Kamanda Mambosasa: Mwandishi Erick Kabendera anahojiwa uraia wake

Acha kujitoa akili, leo kwake kesho kwako hata kwa ndugu yako. Tutumie vichwa kufikiria kwa makini.
Kama angekua raia halali angetii wito tu. Ni either raia mkorofi au uraia wake una walakini au sio raia kabisa
 
Kuna wakati Hayati Mwalimu J.K.Nyerere alisema, "ukihoji sana uraia wa mtu katika Inchi ya Tanganyika/Tanzania hakuna atakaye kaa salama. Kila kabila hapa halina asili ya Tanganyika na hata jina Tanganyika halijulikana limetoka wapi."
Kitu cha maana kwa kila Mtanzania ni kuweka kumbu kumbu zake sawa ikiwa ikiwa ni pamoja na Kumbu kumbu muhimu kama vyeti halali vya kuzaliwa, wazazi walikozaliwa, shule ulizosoma n.k.
Hata kama hukuzaliwa Tanzania na kusomea Tanzania, kuna taratibu ya kufuata ili upate urai wa Tanzania.
Ndani ya Inchi yetu kuna Wahindi, Waarabu na hata Wazungu wana uraia wa Tanzania.
Kwa nini mtu anaanza kupelelezwa mambo yake na kukamatwa?
Jibu ni rahisi. Mtu kwa namna Fulani akianza kuchokonoa usalama wa Inchi kwa kufanya propaganda lazima Serikali imfuatilie nyendo zake na kumthibiti ili asije kuleta madhara kwa wengi.
Propaganda ni kumweleza mtu jambo nyeti kwa njia ya uovu au uongo ili kumtia hamasa na kumfanya achukue au atende jambo la uovu au jinai bila kufikiri kwa maslahi ya mfanya propaganda au kwa madhara ya mfanyiwa propaganda.
Kwa kifupi ukitenda kosa moja la jinai linasababisha wapelelezi kuongeza wigo wa kufuatilia nyendo zako zingine ambazo wanawasisi nazo.
Ukipekuliwa nyumbani kwako wakakukuta na bangi hawawezi kuicha tu kwa sababu lengo lao lilikuwa si kutafuta bangi.
Watanzania tunatakiwa kuwa watii na waaminifu kwa Serikali kama Nabii Yesu Kristo alivyokuwa mtii kwa mamlaka ya Ponsio Pilato hadi mauti, mauti ya Msalaba.
 
Walipomfuata Kabendera hawakujitambulisha.
Walimbeba mzobemzobe mbele ya mama yake mzazi ambaye pia ni Mgonjwa kwa mwaka wa tatu mfululizo sasa

Kwahiyo Mama yako akiwa Mgonjwa au Mahututi ndiyo kunazuia Polisi ( Mamlaka husika ) Kutekeleza wajibu wake wa Kisheria?
 
Huyo alikuwa na uhusiano na mtangazaji wa zamani wa Radio Rwanda marehemu Kabendera Shinani?
 
Kuna mmoja alikuwepo mtangazaji wa Rwanda aliitwa Kabendera Shinani. Nadhani hilo jina limemletea kizaazaa!
Hivi akiwepo mtu anaitwa Lazaro Mambosasa au john Magufuli kule Rwanda au Zambia au malawi itamaanisha kuwa hawa wenzetu si raia? au hiyo inaaply kwa sisi tusio na madaraka
 
Ni habari gani ya kiuchunguzi aliyoandika?
 
hii ni ile mutoto ya marehemu kabendela Shinani? aliyejinyongea ziwani au
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…