Uchaguzi 2020 Kampeni za Uchaguzi mkuu - 2020 mitandaoni ni mtifuano wa kufa mtu kati ya TEAM Tundu Lissu (CHADEMA) vs TEAM John Magufuli (CCM)

Uchaguzi 2020 Kampeni za Uchaguzi mkuu - 2020 mitandaoni ni mtifuano wa kufa mtu kati ya TEAM Tundu Lissu (CHADEMA) vs TEAM John Magufuli (CCM)

Kwa mitandaoni Magufuli aka Yesu kapigwa vibaya mno na mbeba maono mwana wa Africa Tundu Lissu!
Hakika lina heri tumbo lililomzaa
Teh teh 🎶 teh 🎶🎵 mna maneno sana nyie raia ila huu uchaguzi huenda ukaja na mengi.
 
Katika hali ya kawaida CCM itakuwa inajidanganya sana kudhania watanzania na ugumu wa maisha ya watu ulivyo hii awamu wanayo hamu hata kusikia hicho chama. Kila mtu amechoka mno tuvumiliane ifike tu October siyo mbali. Kwa ugumu wa maisha sasa hivi hata angekuwa amejenga flyover mikoa yote na kukamilisha kabisa ujenzi wa SGR asingeweza kupata kura watu wameumizwa sana na ugumu wa maisha. Jana kuna doctor mmoja alisema kuna mgonjwa aliletwa hospitalini mme akawa amebeba kuku kwamba atauza apate pesa ya matibabu alizunguka na kuku siku nzima bila kupata mnunuzi ikabidi amuombe doctor achukuwe huyo kuku na kumtibu mgonjwa wake. Maisha kama hayo ndo mwananchi atapigia kura CCM kweli tusuburi tuone.

Mimi nimekuwa around kwa miaka zaidi ya 70. Ugumu wa maisha umekuwepo tangu nizaliwe, na jinsi siku zinavyopita kunakuwa na nafuu sehemu fulani na kluongezeka sehemu nyingine. Ugumu wa maisha unachangiwa na sababu nyingi. Pia tukumbuke huo ugumu wa maisha unaongelewa mara nyingi ni wa wapiga "deal" ambao hutegemea ufisadi kupata pesa. Mara nyingi ukisikia hao wanalia ugumu wa maisha, maana yake ni kuwa njia za ufisadi zimefungwa na pesa inapatikana tu kwa kufanya kazi.
 
Lissu atashangazwa kivipi wakati kwa opinion poll anaongoza kwa asilimia 70+. Hakuna namna magufuli anaweza mshinda Tundu Lissu ndugu yangu nakwambia. There is no way. Never

This is day dreaming.
 
Mkuu,,! Tangu technology hii ya simu za smart iingie nchini utaona tangu 2015 chadema ni washindi wa mitandaoni!

Ccm si watu wa makelele, kuna vigogo wako huko ccm wanajua nini cha kufanya ili kupata ushindi! Wanajua ushindi hauko kwenye kelele za mitandaoni kama chadema wafanyavyo!

Kingine, mashabiki wa Lisu hawana tofauti na wale wa Bob Wine yule wa uganda!
Ni mashabiki mihemuko, hutawaona kwenye foreni ya kupiga kura! Mfano kuna mmoja humu ni mshabiki wa Lisu na anajipinda kweli kushambulia hapa jf, lakini juzi nlishangaa anaulizia kitambulisho cha kupigia kura atakipataje [emoji3][emoji3][emoji3][emoji3].
Hao ndio mashabiki wa chadema.

Kwangu mimi 2015 ilinipa somo kubwa sana na inafanya nisiwe na wasiwasi juu ya ushindi wa ccm hapo oktoba.
Wewe unafikiri kitoto sana, eti wa mitandaoni. Wanalala wapi humo mitandaoni? Si ni watu kama wewe, ni wapiga kura kama wewe. Tukusaidie cha kusema ili ueleweke, labda hoja yako ungeiweka hivi'' ccm wanatumia ujinga wa baadhi wa baadhi ya watu, tume ya uchaguzi na matumizi mabaya ya vyombo vyetu vya usalama kupata ushindi wa kulazimisha (rejea mambo ya kuudhi ya Jecha 2015, nk)
 
Wapiga kura waliojiandikisha ni takribani milioni 29 wametapakaa vijiji elfu 12 na miji yote wakinufaika na mambo aliyoyafanya JPM
. Walioko mitandaoni ni sehemu ndogo sana ya wapiga kura.

JPM ana mtaji wa kutosha wa mamilioni ya wapiga kura vijijini na mijini wanaonufaika na huduma za afya katika zahanati na vituo vya afya kila kijiji na kata, hospitali za wilaya na mikoa zilizojengwa, kukarabatiwa na kupewa madaktari bingwa na madaktari wapya kuajiriwa; elimu bure kuanzia chekechea hadi form IV, huduma za maji safi sehemu nyingi na zile anbazo bado miradi ya maji inajengwa na iko mbioni kukamilika; barabara za lami zimekamilika na zingine zinaendelea kujengwa; madaraja yanayounganisha wilaya na wilaya yamejengwa na mengine yanaendelea kujengwa; meli mpya katika maziwa makuu, bandari katika maziwa makuu zinajengwa na kupanuliwa; relu ya kisasa ya SGR, umeme wa Stigler gorge na wa vyanzo vya gesi Kinyerezi II na kwingineko; stand za mabasi na masoko ya mazao ya wakulima yamejengwa. Hayo ni baadhi tu ya mambo yatakayombeba asubuhi kweupe anashinda tena kwa kishindo.
Ninyi ndio mnampoteza Magu wallah...kwa unafiki wenu huo.
 
Mimi nimekuwa around kwa miaka zaidi ya 70. Ugumu wa maisha umekuwepo tangu nizaliwe, na jinsi siku zinavyopita kunakuwa na nafuu sehemu fulani na kluongezeka sehemu nyingine. Ugumu wa maisha unachangiwa na sababu nyingi. Pia tukumbuke huo ugumu wa maisha unaongelewa mara nyingi ni wa wapiga "deal" ambao hutegemea ufisadi kupata pesa. Mara nyingi ukisikia hao wanalia ugumu wa maisha, maana yake ni kuwa njia za ufisadi zimefungwa na pesa inapatikana tu kwa kufanya kazi.
Watu na kazi zao banaa. Embu tuache sisi ambao tupo mtaani tangu 2015 tukisugua bench.
 
Wapiga kura waliojiandikisha ni takribani milioni 29 wametapakaa vijiji elfu 12 na miji yote wakinufaika na mambo aliyoyafanya JPM
. Walioko mitandaoni ni sehemu ndogo sana ya wapiga kura.

JPM ana mtaji wa kutosha wa mamilioni ya wapiga kura vijijini na mijini wanaonufaika na huduma za afya katika zahanati na vituo vya afya kila kijiji na kata, hospitali za wilaya na mikoa zilizojengwa, kukarabatiwa na kupewa madaktari bingwa na madaktari wapya kuajiriwa; elimu bure kuanzia chekechea hadi form IV, huduma za maji safi sehemu nyingi na zile anbazo bado miradi ya maji inajengwa na iko mbioni kukamilika; barabara za lami zimekamilika na zingine zinaendelea kujengwa; madaraja yanayounganisha wilaya na wilaya yamejengwa na mengine yanaendelea kujengwa; meli mpya katika maziwa makuu, bandari katika maziwa makuu zinajengwa na kupanuliwa; relu ya kisasa ya SGR, umeme wa Stigler gorge na wa vyanzo vya gesi Kinyerezi II na kwingineko; stand za mabasi na masoko ya mazao ya wakulima yamejengwa. Hayo ni baadhi tu ya mambo yatakayombeba asubuhi kweupe anashinda tena kwa kishindo.
SGR stand za bus sijui masoko yote haya yatamsaidia mtu aishiye kijijini Aliyelima kufa na kupona auze mazao ampelekee mtoto shule lakini aliambulia kudhulumiwa hakuna masoko ya kuuza mazao kodi zimezidi mtoto hajaweza kwenda shule wote wapo shambani kujilimia wapate chakula wasife njaa.
Tatizo lenu mnaona WaTz wajiiinga
Eti reli barabara madaraja ndege hivi vyote havina faida kwa mkulima na mfugaji hata mfanyabiashara mmetuchosha na hadithi zenu za alfu ulelaulela......
 
Hoja zako ni za kijiweni. Hicho chakula unachokula hapa mjini kinatoka wapi kama hakuna masoko? Umecheki data za export za mazao mbalimbali against priduction? Fungua website za World bank, UNCTAD utazame data japo nina shaka kama unaweza hata kufanya analysis maana nikikuambia tazama data za TRA, NBS na BOT utasema zimepikwa. Hali nzuri sio watu kufaidika na wizi au mnyororo wa wizi na ufisadi.
Unaposema hali mbaya unatakiwa ulinganishe na kwa kutumia data.
Unashindwa kuona bavkward and forward linkage ya ujenzi wa miundombinu ya reli, barabara, viwanja vya ndege, masoko nk katika kumnufaisha mkulima au mtu wa kijijin au wa mjini? Sio kila mtu ni mchumi au anaujua uchumi.
Kama unafikiri maisha mazuri yatashuka kama mvua nakuhakikishia mpaka unakufa hutayapata hata atawale nani.
Kwa level yako nenda katika soko lolote asubuhi uone malori yanavyoshusha mazao toka vijijini.
 
Inamaanisha kuwa nchi hii ya Tanzania ilijipatia Uhuru wake 2015?Ilikuwa koloni LA Old CCM na sasa imepata mkombozi CCM Mpya?
Tulikuwa na reli ya Dar-Kigoma and Mwanza via Tabora.Nyingine Tabora-Mpanda.Dar-Moshi and Tanga,SGR ya TAZARA toka Dar-Kapiri mposhi Zambia na pia kuna ile ya kusini Lindi-Mtwara.Acha usafiri wa Barabara za kuunganisha mikoa yote kabla huyu MTU wenu hajaingia 2015,kufanya nini zaidi kuwazidi waliomtangulia?CCM ndiyo iliyokuwa madarakani miaka yote baada ya TANU&ASP,mnataka kutuaminisha kuwa Mwl.Nyerere,Mzee Mwinyi,Mzee Mkapa(RIP) na Mzee J.M Kikwete walikuwa wazembe?Acheni kuwatukana Wazee hawa kwa manufaa ya Mtu wenu.
Watanzania tuamke,ulaghai hauwezi kutusaidia.Chagua Viongozi wenye Utu,wanaozingatia Usawa na watenda Haki na siyo Watawala.
 
Mimi nimekuwa around kwa miaka zaidi ya 70. Ugumu wa maisha umekuwepo tangu nizaliwe, na jinsi siku zinavyopita kunakuwa na nafuu sehemu fulani na kluongezeka sehemu nyingine. Ugumu wa maisha unachangiwa na sababu nyingi. Pia tukumbuke huo ugumu wa maisha unaongelewa mara nyingi ni wa wapiga "deal" ambao hutegemea ufisadi kupata pesa. Mara nyingi ukisikia hao wanalia ugumu wa maisha, maana yake ni kuwa njia za ufisadi zimefungwa na pesa inapatikana tu kwa kufanya kazi.

Hii kauli ya "ugumu wa maisha" inayosemwa semwa sana huko CCM kuwa ni ya "wapiga deal, waliozoea kula rushwa", it sounds awkward always....!!

Hivi mkulima huyu wa korosho na mbaazi wa Tandahimba, Mtwara, na Lindi...

Wakulima wa zao la mkonge wa Tanga na Morogoro....

Wakulima wa zao la pamba wa mikoa ya Tabora, Simiyu, Mwanza, Geita, Shinyanga, Mara na Singida....

Utaiwaitaje ni wala rushwa na wapiga deal na hawafanyi kazi wakati hali zao ngumu za kimaisha zimesababishwa na SERA na MAAMUZI ya hovyo ya Rais Magufuli na CCM yake??

Kama ndivyo unavyofikiri ndugu yangu, basi wewe una shida ktk ubongo wako haijalishi una umri gani Mzee au kijana....!!
 
Usimjaribu yesu wa chattle 🤣 🤣
Mmekosa majina mengine hadi mtumie YESU? Kuweni na adabu unapotaja Hilo jina uwe unafikiri kabla,Kuna wakati mnawakosesha sapoti wagombea wenu sababu ya upuuzi wa wapambe wasio na hekima Kama wewe
 
Mkuu,,! Tangu technology hii ya simu za smart iingie nchini utaona tangu 2015 chadema ni washindi wa mitandaoni!

Ccm si watu wa makelele, kuna vigogo wako huko ccm wanajua nini cha kufanya ili kupata ushindi! Wanajua ushindi hauko kwenye kelele za mitandaoni kama chadema wafanyavyo!

Kingine, mashabiki wa Lisu hawana tofauti na wale wa Bob Wine yule wa uganda!
Ni mashabiki mihemuko, hutawaona kwenye foreni ya kupiga kura! Mfano kuna mmoja humu ni mshabiki wa Lisu na anajipinda kweli kushambulia hapa jf, lakini juzi nlishangaa anaulizia kitambulisho cha kupigia kura atakipataje [emoji3][emoji3][emoji3][emoji3].
Hao ndio mashabiki wa chadema.

Kwangu mimi 2015 ilinipa somo kubwa sana na inafanya nisiwe na wasiwasi juu ya ushindi wa ccm hapo oktoba.
mwaka 2015 JPM alipata kura 54000 tu Dsm nzima .hili halijatangazwa popote. wewe kwa ujinga wako unadhani mitandao haina nguvu bado. kalagabaho
 
This is very interesting, kwa kweli...

Kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi ya Taifa (NEC), kampeni rasmi za kila mgombea za nchi kavu, angani au majini za kutembea kijiji kwa kijiji, kata kwa kata, jimbo kwa jimbo Tanzania nzima zitaanza trh 26/8/2020....

Lakini kampeni zisizo rasmi za MTU kwa MTU au NYUMBA kwa NYUMBA na hasahasa za kupitia mitandao ya kijamii (social media) zenyewe hazihitaji ruhusa ya mtu ama chombo chochote cha kisheria. Hizi zilishaanza muda mrefu tangu ama pengine labda kabla hata ya mwezi May, 2020...

Nimefanya utafiti wangu fast fast kwa kupitia baadhi mitandao ya kijamii maarufu zaidi kama JF, Instagram, Twitter, Facebook, Telegram, YouTube nk, mjadala unao - trend kwa sana ni uchaguzi mkuu Tanzania - 2020....

Mijadala hii inawahusisha wagombea wawili; Tundu Lissu (CHADEMA) na Magufuli Pombe ( CCM)....

Kwa uwazi kabisa, mtu aweza kusema kuwa ni timu mbili zinazotifuana na kupambana vilivyo....

Upande huu ipo TEAM TUNDU LISSU - CHADEMA + vyama shindani vilivyo nje ya serikali...

Upande wa pili ipo TEAM POMBE MAGUFULI + serikali nzima + NEC + baadhi ya TISS waasi wa ethics za utumishi wao + baadhi ya maafisa wa polisi waasi wa ethics za Utumishi wao + mahakama ikihusisha baadhi ya Mahakimu/majaji waasi wa ethics zao za utumishi + Msajili wa vyama vya siasa + vyama washirika vilivyo nje ya serikali kama UDP ya Cheyo, TLP ya Mrema, NCCR - Mageuzi ya Mbatia na vingine...

JWTZ sitawaingiza hapa kwa sababu, ktk uchaguzi wa mwaka huu 2020, hawa wameshatoa clear statement kuwa, JESHI HALINA CHAMA CHA SIASA. Kwa hiyo tunawapa "benefit of doubt" ya kuwa wanamaanisha walichokisema....

Mijadala ni mikali sana ktk kila mtandao. Upepo unaonekana kuivumia vibaya TEAM POMBE MAGUFULI - CCM. Wanaonekana kuzidiwa kwa hoja ktk kila idara na mpinzani wao TEAM TUNDU LISSU - CHADEMA....

Sasa waneona, the best option kwao ni kuanza kurusha matusi ya nguoni wakijifaragua na kudhani hiyo ndiyo njia ya ku - neutralize hoja za washindani wao. Huu ni utoto wa shule....!

Imefikia mahali wanatishia kuua mtu kwa RISASI za SMG ama AK47. Na pia wanatisha vyombo vya habari Redio na TV kutorusha lolote kuhusu Tundu Lissu. Magazeti yote neutral yalishauwawa na kuzikwa. Kwa kweli hali ya mgombea wao na CCM kwa ujumla haileti matumaini SI NZURI, ni MAHUTUTI inaweza "kufa" wakati wowote....!

Mtifuano wa timu hizi mbili wiki mbili zilizopita ulikuwa unaonesha kuwa PRAISE TEAM MAGUFULI - CCM ingeweza ushinda kwa goli la mkono huku TEAM TUNDU LISSU - CHADEMA, wachezaji wake wakiwa wanyonge na wasio na ari ya mchezo kabisa kutokana na mashambulizi ya wapinzani wao....

Wapinzani wa TEAM TUNDU LISSU - CHADEMA yaani TEAM MAGUFULI - CCM ktk namna fulani ya ajabu, ilianza kupata "back up" kutoka TEAM MEMBE - ACT WAZALENDO....

Lakini baada ya ujio wa Tundu Lissu, hiyo "back up" haina kazi tena. Iko kila dalili kuwa, TIMU MEMBE itaungana na TIMU LISSU dhidi ya TIMU POMBE - CCM....

Mashambulizi ya TEAM PRAISE MAGUFULI - CCM yalilenga zaidi kukata stimu na ari ya TEAM TUNDU LISSU. Hoja zao zilikuwa hizi. Kwamba, TUNDU LISSU;

å Hawezi kurudi huyo toka Ubelgiji...

å Ni mkimbizi wa kisiasa huyo, harudi TZ ...

å Kanunuliwa na "mabeberu" huyo, harudi....

å Akija lazima tumuue huyo, na safari hii hatukosei target...

å Akija huyo, pingu zinamsubiri hapohapo uwanja wa ndege....

Eti hoja yao ikiwa ni "kwa kuichafua serikali na Rais wao" akiwa nje ya nchi....

Looh, hawa jamaa mazuzu kweli kweli. Na hawa eti ndiyo "think tank" ya "JIWE" naarufu kama LB7 FC..!!

å Akija, hana sifa ya "kimaadili" ya kugombea Ubunge ama Urais....!!

HOJA hizi ziliinyong'onyeza kuvunja ari ya mpambano kabisa TEAM TUNDU LISSU - CHADEMA....

Tangazo la kurudi nyumbani tarehe 27/7/2020 la Tundu Lissu, lilianza kuamusha ari ya vita ya TEAM TUNDU LISSU - CHADEMA....

Matumaini ya TEAM TUNDU LISSU - CHADEMA yaliyokuwa ya mashaka, yaligeuka kuwa ya KWELI, HALISI na HAKIKA tarehe 27/7/2020 saa 7.30mchana pale Tundu Lissu alipoikanyaga ardhi ya Tanzania baada ya miaka mitatu kuwa nje kwa matibabu...

Hii iligeuza kabisa sura ya mpambano. Unyonge, kunyong'onyea na kukata tamaa na kukosa ari ukawa upande wa TEAM POMBE MAGUFULI - CCM. Wakawa "paralyzed" ghafla wasijue nini cha kufanya. Ndipo walipogundua kuwa assumptions zao zote zile hapo juu kwa wafuasi wao ilikuwa ni UONGO na KUWALISHA upepo tu....!

Mgeuko huu hasi na wa ghafla dhidi ya PRAISE TEAM MAGUFULI - CCM ukanikumbusha fainali ya mwaka 2004/2005 ya UEFA Champion League kati ya AC MILAN FC (Italy) vs LIVERPOOL FC (England)...

Hii ilikuwa moja ya historical UEFA Champion League finals kuwahi kushuhudiwa na wapenzi wa soka duniani...

Mpaka kipindi cha kwanza kinaisha, AC MILAN FC walikuwa mbele kwa goli 3 huku LIVERPOOL FC wakiwa hawana goli (0)...

Second period ilipoanza, wapenzi wa AC MILAN na wachezaji wao, hawakuamini kilichotokea uwanjani. Liverpool FC, walirudisha goli zote hadi dakika 45 za kipindi cha pili zinamalizika....

Dakika 30 zikaongezwa bila mshindi kupatikana. Wakaingia kwenye matuta (penalties). Liverpool FC wakiubuka kidedea kwa ushindi wa penalties 4 - 2 na kutawazwa mabingwa wa Ulaya msimu wa 2004/2005....!!

Huu mpambano wa TUNDU LISSU vs POMBE MAGUFULI naufananisha pia na fainali hii. Tundu Lissu - CHADEMA (Liverpool FC) na Pombe Magufuli - CCM (AC Milan FC)....

Mpaka mwezi Jana (July), Team Pombe Magufuli - CCM walikuwa mbele kwa goli 3 bila. Wiki mbili tu zimepita, Team Tundu Lissu - CHADEMA wamesharudisha goli zote. Tupo kwenye penalty shoot out na mpaka sasa LIVERPOOL FC TEAM TUNDU LISSU wanaongoza kwa goal penalty 3 dhidi ya 1 PRAISE TEAM MAGUFULI - CCM....

Mashabiki wa TEAM POMBE MAFUGULI CCM hawaamini kinachotokea. Vichwa vimeinama chini. Wenye roho ndogo wanarusha chupa za maji uwanjani. Wengine wanarusha matusi kwa wapinzani wao na wachezaji na kocha wao wakiwatuhumu kwa uzembe..

Kwa kifupi hali si shwari kabisa kwa TEAM POMBE - CCM. Ishara na dalili zote zinaonesha kuwa wanapoteza pambano hili ambalo walilitawala sana kipindi cha kwanza....!!

Heko TEAM TUNDU A.M LISSU - CHADEMA....
Kipi atakachokifanya Tundu Antipasi Lissu akishapewa dhamana ya kuongoza nchi??
 
Mmekosa majina mengine hadi mtumie YESU? Kuweni na adabu unapotaja Hilo jina uwe unafikiri kabla,Kuna wakati mnawakosesha sapoti wagombea wenu sababu ya upuuzi wa wapambe wasio na hekima Kama wewe
gufuli ni yesu wa chattle au vipi 😁 😁
 
JPM katili sana, ndiye aliyebariki shambulio la Lissu kuchapwa zile mvua za risasi. Muda ukifika tutaweka wazi kila kitu.
 
Back
Top Bottom