Kampuni ya ICTE kutoka Ufilipino imeshinda tenda kuendesha bandari ya Darbun, SA kwa miaka 25

Kampuni ya ICTE kutoka Ufilipino imeshinda tenda kuendesha bandari ya Darbun, SA kwa miaka 25

The Assassin

JF-Expert Member
Joined
Oct 30, 2018
Posts
4,942
Reaction score
20,077
Kampuni ya uendeshaji wa shughuli za bandari ya International Container Terminal Services kutoka Ufilipino imeshinda kandarasi ya kuendesha bandari ya Durban nchini Afrika Kusini kwa kandarasi ya miaka 25.

Swali, kwa nini sisi DP World hatuambiwi watafanya kazi kwa muda gani?

=======
Philippine giant wins bid to run Durban port's container terminalTransnet has selected Manila-headquartered International Container Terminal Services (ICTSI) as the preferred bidder for a joint venture to develop and upgrade the flagship Durban Container Terminal Pier 2.Over a 25-year term, ICTSI will partner with Transnet Port Terminals (TPT) to develop and upgrade Transnet’s biggest container terminal, handling 72% of the Port of Durban’s throughput and 46% of South Africa’s port traffic.
1689726493793.png
 
Watanganyika wakihoji mkataba wa dpw ni wa miaka mingapi wenye mamlaka wanamsingizia Mungu kwamba amewapa mtihani.
Mkataba wa uendeshaji wa bandari kati ya Dp world na TPA bado, hatua hio itakavyofikia muda wa mkataba na mambo mengine yatawekwa humo. Mkataba ulioridhiwa na Bunge unahusu mashirikiano kati ya Dubai na Tanzania.
 
Kampuni ya uendeshaji wa shughuli za bandari ya International Container Terminal Services kutoka Ufilipino imeshinda kandarasi ya kuendesha bandari ya Durban nchini Afrika Kusini kwa kandarasi ya miaka 25.

Swali, kwa nini sisi DP World hatuambiwi watafanya kazi kwa muda gani?

=======
Philippine giant wins bid to run Durban port's container terminalTransnet has selected Manila-headquartered International Container Terminal Services (ICTSI) as the preferred bidder for a joint venture to develop and upgrade the flagship Durban Container Terminal Pier 2.Over a 25-year term, ICTSI will partner with Transnet Port Terminals (TPT) to develop and upgrade Transnet’s biggest container terminal, handling 72% of the Port of Durban’s throughput and 46% of South Africa’s port traffic.
View attachment 2692567
Jamani kwani mpaka leo hatujui nini kimejiri mpaka diipiiwed anabebwa kwa mbeleko kubwa kiasi hiki? Tutaishia marungu tuu
006c208b814e2000402713af243c5c13.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkataba wa uendeshaji wa bandari kati ya Dp world na TPA bado, hatua hio itakavyofikia muda wa mkataba na mambo mengine yatawekwa humo. Mkataba ulioridhiwa na Bunge unahusu mashirikiano kati ya Dubai na Tanzania.
Bahati mbaya kwa upande wenu enyi mawakili upande wa utetezi HAMUAMINIKI kwa kuwa MAJIBU yenu kwenye hoja hizi ngumu huwa YANAPISHANA kila siku. Sijui hamkai pamoja chumba cha siri na mtoke nje na jibu moja? Aliuza wakili msomi "Ni nini kinachopitishwa na bunge (kisheria) kati ya vitu hivi viwili 1. MAKUBALIANO 2. MKATABA. Jibu ni mkataba" Na nini tofauti ya vitu hivi viwili?. Kwa ujumla HAMJAELEWEKA KABISA.
 
Mkataba wa uendeshaji wa bandari kati ya Dp world na TPA bado, hatua hio itakavyofikia muda wa mkataba na mambo mengine yatawekwa humo. Mkataba ulioridhiwa na Bunge unahusu mashirikiano kati ya Dubai na Tanzania.
Dubai sio nchi..
 
Afrika Kusini inakusudia kubinafsisha shughuli za bandari katika mpango wa muda mrefu ili kuboresha shughuli na kuongeza ufanisi kutokana na bandari hizo kukosolewa kwa muda mrefu kwa kutofanya kazi vizuri, miundombinu iliyochakaa na msongamano.

Transnet, kampuni inayomilikiwa na serikali ambayo inahusika na bandari na mfumo wa usafirishaji, ilitangaza kuichagua kampuni ya Kimataifa ya Huduma za Makontena ya Kimataifa (ICTSI) kutoka Ufilipino kama mnunuzi aliyechaguliwa kwa ubinafsishaji wa bandari ya makontena ya Durban kwenye Gati 2, mchakato ulioanza mwaka 2021.

Baada ya kufanya mapitio ya kampuni zilizowasilisha maombi, Transnet iliripoti kuwa imechagua ICTSI na itaunda kampuni mpya ya pamoja kwa ajili ya uendeshaji wa gati hiyo. Transnet itamiliki zaidi ya asilimia 50 ya kampuni mpya ambayo itakuwa na mkataba wa miaka 25 ambao unaweza kuongezwa hadi miaka 30 kulingana na wakati wa operesheni ya kuongeza kina katika Gati ya Kaskazini kwenye Gati 2.

"Ushiriki wa sekta binafsi kwenye Gati 2 ni muhimu sana katika kubadilisha upya Bandari ya Durban kuwa bandari kuu ya makontena. Ushirikiano katika Gati 2 ni hatua kubwa kwenye programu yetu ya kuwaleta wataalamu wa kimataifa kuboresha ufanisi katika bandari zetu, na inakuza vizuri mipango yetu ya kuhamasisha sekta binafsi katika maeneo yaliyotambuliwa kwa ukuaji," amesema Portia Derby, Afisa Mtendaji Mkuu wa Kundi la Transnet.

Wakati wa kutangaza makubaliano hayo, walibainisha kuwa si tu itaboresha upangaji wa vifaa katika bandari za Afrika Kusini lakini pia itachangia sana katika kuchochea biashara ya kuuza nje na kuagiza. Durban imekuwa ikipoteza shehena katika miaka ya hivi karibuni kutokana na changamoto zake za uendeshaji.

Chanzo: Swahili Times
 
Afrika Kusini inakusudia kubinafsisha shughuli za bandari katika mpango wa muda mrefu ili kuboresha shughuli na kuongeza ufanisi kutokana na bandari hizo kukosolewa kwa muda mrefu kwa kutofanya kazi vizuri, miundombinu iliyochakaa na msongamano.

Transnet, kampuni inayomilikiwa na serikali ambayo inahusika na bandari na mfumo wa usafirishaji, ilitangaza kuichagua kampuni ya Kimataifa ya Huduma za Makontena ya Kimataifa (ICTSI) kutoka Ufilipino kama mnunuzi aliyechaguliwa kwa ubinafsishaji wa bandari ya makontena ya Durban kwenye Gati 2, mchakato ulioanza mwaka 2021. Baada ya kufanya mapitio ya kampuni zilizowasilisha maombi, Transnet iliripoti kuwa imechagua ICTSI na itaunda kampuni mpya ya pamoja kwa ajili ya uendeshaji wa gati hiyo.

Transnet itamiliki zaidi ya asilimia 50 ya kampuni mpya ambayo itakuwa na mkataba wa miaka 25 ambao unaweza kuongezwa hadi miaka 30 kulingana na wakati wa operesheni ya kuongeza kina katika Gati ya Kaskazini kwenye Gati 2. "Ushiriki wa sekta binafsi kwenye Gati 2 ni muhimu sana katika kubadilisha upya Bandari ya Durban kuwa bandari kuu ya makontena.

Ushirikiano katika Gati 2 ni hatua kubwa kwenye programu yetu ya kuwaleta wataalamu wa kimataifa kuboresha ufanisi katika bandari zetu, na inakuza vizuri mipango yetu ya kuhamasisha sekta binafsi katika maeneo yaliyotambuliwa kwa ukuaji," amesema Portia Derby, Afisa Mtendaji Mkuu wa Kundi la Transnet.

Wakati wa kutangaza makubaliano hayo, walibainisha kuwa si tu itaboresha upangaji wa vifaa katika bandari za Afrika Kusini lakini pia itachangia sana katika kuchochea biashara ya kuuza nje na kuagiza

Durban imekuwa ikipoteza shehena katika miaka ya hivi karibuni kutokana na changamoto zake za uendeshaji.
 
Mkataba wa uendeshaji wa bandari kati ya Dp world na TPA bado, hatua hio itakavyofikia muda wa mkataba na mambo mengine yatawekwa humo. Mkataba ulioridhiwa na Bunge unahusu mashirikiano kati ya Dubai na Tanzania.
Kichwan bado mtupu sana , mkataba bado mara mkataba wa mashirikiano ( kwenye nini ? Na kwann mashirikiano yasiwe na muda ?) Ebu amka asee , bado mtupu kbs kichwan , bungen huenda kitu kitakacho fanyiwa kaz ( elewa makubaliano kwenye maandishi ambayo yana guide ushirikiano -Mkataba ) USIPENDE KUSIKILIZA BILA AKIL YAKO KUCHAKACHUA
 
Back
Top Bottom