Bungeni au kila chaguzi kushinda .

Asante.
 
Wewe uliuona uchaguzi tar 28?
Wewe uliuona? Ni yeye...
117356827_101995408283720_1506539019369461386_n.jpg
 
Kudhamiria ni kosa?

Unapimaje kudhamiria?

Je, mtu akidhamiria kuandamana halafu akaahirisha dakika ya mwisho napo amefanya kosa?

Unajuaje huyu kadhamiria na huyu hajadhamiria?

Unahakikishaje wameshikiliwa kwa haki na si kisiasa?

Kesi ya kudhamiria unawezaje kuthibitisha Polisi hawawabambikii watu dhamira za uongo?

Unaweza vipi kumzuia Polisi anayekuchukia kukuzushia kesi ya kudhamiria kuiba wakati huna dhamira hiyo?
Kudhamiria ni kosa? Ni kosa pale ambapo dhamira hiyo itakuwa iko kinyume cha sheria. Soma tena post yangu ya kwanza hii hapa chini, taking note of the bolds!


Hivi kwa mfano, ukawa umedhamiria kufanya kitu ambacho wakati mwingine (na si wakati wote), kinachukuliwa kuwa ni kinyume cha sheria, ikitokea ukashindwa kukitekeleza kwa sababu tu ya kuwekewa mazingira pingamizi, kisheria unakuwa huna hatia? Mfano ulidhamiria kwenda kuiba nyumbani kwa A, bahati mbaya ukakuta mazingira hayaruhusu, ukashidwa kuiba, je unakuwa huna hatia katika mazingira hayo, assuming umejulikana?

Kwenye sheria, dhamira ni kitu muhimu sana kuwezesha ruling ya kujua kama kitu ni legal au illgal. Most important , kwenye kujenga mahusiano ya kimkataba wa kisheria, huwa kuna kitu kinaitwa "intention ti create legal relations". Hii ni dhamira ya mkataba.

Tusseme , mkiwa na intention ya kuuziana bangi kwa mfano , mkijulikana mnakuwa na hatia hata kabla hamjaanza mchakato wenu wa kuuziana hiyo bangi.


Kwenye sheria, dhamira ni kitu muhimu sana kuweza kum-judge mtu kama ni mhalifu au siyo mhalifu, hata kabla hajatimiza azma ya kufanya kile alichokuwa amekikusudia.

Haya maswala ya hawa watu yanaangukia kwenye scenerio sawa na hii niliyoieleza hapa

Nyani Ngabu
 
Kudhamiria ni kosa?

Unapimaje kudhamiria?

Je, mtu akidhamiria kuandamana halafu akaahirisha dakika ya mwisho napo amefanya kosa?

Unajuaje huyu kadhamiria na huyu hajadhamiria?

Unahakikishaje wameshikiliwa kwa haki na si kisiasa?

Kesi ya kudhamiria unawezaje kuthibitisha Polisi hawawabambikii watu dhamira za uongo?


Unaweza vipi kumzuia Polisi anayekuchukia kukuzushia kesi ya kudhamiria kuiba wakati huna dhamira hiyo?
Dhamira: walisema wao wenyewe na wakakutwa katika mazingira yanayothibitisha kile waichokuwa wamekisema
Whether ni kisiasa au si kisiasa, kinachoangaliwa hapa kisheria ni dhamira tu basi na si kitu kingine
 
Bora demokrasia mkuu unapambana na watu majukwaani huku unawaona kuliko kuzuia wapinzani wa majukwaani ili uzalishe waasi ambao watapambana nawe kwa kukuvizia na kukimbilia msituni.​
Uko right mkuu nimefuatilia documentary za utawala wa Miamba ya Africa Gaddafi na Mubarak pia Saddam Hussein kilichowaponza ni kujisahau ktk madaraka huwezi amini ilifikia muda Mubarak anaona hakuna anayeweza kutawala zaidi yake hata kumrithisha Mwanae alone sio matokeo yake mapinduzi yaliyofuta mazuri yote waliyofanya (YouTube Uncle Saddam, The family )
 
Kumbe safari bado ni ndefu kwa watanzania, hata wanaojua kusoma na kuandika! Kura ni uamuzi wa wananchi siyo mgombea. Katika hili anayenufaika ni mwananchi siyo aliyepigiwa kura!
Wewe unajuaje kama kura yako iko upande wa ushindi!?

Una uwezo gani kisheria kuhakikisha unajua kura ya mwenzio iko upande gani!?

Nakumbusha, Kura ni siri, Haiandikwi jina..

Kwa upande mwingine Wagombea wamepewa mamlaka kisheria kusimamia zoezi zima na kuhesabu na kulinda kura...

Ikitokea zimeibwa nani aandamane, Mgombea na Wakala!? Au Mwananchi!?

Kwa mgombea na wakala naona wanasababu halali kabisa ila kwa mwananchi sioni... Ukikamatwa ukaambiwa uthibitishe kuwa ulipiga kura ya ushindi unaweza!?

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Wewe unajuaje kama kura yako iko upande wa ushindi!?

Una uwezo gani kisheria kuhakikisha unajua kura ya mwenzio iko upande gani!?

Nakumbusha, Kura ni siri, Haiandikwi jina..

Kwa upande mwingine Wagombea wamepewa mamlaka kisheria kusimamia zoezi zima na kuhesabu na kulinda kura...

Ikitokea zimeibwa nani aandamane, Mgombea na Wakala!? Au Mwananchi!?

Kwa mgombea na wakala naona wanasababu halali kabisa ila kwa mwananchi sioni... Ukikamatwa ukaambiwa uthibitishe kuwa ulipiga kura ya ushindi unaweza!?

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Point sana Mzaz,Shida nyomi na miluzi.
 
Lema atakuwa alikuja dar kwa nia ovu
Police Dar es salaam yaanza kuwakamata waliopanga maandamano.

Walio kamatwa ni pamoja na Aliye kua mbunge wa Arusha Godbless Lema pamoja na Mwwnyekiti wa CHADEMA taifa Mbowe
 
  • Thanks
Reactions: Dua
Wakishinda wao ni huru na haki, wakishindwa ni matusi kashfa kelele kukimbilia kwa mabeberu na nini?! Eti hawa ndio wapenda demokrasia, ila demokrasia yao ni lazima washindi wawe wao tu?!
Ndorobo kabisa...
 
UPDATE

View attachment 1617804

"Mbowe na wenzake watashtakiwa kwa makosa ya ugaidi kwa sababu kuna mtu ametupa ushahidi kuwa walipanga kulipua vituo vya mafuta jijini Dar na kuleta maafa makubwa," Lazaro Mambosasasa, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya DSM.

=====

Kamanda wa Polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam ACP Lazaro Mambosasa amesema wanawashikilia watu kadhaa wakiwemo viongozi watatu wa CHADEMA.

Viongozi wa CHADEMA wanaowashikilia ni pamoja na Freeman Mbowe ambaye ni mwenyekiti wa CHADEMA taifa, Godbless Lema na Boniface Jacob.

Amesema wanawashikilia viongozi hao kwa kuwa wanahatarisha usalama wa Raia na mali zao kwa kuwa Novemba 2 walipanga kuwatumia vijana kuchoma moto miundominu na vituo vya mafuta.

Aidha kwa usiku huu wanaendelea kuwatafuta watu ambao wanawashawishi vijana kushiriki maandamano ambayo Polisi wamesema ni ya Vurugu na si amani kwa kuwa wanaoshawishiwa ni vijana wavuta bangi.

Amesema hayo katika kipindi mubashara kilichorushwa na ITV.

PIA SOMA
= > Uchaguzi 2020 - Dar es Salaam: Watu watatu zaidi wakamatwa kuzuia maandamano
Magaidi wamepewa dhamana!!!! Mambosasa, akili za kuambiwa changanya na za kwako. Umekuwa kituko. Hovyooo.
 
Back
Top Bottom