Kamati Kuu ya CHADEMA yawavua nyadhifa na uanachama Halima Mdee na wenzake 18 walioapishwa kuwa Wabunge wa Viti Maalum

Pascal Mayalla

Speech ya Mbowe umeisikiliza lakini?
He sounds 100 times more sophisticated and presidential material kuliko poti wako aisee!
 
Sasa na wao viongozi si wawe wanaandamana peke yao kutuwakilisha kama wanavyotuwakilisha bungeni ?

Au kwenye shida tuwe nao ila kwenye raha na kula viyoyozi bungeni wale peke yao.

Aisee maandamano na migomo ni njia za walio kosa mbinu za ukombozi na kukata tamaa.
 
Kwahiyo kamati kuuuu imeungana na sipikaaa? Acheniiii blaablaaa mbele ya maisha ya watuu
 
Laana kubwa kwa covid 19 umetoka kwa wapenzi wanachama wa chadema waliopigwa kujeruhiwa kubambikiwa kesi na Polisiccm na wengine wapo jela mpaka sasa kwa kujitoa mhanga kuwatetea wao, laana za hawa wanachama ndizo zitawatafuna wote mpaka waje kujutia huo ubunge wa mahakamaccm ambao wanaenda kumiliki kuanzia kesho,
 
Mojawapo ya failure kubwa sana ndani ya CHADEMA ni ile ya kutokuwa na conflict resolution strategies nzuri; ndiyo maana imekuwa inamegeka vipande kidogo kidogo. Timu ya Samson Mwigamba, Zitto kabwe na Kitila Mkumbo ilianza kumegeka, halafu ikaja timu ya Slaa, na pigo kubwa likawa ni lile la timu ya Lowassa na Sumaye, na sasa litakuja hili hili la timu ya Bawacha. Ningekuwa nimeazimwa kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA; kwanza ningemzuia Katibu Mkuu asiwashe taa kali kwa chadema kwani Mnyika aliiweka chadema kwenye spotlight kwa kuwatishia akina mama hao kuanza kuigopa chadema. Halafu tungeshughulika ndani ya chama kutafuta jibu lake mwafaka hata kabla ya kuita waandishi wa habari.

Lakini chadema huwa na papala ambazo husababisha imeguke kwa sababu za kujitengezea tu. Sijajua kama yule mama aliyempiga chini mgombea wa CCM naye watamfukuza uanachama ili wabaki kuwa irrelevant kwa kutegemea kuwa wafadhili watainyima serikali misaada. Sikujua kuwa siku hizi CHADEMA kuna watu wana akili ndogo sana ya kupambanua mambo. Kosa kubwa sasa ni kuwa wameshajigawanyika tena.

Niliwahi kusoma hapa JF kuwa Mnyika alisoma UDSM lakini hakumaliza chuo, na halafu Mbowe naye alikwenda kusoma Hull lakini pia hakumaliza!! Sijui kama trend hiyo ya kutokukamilisha mambo ni reflection ya sasa ya mwelekeo wa chama au vipi. "... we will see....." by Trump
 
Laana kabisa. Mfano Matiko kwenye kanda yake anayoongoza tena ndani ya wilaya yake anayotoka kwenye jimbo la Heche kuna watu waliuwawa.
 
Inatakiwa ccm iwatafutie ofisi na vitendea Kazi Kama mihuri ya chama ili wapige kazi. Hawajifunzi kwa kina Kalanga, nassari, lijuakali walovyooachwa solemba hakuna mpinzani aliyewahi kula haramu ya ccm na akabaki salama wote walikufa kisiasa
 
Dharau kubwa aliyoionyesha mdee kwa Uongozi kuwadhihaki mwenyekiti katibu mkuu na makamu mwenyekiti isingeweza kuvumilika kamwe na endapo hao covid 19 wanandungai wangesalia chadema ingefariki ghafra na kuwa kama TLP NCCR na CUF ya Lipumba
 
Inatakiwa ccm iwatafutie ofisi na vitendea Kazi Kama mihuri ya chama ili wapige kazi. Hawajifunzi kwa kina Kalanga, nassari, lijuakali walovyooachwa solemba hakuna mpinzani aliyewahi kula haramu ya ccm na akabaki salama wote walikufa kisiasa
Zito slaa walikwenda sembuse hao vikaragosi mama gubu mdee
 
Leo ilikuwa chadema ifariki ghafra endapo ingewakumbatia wabunge haramu covid 19 lakini baada ya kuwafukuza chadema itaimarika zaidi na kuwa chama bora zaidi
 
Covid 19 wamekutana na remdesivir (Mbowe) chaliiiii
 
Benson Mramba hivi una gundu gani? Mbona CCM hawakupi uteuzi?

Umewatukana sana CHADEMA ila ulaji hupewi. Nenda kwa Mwamposa akakusafishe nyota kwa kukanyaga mafuta.
 
Baada ya kupata taarifa hizo za ki-intelijensia wangetuma Kamanda Mambosasa akatawanye mkutano kwa kuwa unalengo baya la kuwadhulu hao COVIDs
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…