Influenza
JF-Expert Member
- Jul 1, 2018
- 1,509
- 3,756
Kamati ya Maadili imemkuta Mgombea wa Jimbo la Vunjo kupitia NCCR Mageuzi, James Mbatia na hatia katika tuhuma ya uvunjivu wa Maadili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya Mwaka 2020.
Hivyo Kamati hiyo imemsimamisha James Mbatia kufanya kampeni kwa muda wa siku 7 kuanzia tarehe 17 Oktoba 2020 hadi tarehe 23 Oktoba 2020 kwa mujibu wa Kanuni ya 5.11 (d) ya Maadili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya Mwaka 2020.
Hiyo ni baada ya Kamati ya Maadili Jimbo la Vunjo iliyokaa Oktoba 16, 2020 kupitia tuhuma ya uvunjivu wa Maadili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya Mwaka 2020 dhidi Mbatia ya kujihusisha na kutumia kipeperushi cha kampeni ambacho hakijaidhinishwa na Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Vunjo.