Kamati Kuu ya CHADEMA yawavua nyadhifa na uanachama Halima Mdee na wenzake 18 walioapishwa kuwa Wabunge wa Viti Maalum

Kamati Kuu ya CHADEMA yawavua nyadhifa na uanachama Halima Mdee na wenzake 18 walioapishwa kuwa Wabunge wa Viti Maalum

Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe atazungumza na Umma wa Watanzania kupitia mkutano na waandishi wa habari, leo Novemba 27, 2020, kuanzia saa 3.00 (usiku huu), kuhusu maamuzi ya Kikao cha Kamati Kuu ya Chama

Vyombo vya habari vya Kitaifa na Kimataifa vimealikwa.

Stay Tuned for Updates

======================
Waandishi wanaanza kuwasili ukumbini wanaoingia wanatakiwa kuwa vitambulisho.
Muda wowote kuanzia Viongozi wa Chadema wataingia ukumbini kuongea na waandishi wa habari.
22:08
Bado Viongozi wa Chadema hawajafika ukumbini
Mkutano huo utakuwa live kupitia
Tayari Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe ameshafika ukumbini
Tunawashukuru Watanzania wengi ambao wanafuatilia kikao maalum cha ajenda moja ya kujadili, kushauriana na kutafakari juu ya wanachama wetu 19 waliokwenda kuapa kuwa wabunge wa viti maalum- Freeman Mbowe
"Sisi kama kamati kuu ya chama kikuu cha upinzani, tumeona na kuridhishwa kuna ukiukwaji mkubwa umekiukwa katika mchakato mzima wa uchaguzi na huu wa viti maalum. Tumejiridhisha ndani ya chama kuhusu mapungufu kadhaa yaliyofanyika-; Mbowe
“Chama chetu hakijateuwa Wabunge wa Viti Maalum lakini tunaona wapo Bungeni wanaapishwa”Mbowe
Tangu nchi hii ipate uhuru hatujawai kuona Mbunge/Wabunge wakiapishwa garage, mambo ya kihuni kabisa haya..." Mbowe
“Hiki chama kinaongozwa na principles bila kujali maumivu makubwa tuliyopitia chama chetu kitafuata utaratibu siku zote, kwahiyo kamati kuu imewavua nafasi zao za uongozi viongozi wote waliokua na nafasi katika mabaraza ya chama.”
@freemanmbowetz

“Kamati Kuu imewavua Uongozi wale wote ambao walikuwa Viongozi kwenye Mabaraza kati ya hao Dada zetu 19 sitaki kupoteza muda kuwataja majina, kwahiyo kuanzia sasa hawapaswi kushughulika na lolote kama Viongozi na tumeelekeza nafasi zao zizibwe haraka” -MBOWE

"Ili kanuni ambayo Spika ametumia iweze kufanya kazi kuapisha wabunge wetu. Kwanza wangestahili kubadilisha Katiba iruhusu wabunge kuapishwa nje ya utaratibu ambao ni ndani ya Bunge" -


Nusrate Hanje Katibu wa Bavicha amefungwa jela siku 133 kwa makosa yenye dhamana, hawa Watesi wetu wanakwenda kumtoa saa moja usiku akaape.”


”Chama chetu hakijateua Wabunge wa Viti Maalum tunaona tu Watu wetu wanaapishwa na hatuna taarifa, hatujapeleka majina, fomu za Tume zipo ofisini Mama zetu hawa Dada zetu hawajajaza fomu, ila tunaona tu wanaaapishwa”-

"Sisi kama chama cha siasa, hii 'process' yote hatuijui, tunaona tu wabunge wetu wanaapishwa. Chama chetu hakijateua wabunge wa viti maalum" -

"Wabunge hawa 19, mama zangu na dada zangu wameapishwa kiapo batili kwani Katiba inasema waapishwe mbele ya Bunge. Sasa kanuni zimebadilishwa ili kumruhusu Spika kumwapisha popote hata eneo la gereji-

“Tangu Nchi yetu imeanza hatujawahi kuona Wabunge wanaapishwa Gereji, lakini Dada zetu na Mama zetu hawa wameapishwa nje ya Bunge, wakati Katiba inataka waapishwe ndani ya Bunge, kwahiyo wamekula kiapo batili”
Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe amesema Kamati Kuu ya Chama hicho iliyoketi leo Nov 27,2020 imeazimia kuwavua uanachama Halima Mdee na wenzake 18 waliopishwa juzi kuwa Wabunge Viti Maalum “wamekinajisi Chama na wamekataa kuja kwenye Kamati Kuu”

”Chama chetu hakijateua Wabunge wa Viti Maalum tunaona tu Watu wetu wanaapishwa na hatuna taarifa, hatujapeleka majina, fomu za Tume zipo ofisini Mama zetu hawa Dada zetu hawajajaza fomu, ila tunaona tu wanaapishwa”

“Kamati Kuu imewavua Uongozi wale wote ambao walikuwa Viongozi kwenye Mabaraza kati ya hao Dada zetu 19 sitaki kupoteza muda kuwataja majina, kwahiyo kuanzia sasa hawapaswi kushughulika na lolote kama Viongozi na tumeelekeza nafasi zao zizibwe haraka”
"Kamati Kuu imeazimia kuwavua uanachama wake wote 19 wakiongozwa na Halima Mdee , walioapa kule Dodoma.-Mbowe

Pascal Mayalla

Speech ya Mbowe umeisikiliza lakini?
He sounds 100 times more sophisticated and presidential material kuliko poti wako aisee!
 
Wana-JF,

Kama ilivyo issue ya kuku na yai ni nini kilianza, issue ya akina Mdee nayo yaweza kuangaliwa hivyo hivyo.

Uchafuzi wa uchaguzi wa 27 na 28 Oktoba 2020 ulikuwa wazi kabisa nchi nzima. Wakubwa kwa wadogo waliona kilichotokea. Uchafuzi ule ulipigwa picha na video sehemu mbalimbali za Tanzania. Unyang'anyi na udhalimu ule haukufichwa hata kidogo.

Baada ya hilo, viongozi waliitisha maandamano ya amani. Wananchi hawakujitokeza. Hawa hawa walioshuhudia wizi wa kura mpaka wakapiga video na kuweka kwenye social media, walikataa kuandamana walipotakiwa kufanya hivyo. Kule Zanzibar niliona Maalim akindamana na kundi la watu kama 20 hivi. Mita kama 50, wakapigwa mabomu na kukamatwa. Na ndio uliokuwa mwisho huo.

Hivi Watanzania tunategemea viongozi watuletee mabadiliko bila sisi kushiriki? Je, attitude hii ya Watanzania, haihusiki katika kukatisha tamaa viongozi? Viongozi nao wakiamua kutafuta riziki zao na familia na kuweka masilahi ya Watanzania nyuma, wanastahili lawama?

Naamini 100% kuwa saliti ni kitu kibaya. Lakini sisi Watanzania kwa tabia zetu, hatuchangii katika hali hii?

Fikiria na chukuwa hatua.
Sasa na wao viongozi si wawe wanaandamana peke yao kutuwakilisha kama wanavyotuwakilisha bungeni ?

Au kwenye shida tuwe nao ila kwenye raha na kula viyoyozi bungeni wale peke yao.

Aisee maandamano na migomo ni njia za walio kosa mbinu za ukombozi na kukata tamaa.
 
Wana siku thelathini za kuomba msamaha. Ila kama wanaona wameonewa, wana siku hizo hizo thelathinu za kukata rufaa na kupeleka suala lao kwenye Baraza Kuu la chama kilichokuwa chao. Aidha, wanaweza kwenda Mahakamani kukishitaki chama kilichokuwa chao kwa kutowatendea haki. Mahakama inaweza kutoa zuio ambalo litadumu kwa miaka mitano. Njia rahisi katika zote ni kumsikiliza Spika atakachosema na kujiunga na wakina Silinde na Mollel bungeni kutetea wananchi wa taifa letu la Tanzania. Baada ya miaka mitano wataweza kuwafuata wenzao rasmi kwenye chama cha Spika.

Amandla...
Kwahiyo kamati kuuuu imeungana na sipikaaa? Acheniiii blaablaaa mbele ya maisha ya watuu
 
Laana kubwa kwa covid 19 umetoka kwa wapenzi wanachama wa chadema waliopigwa kujeruhiwa kubambikiwa kesi na Polisiccm na wengine wapo jela mpaka sasa kwa kujitoa mhanga kuwatetea wao, laana za hawa wanachama ndizo zitawatafuna wote mpaka waje kujutia huo ubunge wa mahakamaccm ambao wanaenda kumiliki kuanzia kesho,
 
Mojawapo ya failure kubwa sana ndani ya CHADEMA ni ile ya kutokuwa na conflict resolution strategies nzuri; ndiyo maana imekuwa inamegeka vipande kidogo kidogo. Timu ya Samson Mwigamba, Zitto kabwe na Kitila Mkumbo ilianza kumegeka, halafu ikaja timu ya Slaa, na pigo kubwa likawa ni lile la timu ya Lowassa na Sumaye, na sasa litakuja hili hili la timu ya Bawacha. Ningekuwa nimeazimwa kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA; kwanza ningemzuia Katibu Mkuu asiwashe taa kali kwa chadema kwani Mnyika aliiweka chadema kwenye spotlight kwa kuwatishia akina mama hao kuanza kuigopa chadema. Halafu tungeshughulika ndani ya chama kutafuta jibu lake mwafaka hata kabla ya kuita waandishi wa habari.

Lakini chadema huwa na papala ambazo husababisha imeguke kwa sababu za kujitengezea tu. Sijajua kama yule mama aliyempiga chini mgombea wa CCM naye watamfukuza uanachama ili wabaki kuwa irrelevant kwa kutegemea kuwa wafadhili watainyima serikali misaada. Sikujua kuwa siku hizi CHADEMA kuna watu wana akili ndogo sana ya kupambanua mambo. Kosa kubwa sasa ni kuwa wameshajigawanyika tena.

Niliwahi kusoma hapa JF kuwa Mnyika alisoma UDSM lakini hakumaliza chuo, na halafu Mbowe naye alikwenda kusoma Hull lakini pia hakumaliza!! Sijui kama trend hiyo ya kutokukamilisha mambo ni reflection ya sasa ya mwelekeo wa chama au vipi. "... we will see....." by Trump
 
Laana kubwa kwa covid 19 umetoka kwa wapenzi wanachama wa chadema waliopigwa kujeruhiwa kubambikiwa kesi na Polisiccm na wengine wapo jela mpaka sasa kwa kujitoa mhanga kuwatetea wao, laana za hawa wanachama ndizo zitawatafuna wote mpaka waje kujutia huo ubunge wa mahakamaccm ambao wanaenda kumiliki kuanzia kesho,
Laana kabisa. Mfano Matiko kwenye kanda yake anayoongoza tena ndani ya wilaya yake anayotoka kwenye jimbo la Heche kuna watu waliuwawa.
 
Inatakiwa ccm iwatafutie ofisi na vitendea Kazi Kama mihuri ya chama ili wapige kazi. Hawajifunzi kwa kina Kalanga, nassari, lijuakali walovyooachwa solemba hakuna mpinzani aliyewahi kula haramu ya ccm na akabaki salama wote walikufa kisiasa
 
Anafukuza watu halafu anawapa nafasi ya kukata rufaa? Ina maana bado wanahitajika.

Inanikumbusha JK alivyomfukuza kazi Tibaijuka mbele ya wazee wa Dar baada ya kushinikizwa na umati, baada ya kustukia makosa yake kabla ajaongeza mengine ilibidi amalize mkutano haraka.

Pamoja na makelele yetu yote uhalisia ni kwamba Mbowe anajua kachukua maamuzi magumu mno kupoteza askari wake muhimu vitani kama Mdee, Matiko na Bulaya sio pengo dogo.

Asilimia kubwa ya makamanda wenye elimu zenu na mafanikio ya kibiashara amko tayari kuacha proffesional jobs au mafanikio kuunga mkono juhudi za upinzani mnachojuwa ni makelele ya mitandaoni.

It was a trap kuwaacha ingeweza leta sura mbaya lakini bado una askari wako muhimu, kuwafukuza askari muhimu kunapunguza nguvu ya kupambana.

Catch 22 chaguo alilochukua mwenyekiti kwa upande wangu sio sahihi; it must be said kutotokea kwao nako kumechangia kufukuzwa.
Dharau kubwa aliyoionyesha mdee kwa Uongozi kuwadhihaki mwenyekiti katibu mkuu na makamu mwenyekiti isingeweza kuvumilika kamwe na endapo hao covid 19 wanandungai wangesalia chadema ingefariki ghafra na kuwa kama TLP NCCR na CUF ya Lipumba
 
Inatakiwa ccm iwatafutie ofisi na vitendea Kazi Kama mihuri ya chama ili wapige kazi. Hawajifunzi kwa kina Kalanga, nassari, lijuakali walovyooachwa solemba hakuna mpinzani aliyewahi kula haramu ya ccm na akabaki salama wote walikufa kisiasa
Zito slaa walikwenda sembuse hao vikaragosi mama gubu mdee
 
Leo ilikuwa chadema ifariki ghafra endapo ingewakumbatia wabunge haramu covid 19 lakini baada ya kuwafukuza chadema itaimarika zaidi na kuwa chama bora zaidi
 
Covid 19 wamekutana na remdesivir (Mbowe) chaliiiii
 
Benson Mramba hivi una gundu gani? Mbona CCM hawakupi uteuzi?

Umewatukana sana CHADEMA ila ulaji hupewi. Nenda kwa Mwamposa akakusafishe nyota kwa kukanyaga mafuta.
 
Kwani CCM ni chademaa?? Mmewaonea kwa kuwa ni wanawakeee. Maaana sababu wamezitoa na wameomba ifanyike siku nyingine maaana kiukweli mazingira hayakua salama kwao, watu walikua na hasira na Mbowe akasema mazingira yalikua salama na huku wafuasi wengi wachadema waliandamana huku wakiwashikia mabango yaliyokuwa na matusi ya kuwalinganisha na gonjwa baya la korona covid 19. Hivyo mazingira hayakua salama kwao. Kamatii kuuu ilipaswa iahishishe mpaka hapo wao walipo omba wafike mkutanoni.
Baada ya kupata taarifa hizo za ki-intelijensia wangetuma Kamanda Mambosasa akatawanye mkutano kwa kuwa unalengo baya la kuwadhulu hao COVIDs
 
Back
Top Bottom