waco1920
Member
- Oct 20, 2020
- 14
- 33
Ukiangalia sintofahamu na matukio ya kihuni yanayoendelea ndani ya CHADEMA na katika Taifa hili, kwa ujumla wake ukiangalia katika macho ya kiroho, utagundua kuwa uwepo wa changamoto hizi zinazopitiwa na Chadema, hauna tofauti na zile ambazo wana wa Israeli walizipitia wakati wakitoka katika Nchi ya utumwa ya MISRI kuelekea katika nchi ya ahadi ya KANANI.
Maana katika kundi lile wapo waliopewa nguvu kubwa sana ya kuongoza na kuwaaminisha wenzao kuwa ndiyo watakaowafikisha katika nchi ya AHADI. Lakini haikuwa hivo! Kwani wengi wao waliishia njiani na wakafa bila kuiona nchi hiyo. Katika vizazi vilivyobaki wapo waliokata tamaa, lakini wengine waliwatia moyo na kusema, tunaishi kwa AHADI ya MUNGU! Lazima tufike katika nchi ya AHADI.
Hivi ndivyo ilivyo leo kwa haya yanayowatokea akina HALIMA MDEE na wenzake! Yawezekana wakati wanafanya hayo walifikiri kuwa wao ndiyo CHADEMA! Lakini CHADEMA ni Taasisi kubwa ambayo mtu yeyote anaweza kuiongoza kwa misingi ya kufuata Kanuni na Sheria zake. Na wapo tena wazuri Zaidi ya hao!
Kwa tafsiri nyingine inafaa tuiangalie CHADEMA kama ni mpango wa MUNGU! Kwamba huu ndiyo wakati sahihi wa MUNGU sasa kuandaa watakatifu ambao wanastahili kukabidhiwa DOLA! Akina MDEE watabaki kwenye historia kuwa walianzisha safari lakini walifia njiani kama ilivyokuwa kwa akina MUSA na wenzake.
ITOSHE TU KUSEMA, KUWA UKIONA HAYA YANATOKEA, UJUE KUWA MPANGO WA MUNGU UNAKARIBIA.
UAMZI WA KAMATI KUU NI 100%