Kanisa Katoliki kutoa hifadhi kwa waumini wa Gwajima

Kanisa Katoliki kutoa hifadhi kwa waumini wa Gwajima

Ukisikia ukichaa ndiyo huu!!

Hivi kuteka na kuua watu ndiyo amani?

Hivi anayeteka watu na kuua, na anayekemea utekaji na mauaji, ni nani anaharibu amani ya nchi?

Au damu za watu mlizozimwaga zimewaharibu hata akili ndogo mlizokuwa nazo?
Chawaccm wao vitendo haramu vya kishetani huvigeuza kuwa ni Amani
 
Ngoma bado mbichi,haya msando agiza vijana wako wakawatoe na huko.
Wamesema wanaendelea na maombi yao hadi yatoe jawabu, sasa jawabu DC atakuwa anajiuliza kila mara kwani hajui jawabu lijalo litakuwa vipi
 
Kufuatia kufungwa kwa kanisa la Glory of Christ (Ufufuo na Uzima), viongozi wa kanisa hilo sasa wamesema wamepata hifadhi katika Kanisa Katoliki kigango cha Bikira Maria Kimara Dar es Salaam.

Akizungumza leo Julai 27 katika ibada iliyofanyika katika ukumbi wa Kilato uliopo Kimara Stop Over, kiongozi wa kanisa hilo, Askofu Baraka Tenge, amesema baada ya usumbufu wa kupata sehemu ya kuabudu sasa wamepata hifadhi hiyo.

View attachment 3420939
Awali baada ya kanisa hilo kifungwa Juni 2, 2025 waumini hao walikiwa wakikusanyika pembeni ya kanisa hilo lililopo Ubungo Kibo, lakini walifukuzwa na polisi.

Baadaye walitafuta hifadhi katika Kanisa la Kilutheri la Afrika Mashariki (KKAM), ambapo pia walifukuzwa na sasa kanisa hilo limevunjwa.

Kisha waumini hao walihamia katika Ukumbi wa Tanzanite uliopo Kimara.
Hata hivyo, Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Albert Msando alisema waumini hao wamemaliza semina hivyo waondoke.

Katika ibada ya leo Mwenyekiti wa Umoja wa Maaskofu wa Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (CPCT), Askofu Vernon Fernandes alishiriki na alihubiri.

View attachment 3420938
Hapo patamu chacha
 
Hifadhi gani watapewa na kanisa katoliki,kama ni ukumbi au eneo la kufanyia ibada zao hapo sawa,lakini kama ni kushiriki, ibada zao ziko tofauti na kuzifahamu mpaka upate mafundisho sio pungufu ya miaka 2 hadi 3, ubatizwe na kukomunika kisha kipaimara, kabla ya hapo ukiri Imani katoliki ya mitume, sasa wakifanya hayo, maana yake dhehebu lao limekufa na wao sasa wanakuwa wakristo wakatoliki, kitu ambacho sidhani kama ndilo lengo lao, hata hivyo inasikitisha watu kugeuka wakimbizi wa kidini ndani ya nchi yao wenyewe, kitu ambacho kinaweza kuepukwa kwa kukaa mezani kwa dakika chache tu, Mungu aisaidie sana hii nchi kwakweli.
Yani wawekeze miaka miwili mingine kwenye upotevu? Waoneeni huruma miaka waliyokaa kwenye upotevu imetosha msiwaalike kwenye uporevu mpya wa kuomba toba na baraka mbele ya mifuko miwili ya cement iliyochanganywa na kokoto
downloadfile.png
 
Hata huko watafukuzwa tu. Hao ni wahuni. Hawahitajiki Tanzania na Mbinguni. Na Kanisa Katoliki wakijifanya wajuaji na kuwapokea wahuni wa Gwajima nao watafungiwa!😡😡😡😡!!!!
Katoliki ifungiwe? Unaota wewe amka
 
ibirisi wa ccm badala ya kuwekeza kwenye maendeleo wapate wapiga kura wengi bila uchakachuaji, wamekalia kutumia mabilioni ya walipa kodi kuwalipa watesi waonevu watekaji wauaji watese kuwanyanyasa kuwabambikia kesi wakosoaji wa Sera mbovu za ccm, Pesa inayopigwa na mbowe, Amos makala, chawaccm kuidhoofisha kuihujumu chadema ni nyingi sana na laiti ingekuwa umetumika kujenga vyuo mashule barabara na huduma za maji kote Nchini hakika ccm wangepata wangevuna kura nyingi na kusingekuwa na haja ya kuwaonea chadema kuwabambikia kesi za uongo na mambo mengi haramu ya kishetani
 
Hata huko watafukuzwa tu. Hao ni wahuni. Hawahitajiki Tanzania na Mbinguni. Na Kanisa Katoliki wakijifanya wajuaji na kuwapokea wahuni wa Gwajima nao watafungiwa!😡😡😡😡!!!!
Kanisa Katoliki ni dude kubwa hata Rais wako Samia analijua.Hapo walipo enda wapo salama sana
 
ccm kwa sasa ni uwanja wa kula pesa kwa kisingizio cha kuwakomoa wakosoaji wa mapungufu ya ccm, chawaccm na Akina Mbowe na chauma ubwabwa wametumia fursa hizo kupiga pesa toka ccm,kila mwenye wazo Ovu la kuwahujumu chadema anakula pesa za ccm, hawataki kuamini kuwa maendeleo ndiyo njia bora ya kupata kura kuliko kuwalipa akina Mbowe na chawaccm kufanya vitendo haramu vya kishetani
 
taratibu taratibu wakristo wameanza kuungana. atabaki mwamposa na maboya peke yao. ukiona hadi wakatoliki na walokole wanaungana ujue wamefikia mahali wakaamini adui yao ni mmoja. serikali inakotupeleka sio kuzuri. wafanyeje sasa manake maaskofu wa katoliki wanawindwa na kufuatilia hadi na magari, kwa sababu tu wamehubiri, mapadre wanavamiwa na kupigwa, hadi imefikia mahala siasa zimezuiwa, ila samia bado tu haelewi anakoipeleka nchi.
Udini
 
Back
Top Bottom