Uchaguzi 2020 Kampeni za Uchaguzi mkuu - 2020 mitandaoni ni mtifuano wa kufa mtu kati ya TEAM Tundu Lissu (CHADEMA) vs TEAM John Magufuli (CCM)

Kwa mitandaoni Magufuli aka Yesu kapigwa vibaya mno na mbeba maono mwana wa Africa Tundu Lissu!
Hakika lina heri tumbo lililomzaa
Teh teh 🎢 teh 🎢🎡 mna maneno sana nyie raia ila huu uchaguzi huenda ukaja na mengi.
 

Mimi nimekuwa around kwa miaka zaidi ya 70. Ugumu wa maisha umekuwepo tangu nizaliwe, na jinsi siku zinavyopita kunakuwa na nafuu sehemu fulani na kluongezeka sehemu nyingine. Ugumu wa maisha unachangiwa na sababu nyingi. Pia tukumbuke huo ugumu wa maisha unaongelewa mara nyingi ni wa wapiga "deal" ambao hutegemea ufisadi kupata pesa. Mara nyingi ukisikia hao wanalia ugumu wa maisha, maana yake ni kuwa njia za ufisadi zimefungwa na pesa inapatikana tu kwa kufanya kazi.
 
Lissu atashangazwa kivipi wakati kwa opinion poll anaongoza kwa asilimia 70+. Hakuna namna magufuli anaweza mshinda Tundu Lissu ndugu yangu nakwambia. There is no way. Never

This is day dreaming.
 
Wewe unafikiri kitoto sana, eti wa mitandaoni. Wanalala wapi humo mitandaoni? Si ni watu kama wewe, ni wapiga kura kama wewe. Tukusaidie cha kusema ili ueleweke, labda hoja yako ungeiweka hivi'' ccm wanatumia ujinga wa baadhi wa baadhi ya watu, tume ya uchaguzi na matumizi mabaya ya vyombo vyetu vya usalama kupata ushindi wa kulazimisha (rejea mambo ya kuudhi ya Jecha 2015, nk)
 
Ninyi ndio mnampoteza Magu wallah...kwa unafiki wenu huo.
 
Watu na kazi zao banaa. Embu tuache sisi ambao tupo mtaani tangu 2015 tukisugua bench.
 
SGR stand za bus sijui masoko yote haya yatamsaidia mtu aishiye kijijini Aliyelima kufa na kupona auze mazao ampelekee mtoto shule lakini aliambulia kudhulumiwa hakuna masoko ya kuuza mazao kodi zimezidi mtoto hajaweza kwenda shule wote wapo shambani kujilimia wapate chakula wasife njaa.
Tatizo lenu mnaona WaTz wajiiinga
Eti reli barabara madaraja ndege hivi vyote havina faida kwa mkulima na mfugaji hata mfanyabiashara mmetuchosha na hadithi zenu za alfu ulelaulela......
 
Hoja zako ni za kijiweni. Hicho chakula unachokula hapa mjini kinatoka wapi kama hakuna masoko? Umecheki data za export za mazao mbalimbali against priduction? Fungua website za World bank, UNCTAD utazame data japo nina shaka kama unaweza hata kufanya analysis maana nikikuambia tazama data za TRA, NBS na BOT utasema zimepikwa. Hali nzuri sio watu kufaidika na wizi au mnyororo wa wizi na ufisadi.
Unaposema hali mbaya unatakiwa ulinganishe na kwa kutumia data.
Unashindwa kuona bavkward and forward linkage ya ujenzi wa miundombinu ya reli, barabara, viwanja vya ndege, masoko nk katika kumnufaisha mkulima au mtu wa kijijin au wa mjini? Sio kila mtu ni mchumi au anaujua uchumi.
Kama unafikiri maisha mazuri yatashuka kama mvua nakuhakikishia mpaka unakufa hutayapata hata atawale nani.
Kwa level yako nenda katika soko lolote asubuhi uone malori yanavyoshusha mazao toka vijijini.
 
Inamaanisha kuwa nchi hii ya Tanzania ilijipatia Uhuru wake 2015?Ilikuwa koloni LA Old CCM na sasa imepata mkombozi CCM Mpya?
Tulikuwa na reli ya Dar-Kigoma and Mwanza via Tabora.Nyingine Tabora-Mpanda.Dar-Moshi and Tanga,SGR ya TAZARA toka Dar-Kapiri mposhi Zambia na pia kuna ile ya kusini Lindi-Mtwara.Acha usafiri wa Barabara za kuunganisha mikoa yote kabla huyu MTU wenu hajaingia 2015,kufanya nini zaidi kuwazidi waliomtangulia?CCM ndiyo iliyokuwa madarakani miaka yote baada ya TANU&ASP,mnataka kutuaminisha kuwa Mwl.Nyerere,Mzee Mwinyi,Mzee Mkapa(RIP) na Mzee J.M Kikwete walikuwa wazembe?Acheni kuwatukana Wazee hawa kwa manufaa ya Mtu wenu.
Watanzania tuamke,ulaghai hauwezi kutusaidia.Chagua Viongozi wenye Utu,wanaozingatia Usawa na watenda Haki na siyo Watawala.
 

Hii kauli ya "ugumu wa maisha" inayosemwa semwa sana huko CCM kuwa ni ya "wapiga deal, waliozoea kula rushwa", it sounds awkward always....!!

Hivi mkulima huyu wa korosho na mbaazi wa Tandahimba, Mtwara, na Lindi...

Wakulima wa zao la mkonge wa Tanga na Morogoro....

Wakulima wa zao la pamba wa mikoa ya Tabora, Simiyu, Mwanza, Geita, Shinyanga, Mara na Singida....

Utaiwaitaje ni wala rushwa na wapiga deal na hawafanyi kazi wakati hali zao ngumu za kimaisha zimesababishwa na SERA na MAAMUZI ya hovyo ya Rais Magufuli na CCM yake??

Kama ndivyo unavyofikiri ndugu yangu, basi wewe una shida ktk ubongo wako haijalishi una umri gani Mzee au kijana....!!
 
Usimjaribu yesu wa chattle 🀣 🀣
Mmekosa majina mengine hadi mtumie YESU? Kuweni na adabu unapotaja Hilo jina uwe unafikiri kabla,Kuna wakati mnawakosesha sapoti wagombea wenu sababu ya upuuzi wa wapambe wasio na hekima Kama wewe
 
mwaka 2015 JPM alipata kura 54000 tu Dsm nzima .hili halijatangazwa popote. wewe kwa ujinga wako unadhani mitandao haina nguvu bado. kalagabaho
 
Kipi atakachokifanya Tundu Antipasi Lissu akishapewa dhamana ya kuongoza nchi??
 
Mmekosa majina mengine hadi mtumie YESU? Kuweni na adabu unapotaja Hilo jina uwe unafikiri kabla,Kuna wakati mnawakosesha sapoti wagombea wenu sababu ya upuuzi wa wapambe wasio na hekima Kama wewe
gufuli ni yesu wa chattle au vipi 😁 😁
 
JPM katili sana, ndiye aliyebariki shambulio la Lissu kuchapwa zile mvua za risasi. Muda ukifika tutaweka wazi kila kitu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…