Uchaguzi 2020 Kampeni za Uchaguzi mkuu - 2020 mitandaoni ni mtifuano wa kufa mtu kati ya TEAM Tundu Lissu (CHADEMA) vs TEAM John Magufuli (CCM)

Unadhani way hujapata like .

Sent from my SM-A605FN using JamiiForums mobile app
 

Nina mambo mawili kushea nawe;

1. Uchaguzi wowote ni siasa halisi. Uchaguzi unahusu kumpamba kwa uzuri mgombea wako huku upande wa pili wa wapinzani wako wakitafuta udhaifu wako personally na wakati mwingine SERA na MIPANGO yako na kukubomoa....

Kwa hiyo hili la Tundu Lissu kupambwa lisikukere bali fahamu kuwa, mambo ndivyo yalivyo. Na hata wewe unayo nafasi wa kumpamba utakavyo mgombea unayedhani anakufaa hata kama ni Prof. Ibrahimu Lipumba....

2. Kuhusu baadae kushangaa Tundu Lissu kupata kura kidogo pengine hata kuzidiwa na mgombea wa SAU aliyeingia ofisi za NEC akiwa pekupeku....

Sijui umetumia vigezo vipi kuja na wazo hili. Hii inaonesha kuwa, wewe hata kusikia tu huwezi kusikia; ama hata kuona huoni na wala hujisumbui kujifunza historia...

Naomba nikurejeshe kwenye historia ya CHADEMA kwa kigezo cha ushiriki wa chaguzi za huko nyuma....

Tuanze na uchaguzi mkuu wa 2005 ambapo CHADEMA kikiwa chama kichanga sana (siyo kiumri bali kimtandao) kilimsimamisha Ndg Freeman Mbowe kugombea Urais dhidi ya Jakaya Kikwete (CCM) na Prof. Ibrahimu Lipumba (CUF)...

Matokeo yalikuwa mazuri sana. Freeman Mbowe alipata kura karibu 800,000 na wabunge zaidi ya 10 na kuongoza halmshauri kadhaa akifuatiwa na Lipumba aliyekuwa na kura 1,000,000+ na mshindi akawa JK

Mwaka 2010, CHADEMA wakamsimamisha Dr Willbroad Slaa. Graph ikapaa sana kwa kupata kura 2,600,000+ na viti vya ubunge wa majimbo vya kutosha zaidi ya 30 + halmshauri kadhaa....

Mwaka 2015, CHADEMA wakamsimamisha Ndg Edward Lowassa. Pamoja na kuibiwa kura nyingi na kupewa huyu Rais magumashi wa sasa, CHADEMA alipata kura zaidi 6,000,000+ na wabunge wa majimbo zaidi ya 60 + halmashauri zaidi ya 6....

Katika chaguzi za mwaka 1995 na 2000, CHADEMA hawakusimamisha mgombea URAIS...

Kwa takwimu hizi, unaweza kuona kuwa, graph ya CHADEMA iko very stable, haijawahi kushuka wala kutetereka...

Na kwa taarifa yako, hakuna uchaguzi rahisi kati ya chaguzi zote zilizopita kama huu wa mwaka huu 2020. Ni kwa sababu, katika marais wote wa CCM waliotawala nchi, hakuna Rais mbovu na wa hovyo kama ndugu John Pombe Magufuli....!!

And on the other hand, hakuna ktk chaguzi zote zilizopita za 2005, 2010, na 2015 ambapo CHADEMA wameweka mgombea bora wa Urais na mwenye nguvu ya ushawishi kama Tundu A.M Lissu huku chama kikiwa kimeimarika kimtandao na kirasrimali watu na fedha kama ktk uchaguzi mkuu wa mwaka huu 2020....!!

Nakuambia jambo moja muhimu kuwa, nyie watu msioamini juu ya nguvu ya MAJIRA na NYAKATI kuwa, CCM, Magufuli na ninyi wafuasi wake ndiyo ambao mtashangazwa na matokeo ya uchaguzi wa mwaka huu....!

Nikukumbushe hili pia kuwa, JOHN MAGUFULI mwaka 2015 alipata ushindi hafifu wa 56% ya kura zote...

Na historia inaonesha kuwa, hakuna mgombea Urais wa CCM anayerudia muhula wake wa pili aliyewahi kuongeza % ya kura anapogombea ktk muhula wa pili bali wote hushuka....!!!

Sasa huyu Magufuli ambaye ktk miaka yake mitano kaharibu nchi hii kwa viwango vya kutisha na 2015 akishinda ushindi dhaifu wa 56%, unadhani mwaka huu ata drop kwa % ngapi?....

Jibu ni hili: 56% - 20 = 36%....!!
 
Ndio maana ni ikakwambia ccm lazima ishinde sababu hao vijana hawana uwezo wa kuwazidi nguvu wazee na kina mama wanaoifagilia ccm,
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] Vituko hivi
 
Ni bao la mkono tu ndilo linaweza kuiokoa ccm mwaka huu.
Kwa mitandaoni Magufuli aka Yesu kapigwa vibaya mno na mbeba maono mwana wa Africa Tundu Lissu!
Hakika lina heri tumbo lililomzaa
Hapo kwenye Chadema ongezea ACT wazalendo nao wametangaza leo kumuunga mkono TL
Hahahha.. Subiri oktoba ndio utajua kama mnaishi kwenye computer au laa
Sasa sijui ni kwa vigezo gani Chadema wanadai wameshinda Mitandaoni labda kwa kutukana Sana , hapo nakubali.

Jamaa wanajua kutukana bwana asikwambie mtu.
 
Mkuu,! Ushindi haujawahi kupatikana kupitia coment za jf, fecebook, twitter na Instagram,

Kura zipo huku kitaa huku ndio unaweza kuchukua sample ya ushindi,

Hivi unadhani tulioko huku kwenye mitandao tuko nje ya nchi, na wala hatuko huku mitaani? Ccm walikuwa wanasema wapinzani wana ushawishi mitandaoni tu uchaguzi wa 2015. Matokeo yenye mashaka ya tume isiyo huru yalikuwa mgombea wa ccm kura 8m+, huku wa upinzani akipata 6m+, tena toka kwa mgombea aliyekuwa hawezi kuongea hata dakika 3. Wagombea wa ubunge wa ccm karibia asilimia 20 walishinda ubunge kwa figisu, na wengine kwa tofauti ndogo sana ya kura baina yao na washindani wao.

Baada ya Magufuli kujua hatari wanayoenda kukutana nayo uchaguzi huu, akaanza kutumia madaraka yake vibaya kuzuia wapinzani kufanya siasa kwa mujibu wa sheria, hapa ndio mbinu za kufunga wapinzani zilipoanza, kuteka, kuuwawa kwa wapinzani na ushenzi wote unaojua wewe,ikiwemo kunajisi chaguzi zote ili kuicha ccm ikitamba. Hata kilichowapa ccm nguvu ya kutamka kuwa watashinda uchaguzi huu kabla ya Lisu kurudi, ni mazingira hayo ya hofu waliyopandikiza kwa wapiga kura, na mapenzi bandia waliyoweka.

Na hata uchaguzi huu tayari mazingira ya hatari yanaandaliwa, ili kufanya umafia kwa backup ya vyombo vya dola ili kuibeba ccm. Subiri kampeni zianze na ccm waone mwitikio wa umma kwa vyama vya upinzani. Utaniambia matokeo ya kishenzi yatakavyoshamiri.
 
Tusubiri oktoba mkuu
 

Very sad indeed...

Wafuasi wa Magufuli watakuja na kusema kuwa, huyo ni mzembe. Alitakiwa afanye kazi kwa sababu eti Magufuli baba yao anasema "HAPA KAZI TU"...
 
Ndio maana ni ikakwambia ccm lazima ishinde sababu hao vijana hawana uwezo wa kuwazidi nguvu wazee na kina mama wanaoifagilia ccm,

Vijana ndio wengi nchi hii. Zamani ccm ilikuwa inasema vijana hawapigi kura, bali akina mama, sasa hivi vijana ndio wapiga kura wengi. Hii ndio maana ccm haitaki tume huru ya uchaguzi, na inategemea zaidi vyombo vya dola. Na sababu hasa ya ccm kupata mbeleko ya vyombo vya dola ni kofia ya mwenyekiti wao ambaye ana kofia ya urais. Ni vigumu sana kujua saa ngapi mwenyekiti wa ccm ni mwenyekiti au rais, na hata taasisi zote zinatii maagizo ya ccm, kwakuwa mwenyekiti wake anaitumia kofia ya urais kuzitisha taasisi za kimamlaka kutokana na katiba mbovu.

Madaraka ya urais ya mwenyekiti wa ccm,
ndio nguvu pekee ya ccm na wala sio ushawishi wa kisiasa,. Hata hii nguvu ambayo ccm wanajisifia wanayo hivi sasa, ni kwakuwa mwenyekiti wake anatumia madaraka yake ya urais vibaya kunyanyasa vyama vya upinzani, huku akikipendelea chama chake waziwazi kinyume kabisa na katiba.
 
Unataka kusema technology haina faida? Safi sana, endelea hivyo hivyo na akili zako, dalili ya serikali kuangukia pua ipo karibu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chadema mnashinda mitandaoni si kwasababu hamna kazi,mlitimuliwa vyeti feki na kwenye upigaji.

Wooh...!!

Nawe umewaza na kisha kuandika kwa kutumia kichwa na mikono yako kweli...!!???

Usitake niamini kuwa umetumia kiungo kingine kuwaza kisha ukaandika...
 
Anapanga kujiondoa na kumuunga mkono lissu bado kutangaza tuu
Membe yuko katika ballot process just in case watamfanyia Lissu figisu. Na kutangaza kumuunga mkono ni kimkakati pia ili kama (iff) Lissu atatenguliwa basi CDM waweze kurejesha favour.

Kwa kifupi tu, joto au baridi, NDULI atoke tu!
 

Hakika, hili ndilo linalopaswa kufanyika....

Kuna tetesi kuwa JWTZ wamekataa ujinga wa kuhusishwa na siasa....

CDF - Mabeyo ambaye ni "homeboy" wa Jiwe ameshindwa kuwashawishi mabrigedia wakuu wa vikosi kumuunga mkono homeboy wake kufanya kazi ya polisi ya "kuchakaza" raia ktk uchaguzi huu ili mradi ashinde....

Kwa NEC hii, KANUNI hizihizi, Polisi hawahawa, TISS hawahawa, wasimamizi hawahawa, CCM na Magufuli ni mwisho wao...lazima waondoke...

Kama ulivyosema, kampeni zianze sasa kuhamasisha watu kwenda kupiga kura kwa wingi against CCM na tuhakikishe mshindi halali anatangazwa bara na visiwani....

Watu wanahitaji UHURU kamili wa pili toka kwa MKOLONI MWEUSI mwenzetu baada ya ule wa 1961....!!
 

Kwa nyongeza, unaweza kunisoma 👇
 
Mkuu nenda kwenye page ya Mnyika kule facebook uone maoni ya watu kwenye kile kipande cha hotuba ya Lisu kule dodoma,
 
Asante sana mzee
 
Kwa nyongeza, unaweza kunisoma 👇

Mkuu hizo habari kwamba JWTZ wamegoma kuwa makuwadi wa ccm ni za kweli? Kama ni kweli nianze kushawishi kwa nguvu tena jamaa zangu waliogoma kushiriki huo uhuni uitwao uchaguzi.
 
Fact
 
Ni mtifuano kati ya watu wanaojielewa versus mazwazwa ya lumumba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…