Kampuni ya Adani yasaini Mkataba wa miaka 30 kuendesha Gati ya 2 ya Bandari (Zamani TICTS)

Kampuni ya Adani yasaini Mkataba wa miaka 30 kuendesha Gati ya 2 ya Bandari (Zamani TICTS)

Hivi hakuna mtanzania mzawa aliyeweza kuchukua na kuwekeza
Kwenye gati hilo
Au sisi wazawa tunachoweza ni kukataa mauno tu 😄 na kufungua mabar

Ova
Nimepitia kwa haraka haraka Adani ataendesha hiyo gati kupitia TICTS maana ndiye ana mitambo na muajiri mkuu 😃 Karamagi bado anaendelea kulisongesha gurudumu 🔥🔥🔥
 
Mama waleteeeeeee!

Mpaka maji wayaite mma!

View attachment 3005299
20231224_095052.jpg
 
JPM alikataa bandari ya Bagamoyo na in 3 years alizamisha billioni mbili na zaidi ili kuimarisha bandari ya Dar ifanye kazi Kwa uhakika, na ndio maana SGR ilijengwa ili kupiga Cargo zote za Rwanda, Burundi mpaka Congo na Barabara za kusini zikaimalishwa ili mizigo iingie Malawi,Zambia etc bila shida, sasa kazi yote na capital yote imeenda bure, Leo wanakuja kugawana wapumbavu tuu na mikataba yao isiyoeleweka
Akili za kijamaa hizi, zimeshapitwa na wakati.

Una reli ya SGR ya kisasa inayouleta mzgo huku bandarini kwa kasi kubwa huwezi tena kuendelea kufanya kazi kwa ufanisi ule ule wa kizamani.
 
zamani zile tulijifunza shuleni habari ya njia kuu za uchumi kumilikiwa na wageni.. sasa hii ndio practical stage mkuu..
Sisi wenyewe tunafanya vituko na wizi acha wageni waje watufundishe namna ya kufanya kazi.

Jaji wa mahakama kuu anakuwa sehemu ya njama ya kudhulumu wamiliki halali wa viwanja, wacha wageni waje watunyooshe.

Kiwanja cha brother hapa mbezi beach wanamzungusha kumpa hati kumbe wanacheza mchezo wa kutaka kumuibia waziri kaingilia kati hivi sasa michakato ya kumpatia hati inakwenda kwa kasi, acha kabisa nchi iendeshwe na wawekezaji wenye uwezo sisi ni kelele na ushenzi wa kudhulumiana.
 
Kwa jinsi ambavyo vyoo vya stendi na sokoni havioshwi ni bora viuzwe tu. Sijawahi kuona nchi ya walalamikaji kama Tanzania.

Uvivu nyinyi, uzembe nyinyi, wizi nyinyi, na bado mnataka raslimali zisiuzwe??? HAIWEZEKANI
Nchi ina wapumbavu wengi hii acha hao wageni waje wainyooshe bandari yetu. Ukiona nyuzi nyingi za kuhoji kuhusu muungano jua ni hao hao wapigaji wa TPA wana hasira za kukosa ulaji wa bure kutoka kwenye bandari ya wajinga.
 
Kabakiza kugawa Bagamoyo port, SGR na gas; mengine yote keshauza misitu, mabasi, migodi ilyokuwa reserved na bado anakopa.

Huku wanagawa cash cow assets, halafu huko bungeni wanawaza kodi kwa watu maskini.

Only in Tanzania
Halafu utakuta wanagawiana wahuni wa humu humu nchini

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Sisi wenyewe tunafanya vituko na wizi acha wageni waje watufundishe namna ya kufanya kazi.

Jaji wa mahakama kuu anakuwa sehemu ya njama ya kudhulumu wamiliki halali wa viwanja, wacha wageni waje watunyooshe.

Kiwanja cha brother hapa mbezi beach wanamzungusha kumpa hati kumbe wanacheza mchezo wa kutaka kumuibia waziri kaingilia kati hivi sasa michakato ya kumpatia hati inakwenda kwa kasi, acha kabisa nchi iendeshwe na wawekezaji wenye uwezo sisi ni kelele na ushenzi wa kudhulumiana.
Sisi tuendele kukata mauno,uumbea udaku,kushabikia simba yanga konde mondi zuchu
Tukifungua bar na gesti ndiyo moradi mikubwa kwetu 😄

Ova
 
Nchi ina wapumbavu wengi hii acha hao wageni waje wainyooshe bandari yetu. Ukiona nyuzi nyingi za kuhoji kuhusu muungano jua ni hao hao wapigaji wa TPA wana hasira za kukosa ulaji wa bure kutoka kwenye bandari ya wajinga.
Hakuna anayechukia wawekezaji, tatizo ni hiyo mikataba yote ni wizi mtupu na haina faida yeyote zaidi ya 10% za wapigaji, pitia mikataba ya ndege mpaka dhahabu ni uchafu mtupu na hasara kubwa kwa Taifa
 
unaishi nchi gani dogo,
Kuna watu wameuwawa Kuna watu ni vilema , Kuna watu ni wakimbizi, kwa kupinga uwekezaji unaodai ni wa wazungu,

mtu mwenye akili timamu anapinga uovu bila kuangalia umefanywa na nani? Madhara ya kuwakaribisha wazungu ni sawa na kuwakadrbisha waarabu wote wanyonyaji tu.

Nyie kwenye dini yenu mwarabu akifanya ouvu mnatukuza na kuabudu
Nani kapata ulemavu kupinga uwekezaji wa mzungu!?..maana kifo ni hatua kubwa,hiyo ya ulemavu tu nataka
 
Back
Top Bottom