Kanda ya Ziwa: Tetemeko la Ardhi la ukubwa wa 4.5 kwa vipimo vya Richa latikisa

Kanda ya Ziwa: Tetemeko la Ardhi la ukubwa wa 4.5 kwa vipimo vya Richa latikisa

Poleni...
Sasa kweli nimeamini mtukufu anapendwa na watu humu, wengi wanataka kujua kama tetemeko naye limempitia...😀
Tusihofu ile ni taasisi, na walinzi wapo makini, watalizuia tetemeko kwa KUSALI na KUJIFUKIZA.

Everyday is Saturday................... 😎
 
Hilo tetemeko japo lilichukua mda mfupi ila ni balaa.

Mimi hapa Mwanza nimelisikia vyema kabisa. Kwakweli huu mwaka kazi tunayo, huku mvua, huku korona mara matetemeko; balaa tupu.
 
Wataalamu wetu wanasemaje?

Nimeona watoa mada reference zao ni USGS (United States Geological Survey) tu, je Department ya Geology pale Dodoma (TGS Tanzania Geological Survey) hawakutoa warning kwa wakazi wa Kanda ya Ziwa? Or they didn't see this coming, kama sisi tu.
as of today, hakuna teknolojia ya kupredikti matetemeko ya ardhi duniani!!!.

ingekuwepo, basi nchi kama Japan ungekuta hawapati madhara kabisa wakati wa matetemeko...ikumbukwe nchi ya Japan hupata matetemeko makubwa ya ardhi mara kwa mara.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimelishuhudia tetemeko hili muda huo nilioutaja nikiwa Katika Wilaya ya Mbogwe ( Masumbwe) na mpaka muda huu mbwa wanabweka kuashiria tukio hilo.
Kama umelisikia na wewe kutoka popote pale tujaribu kupeana uzoefu.

Kwa majibu wa US Geological Survey tetemeko hili linaonekana kuwa na kiwango cha 4.5 na limeyokea saa 00:07 kilometa 47 kutokea Nyangwale kutoka hapa nilipo.

Duh had mwasumbwe🤔🤔🤔
 
Poleni...
Sasa kweli nimeamini mtukufu anapendwa na watu humu, wengi wanataka kujua kama tetemeko naye limempitia...😀
Tusihofu ile ni taasisi, na walinzi wapo makini, watalizuia tetemeko kwa KUSALI na KUJIFUKIZA.

Everyday is Saturday................... 😎


🤣🤣🤣🤣🤣😙coment yako imenifanya nicheke sana jamani.hahaahaj
 
Tetemeko hili ni tetetemeko jepesi/ light earth quake kutokana na ukubwa wake wa 4.5.
Tetemeko lenye ukubwa wa 4.0 -4.9 kwenye kizio cha ritcher scale hutambuliwa na baadhi ya wataalamu kuwa ni tetemeko jepesi.
Wataalamu wengine wanaona kuwa tetemeko linalozidi kiwango cha 4.5 kuwa tetemeko kubwa.

Aisee mziki wale ulikuwa si mchezo. Labda kwasababu ilikuwa usiku kumetulia. Madirisha na kila kitu ndani vilikuwa vinatingishwa mnooo.
Sasa kama hili ni dogo sijui picha ya kubwa linakuwaje.

Asante kwa maarifa mjomba/shangazi.
 
Back
Top Bottom