Isitoshe Uchaguzi Mkuu ujao si kati ya Lissu na Magufuli bali Lissu dhidi ya wagombea wengine wa Urais.
Nguvu na muda mwingi unatumika kumpamba Lissu kupitia mgongoni mwa Magufuli na Lissu naye kakamatwa na ugonjwa huo. Mwisho wa siku Lissu na wapambe wake watashangazwa na matokeo. Kwa utabiri wangu Lissu atapitwa kura na wagombea wengine
Nina mambo mawili kushea nawe;
1. Uchaguzi wowote ni siasa halisi. Uchaguzi unahusu kumpamba kwa uzuri mgombea wako huku upande wa pili wa wapinzani wako wakitafuta udhaifu wako personally na wakati mwingine SERA na MIPANGO yako na kukubomoa....
Kwa hiyo hili la Tundu Lissu kupambwa lisikukere bali fahamu kuwa, mambo ndivyo yalivyo. Na hata wewe unayo nafasi wa kumpamba utakavyo mgombea unayedhani anakufaa hata kama ni Prof. Ibrahimu Lipumba....
2. Kuhusu baadae kushangaa Tundu Lissu kupata kura kidogo pengine hata kuzidiwa na mgombea wa SAU aliyeingia ofisi za NEC akiwa pekupeku....
Sijui umetumia vigezo vipi kuja na wazo hili. Hii inaonesha kuwa, wewe hata kusikia tu huwezi kusikia; ama hata kuona huoni na wala hujisumbui kujifunza historia...
Naomba nikurejeshe kwenye historia ya CHADEMA kwa kigezo cha ushiriki wa chaguzi za huko nyuma....
Tuanze na uchaguzi mkuu wa 2005 ambapo CHADEMA kikiwa chama kichanga sana (siyo kiumri bali kimtandao) kilimsimamisha Ndg Freeman Mbowe kugombea Urais dhidi ya Jakaya Kikwete (CCM) na Prof. Ibrahimu Lipumba (CUF)...
Matokeo yalikuwa mazuri sana. Freeman Mbowe alipata kura karibu 800,000 na wabunge zaidi ya 10 na kuongoza halmshauri kadhaa akifuatiwa na Lipumba aliyekuwa na kura 1,000,000+ na mshindi akawa JK
Mwaka 2010, CHADEMA wakamsimamisha Dr Willbroad Slaa. Graph ikapaa sana kwa kupata kura 2,600,000+ na viti vya ubunge wa majimbo vya kutosha zaidi ya 30 + halmshauri kadhaa....
Mwaka 2015, CHADEMA wakamsimamisha Ndg Edward Lowassa. Pamoja na kuibiwa kura nyingi na kupewa huyu Rais magumashi wa sasa, CHADEMA alipata kura zaidi 6,000,000+ na wabunge wa majimbo zaidi ya 60 + halmashauri zaidi ya 6....
Katika chaguzi za mwaka 1995 na 2000, CHADEMA hawakusimamisha mgombea URAIS...
Kwa takwimu hizi, unaweza kuona kuwa, graph ya CHADEMA iko very stable, haijawahi kushuka wala kutetereka...
Na kwa taarifa yako, hakuna uchaguzi rahisi kati ya chaguzi zote zilizopita kama huu wa mwaka huu 2020. Ni kwa sababu, katika marais wote wa CCM waliotawala nchi, hakuna Rais mbovu na wa hovyo kama ndugu John Pombe Magufuli....!!
And on the other hand, hakuna ktk chaguzi zote zilizopita za 2005, 2010, na 2015 ambapo CHADEMA wameweka mgombea bora wa Urais na mwenye nguvu ya ushawishi kama Tundu A.M Lissu huku chama kikiwa kimeimarika kimtandao na kirasrimali watu na fedha kama ktk uchaguzi mkuu wa mwaka huu 2020....!!
Nakuambia jambo moja muhimu kuwa, nyie watu msioamini juu ya nguvu ya MAJIRA na NYAKATI kuwa, CCM, Magufuli na ninyi wafuasi wake ndiyo ambao mtashangazwa na matokeo ya uchaguzi wa mwaka huu....!
Nikukumbushe hili pia kuwa, JOHN MAGUFULI mwaka 2015 alipata ushindi hafifu wa 56% ya kura zote...
Na historia inaonesha kuwa, hakuna mgombea Urais wa CCM anayerudia muhula wake wa pili aliyewahi kuongeza % ya kura anapogombea ktk muhula wa pili bali wote hushuka....!!!
Sasa huyu Magufuli ambaye ktk miaka yake mitano kaharibu nchi hii kwa viwango vya kutisha na 2015 akishinda ushindi dhaifu wa 56%, unadhani mwaka huu ata drop kwa % ngapi?....
Jibu ni hili: 56% - 20 = 36%....!!