Kampuni ya New Habari yasitisha uchapishaji wa Magazeti yake kufuatia mwenendo mbaya wa biashara

Kampuni ya New Habari yasitisha uchapishaji wa Magazeti yake kufuatia mwenendo mbaya wa biashara

Ni nani anunue magazeti ya ccm? Wakawauzie wanasisiem wenzao; si wao wanajioma wajanja? Na bado tutasusa mpaka mtajuta kumtukuza shetan wenu huyo mnayemwita laic.
 
Kampuni ya New Habari imetangaza kusitisha utoaji wa magazeti yake kuanzia Jumatatu ijayo kutokana na mwenendo mbaya wa biashara.

========

NEW HABARI YASITISHA UZALISHAJI MAGAZETI

KAMPUNI ya New Habari 2006 LTD inayozalisha magazeti ya Mtanzania, Rai, Bingwa na Dimba imetangaza kusitisha uzalishaji wa magazeti yote kutokana na mwenendo mbaya wa biashara.

Akizungumza na wafanyakazi wa kampuni hiyo Mhariri Mtendaji, Dennis Msacky amesema uzalishaji wa magazeti hayo utasitishwa kuanzia Jumatatu wiki ijayo.
Huku tunapoelekea makampuni mengi ya habari yatafunga maana wananchi wanachoka kusoma habari zenye mlengo mmoja, yani za kuisifu serikali tu, hakuna uadilifu katika uandishi, ni bias tupu, sasa nani anunua gazeti, mwisho wa siku wanapata hasara, litabaki gazeti la serikali na la CCM tu
 
Kampuni ya New Habari imetangaza kusitisha utoaji wa magazeti yake kuanzia Jumatatu ijayo kutokana na mwenendo mbaya wa biashara.

========

NEW HABARI YASITISHA UZALISHAJI MAGAZETI

KAMPUNI ya New Habari 2006 LTD inayozalisha magazeti ya Mtanzania, Rai, Bingwa na Dimba imetangaza kusitisha uzalishaji wa magazeti yote kutokana na mwenendo mbaya wa biashara.

Akizungumza na wafanyakazi wa kampuni hiyo Mhariri Mtendaji, Dennis Msacky amesema uzalishaji wa magazeti hayo utasitishwa kuanzia Jumatatu wiki ijayo.
Sasa kama magazeti yote ya serikali na binafsi yanafanana kwa vichwa vya habari unadhani nani atanunua zaidi ya gazeti moja kwa siku!!
 
Mbona hii mitano tena imeanza kuwa migumu mapema hivyo? Hapo ajira ngapi zinapotea? Tukisema uwekezaji Tanzania mgumu watu wanakataa
 
Matokeo ya habari za mrengo mmoja mmeziona wenyewe.
IMG_20201204_174317.jpg


Mimi toka habari zianze kupitia kwa Dr. Abbas na kuchambua cha kuandika sikuona tena umuhimu wa magazeti.
Habari nzuri na za kweli kwa sasa zinapatikana mitandaoni tena kwenye vyanzo visivyojulikana
#NasemaUongoNduguZangu?

Kwanini ununue gazeti sasa? Kwenye hii mitano tena tuna kazi sana
Mf. Dangote akiondoka Tanzania hakuna atakayejua Nasema uongo ndugu zangu? Tuendelee kuunga mkono juhudi tu ila madhara ni ya kwetu sote.
 
Hivi kuna kampuni ya uchapazi magazeti itafanya biashara ya kuuza magazeti ambayo kila siku headlines zao ni pambio ya sifa tu kumhusu dikteta Magufuli huku jamii yote ikitambua kuwa huyu ndiye mtu asiyependwa na kuchukiwa zaidi hapa Tanzania na hivyo watu kutopenda kabisa kusikia wala kusoma habari zake?

TBC yenyewe inaendelea kuwepo na kuishi simply tu kwa sababu inapokea ruzuku 100% toka serikalini ili kujiendesha. Ingekuwa si hivi, ingelishakufa siku nyingi sana...!!

Sera za kiuchumi na kibiashara za serikali ya awamu ya tano chini ya ya CCM ya Magufuli zitaua kampuni na taasisi nyingi sana tu mpaka kufikia mwaka 2025...!

Sera za kiuchumi na kibiashara za CCM ya Magufuli hazina urafiki na sekta binafsi kabisa. Zinaiua sekta binafsi kila uchao...

Something has to be done before it's too late...
 
Na bado magazeti yote yatafungwa labda yapewe ruzuku na jiwe ukishatoka hapo tutakuja kwa wakina mawingu,chafu nk
 
Niliacha kusoma gazeti pale nilipopata smartphone na kupata habari zoote za gazetini mitandaoni
 
True hiki kizazi cha social network kimeua kabisa soko la magazeti

Makampuni yote ya habari yanapaswa kuja na mabadiliko na kuwekeza nguvu kubwa zaidi katika Platform za mitandao ya kijamii otherwise wataendelea kuangukia pua tu
Hili la social network nadhani tuliangalie upya, mimi binafsi nakataa maana hiyo mitandao imekuja zamani sana kwa wenzetu, lakini mpaka kesho wenzetu bado wanasoma magazeti,
Nchi nyingi zilizoendelea zina magazeti ambayo ni maarufu na yanasomwa, mfano New York times, The Economic n.k

Sent from my SM-G610F using JamiiForums mobile app
 
Mara ya mwisho kununua gazeti ilikuwa 2014 nilipokuwa nahitaji kuangalia ratiba ya kombe la dunia!!
 
Back
Top Bottom