Kanisa Katoliki lapoteza Mapadri 25 na Watawa 60 kwa tatizo la upumuaji ndani ya miezi miwili

Aiseee sasa Kama Mungu si hirizi kwa nini mapadre na maaskofu katoliki husisitiza watu kumuomba Mungu wakati yeye si hirizi? au kinga au msaada unaoonekana tele wakati wa Mateso yawe ya Corona au vinginevyo?...
Mwombe Mungu usifanye kazi uone itakuwaje.

MUNGU atabariki kazi ya mikono yako....ndio maana tunasema mtembea bure so sawa na mkaa bure ...huko kwenye kutembea kwako MUNGU hukubarikibi
 
Muumini wenu mwenye cheo cha juu kabisa kwa kaisali. Anaingilia hata mambo ya Kiroho.

Pamoja na watu kadhaa kwenye utawala wake kutikiswa na changamoto ya upumuaji bado anahamasisha watu wasivae barakoa.

Hoja yake isiyoeleweka eti mbona huko ulaya wanakovaa barakoa wanakufa sana. Ambacho haelewi ni kwamba yawezekana wasingevaa hizo barakoa wangekua hawapo.

Ushauri wangu kwenu ma askofu , muumini mkaidi adhabu yake ni kupewa karipio. Adhabu hii itolewe Mara moja kwa huyu muumini anaye hamasisha watu wasijilinde na kovid 19 ugonjwa ulopoteza ndugu na jamaa zetu.
 
Wapi huyo muumini alipohamasisha watu wasijikinge? Hebu tuletee ushahidi hapa wa hayo mahamasisho
 
Watakaripia wangapi? Inawezekana kuna majimbo yako kimya kuhusu hizo nyaraka za TEC, ikiwa hivyo TEC wanaweza kumkaripia Askofu. Kuna makanisa hayaweki hata hayo maji ya kunawa mikono sembuse barakoa!

Japo wanasemaga ni Kanisa moja Katoliki, kwa Tanzania nadhani siyo kanisa moja! na TEC ni 'butu'
 
Asante mkuu kwa kuwakemea hawa kwa nguvu zote!! Wanakera!! Wamegeuka kuwa mawakala wa hofu!!
Naandika hii comment nikiwa pembeni ya mama yangu mzazi hospital shida ni “nimonia kali” jamani usiombe yakukute waTz tujikinge niliyoyaona na nayoendelea kuyaona yanatisha!
 
Naandika hii comment nikiwa pembeni ya mama yangu mzazi hospital shida ni “nimonia kali” jamani usiombe yakukute waTz tujikinge niliyoyaona na nayoendelea kuyaona yanatisha!
Je kuna mtu aliyesema tusijikinge? Au kuna mtu aliyepiga marufuku kujikinga?
 
Reactions: Ame
Marekani walikufa sana kutokana na uzembe na hadaa za bwana Trump bwana asiyeambilika.Kwasasa vifo na usambaaji vimepungua kwa hatua madhubuti anazofanya Biden.
Usidanganye!!! Vifo marekani vilifikia kiwango cha juu Sana kuanzia February kipindi ambacho huyu mshabiki wa LGBT alipoingia madarakani. Ingia mtandao wa worldometer coronavirus live updates kuhakiki hilo. Kipindi chake vifo kila siku vilifikia hadi 3,000!!!
 
Father Kitima awashauri Maaskofu wasitishe ibada kuanzia kwenye Jumuiya angalau kwa mwaka mmoja. Kulalamika kwenye vyombo vya habari hakusaidii.
 
Reactions: Ame
Mimi najua kuwa nina pumzi ya Mungu. Pamoja na udhaifu wangu mwingine wote wa kibinadamu, bado nina Roho wa Mungu. Ni aheri niishi hata bila hata ya kuwa mjumbe wa serikali ya mtaa kuliko kuukubali ushetani..
Mwogope Mungu!!
 
Tanzania kuna corona au hakuna?
 
Ina maana waliokufa wote hawakuwajibika?
 
Umepotoka ndugu!
Unamkufuru Mungu, wala huna shukrani. Unaukataa hadharani uponyaji wa Mungu dhidi ya korona kwa Taifa letu. Kwa kufanya hivyo unaiita laana ya corona katika maisha yako nanyumba yako mwenyewe!! Usije kutafuta mchawi utakapoona corona inakutafuna.
Kuacha kufanya vipimo na kutoa takwimu sia uponyaji. Btw ugonjwa unaoitwa changamoto ya upumuaji ni ugonjwa gani huo? Kwa vile ugonjwa huo uko Tz pekee, tumeshataarifu WHO ili kuwe na mkakati wa kidunia wa kuudhibiti?
 
Mungu akubariki. Amina.
 

Watanzania ni wakati sasa tuwe wasikilizaji wazuri wa taarifa maelekezo yanayotolewa na viongozi wetu wa Serikali
Tunaambiwa tujikinge basi tufanye hivyo lakini tunakumbushwa Mungu anasikia hivyo tuwe na Imani nae kwani yeye ndiye muumba wetu
 
Mwendo wa kukata motooo unaendelea duh
MPAKA KWENYE BARAZA UWIII
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…