TANZIA Kamanda wa Polisi ACP Jonathan Shana afariki Dunia

TANZIA Kamanda wa Polisi ACP Jonathan Shana afariki Dunia

sawa, basi usiseme alazwe pema, mwache alazwe anapostahili
Mahindi yanayobanikwa juu ya mkaa ama nyama ndani ya freezer vyote vipo mahali pema kulingana na nature za hivyo vitu....hata peponi roho zote zitakuwa mahali pema kulingana na nature za hizo roho.
 
Ni huzuni & majonzi

Ameumaliza mwendo

Kazi ya Mungu Haina makosa

RIP Kamanda Shana

=====

TANZIA: KAMANDA JONATHAN SHANA AFARIKI DUNIA

Aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoani Arusha, Jonathan Shana amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu

Alifahamika zaidi katika kujihusisha na shughuli za Vyama akiwa na sare za kipolisi. Aidha, aliwahi kufananisha Chama Tawala, Serikali na Dola kwa Kanuni za Kihesabu

Kamanda Shana aliwahi kuwa RCO Mikoa Mbalimbali Nchini ikiwemoRPC-Mikoa ya Pwani, Mwanza na Arusha pia aliwahi kuwa Mkuu wa Upelelezi Simiyu.

ACP Jonathan Shana amefariki akiwa Afisa Mnadhimu katika Chuo cha Polisi (CCP) Moshi



Pia soma >>> RPC Shana anavyotikisha Arusha, awadaka Majangili hatari, AK 45, Meno ya Tembo

Watu 9 waliohusika kutungua chopa na kumuua rubani wakamatwa

Msimpangie Mungu, Mwacheni apange ghalani, matendo ya mtu yamfuate.
Jana Yani Turky analiliwa na kila mtu wa kila chama, tuliobaki tujiulize.
 
Nimepitia comment zote, hitimisho: kumbe kweli wema hauozi, ubaya haulipi. Huyu kiongozi kaondoka lakini yaliyo andikwa humu kumhusu kama ni ya kweli, ndugu na familia kawaachia aibu kubwa.

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app

Wanaomjua wanasema alikua ni mtu poa sana,ila sisi member wa JF tulikua tunamuona tu kwenye media alipokuwa anashabikia ccm basi eti ndio tunamhukumu,tunasahau hilo kosa la u CCM halipo kabisa kwenye mambo ya ki mungu,kuwa CCM hakuwezi kumfanya asiende mbinguni walioishi nae wanasema alikuwa mtu mwema
 
Siku za mwanadamu hapa duniani si nyingi, tuache ujivuni. RIP Kamanda
Maskini! RIP kamanda Shana! hivi huyu ndiye aliyekuwepo kipindi Lema amekwekwa mahabusu miezi sita huko Arusha?🙁
 
Amefanya nini zaidi ya kuwa polisi kada wa chama cha mapinduzi? Na yeye kupitia nafasi yake amekuwa akiunyanyasa upinzani. Ametumika vibaya kisiasa,pia amesababisha niichukie kada yote ya polisi. Naombeni mnisamehe kama nimewakwanza.
R.I.P kamanda kada w CCM
Wewe ni sawa na nyasi moja kudondoka juu ya nyumba huku ukitegeme nyumba ivuje,
 
Back
Top Bottom