Kanisa Katoliki lapoteza Mapadri 25 na Watawa 60 kwa tatizo la upumuaji ndani ya miezi miwili

Kanisa Katoliki lapoteza Mapadri 25 na Watawa 60 kwa tatizo la upumuaji ndani ya miezi miwili

Aiseee sasa Kama Mungu si hirizi kwa nini mapadre na maaskofu katoliki husisitiza watu kumuomba Mungu wakati yeye si hirizi? au kinga au msaada unaoonekana tele wakati wa Mateso yawe ya Corona au vinginevyo?...
Mwombe Mungu usifanye kazi uone itakuwaje.

MUNGU atabariki kazi ya mikono yako....ndio maana tunasema mtembea bure so sawa na mkaa bure ...huko kwenye kutembea kwako MUNGU hukubarikibi
 
Muumini wenu mwenye cheo cha juu kabisa kwa kaisali. Anaingilia hata mambo ya Kiroho.

Pamoja na watu kadhaa kwenye utawala wake kutikiswa na changamoto ya upumuaji bado anahamasisha watu wasivae barakoa.

Hoja yake isiyoeleweka eti mbona huko ulaya wanakovaa barakoa wanakufa sana. Ambacho haelewi ni kwamba yawezekana wasingevaa hizo barakoa wangekua hawapo.

Ushauri wangu kwenu ma askofu , muumini mkaidi adhabu yake ni kupewa karipio. Adhabu hii itolewe Mara moja kwa huyu muumini anaye hamasisha watu wasijilinde na kovid 19 ugonjwa ulopoteza ndugu na jamaa zetu.
 
Wapi huyo muumini alipohamasisha watu wasijikinge? Hebu tuletee ushahidi hapa wa hayo mahamasisho
 
Watakaripia wangapi? Inawezekana kuna majimbo yako kimya kuhusu hizo nyaraka za TEC, ikiwa hivyo TEC wanaweza kumkaripia Askofu. Kuna makanisa hayaweki hata hayo maji ya kunawa mikono sembuse barakoa!

Japo wanasemaga ni Kanisa moja Katoliki, kwa Tanzania nadhani siyo kanisa moja! na TEC ni 'butu'
 
Roma kwenyewe walikufa mapadre wangapi? Why do they make a deal inapokuja hapa Tanzania?

Blame game a satanic character...Kanisa linatakiwa kuleta tumaini, upendo na mshikamano siyo kwa kumshambulia mkuu wa nchi hadharani kama hivi? Huyo ni nembo ya taifa letu ni amiri jeshi mkuu...You have to act responsibly!
Asante mkuu kwa kuwakemea hawa kwa nguvu zote!! Wanakera!! Wamegeuka kuwa mawakala wa hofu!!
Naandika hii comment nikiwa pembeni ya mama yangu mzazi hospital shida ni “nimonia kali” jamani usiombe yakukute waTz tujikinge niliyoyaona na nayoendelea kuyaona yanatisha!
 
Naandika hii comment nikiwa pembeni ya mama yangu mzazi hospital shida ni “nimonia kali” jamani usiombe yakukute waTz tujikinge niliyoyaona na nayoendelea kuyaona yanatisha!
Je kuna mtu aliyesema tusijikinge? Au kuna mtu aliyepiga marufuku kujikinga?
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Marekani walikufa sana kutokana na uzembe na hadaa za bwana Trump bwana asiyeambilika.Kwasasa vifo na usambaaji vimepungua kwa hatua madhubuti anazofanya Biden.
Usidanganye!!! Vifo marekani vilifikia kiwango cha juu Sana kuanzia February kipindi ambacho huyu mshabiki wa LGBT alipoingia madarakani. Ingia mtandao wa worldometer coronavirus live updates kuhakiki hilo. Kipindi chake vifo kila siku vilifikia hadi 3,000!!!
 
Father Kitima awashauri Maaskofu wasitishe ibada kuanzia kwenye Jumuiya angalau kwa mwaka mmoja. Kulalamika kwenye vyombo vya habari hakusaidii.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Mimi najua kuwa nina pumzi ya Mungu. Pamoja na udhaifu wangu mwingine wote wa kibinadamu, bado nina Roho wa Mungu. Ni aheri niishi hata bila hata ya kuwa mjumbe wa serikali ya mtaa kuliko kuukubali ushetani..
Mwogope Mungu!!
 
Hayo ni ya kwako. Hakuna hata siku moja viongozi wa serikali wamesema tusifanye chochote! Hivi una macho au hauna? Una masikio au hauna? Tulichokifanya ni kumtanguliza Mungu mbele ndipo mambo ya tahadhari kama kunawa mikono na kuvaa barakoa yafuate? Acha uongo!...
Tanzania kuna corona au hakuna?
 
Katibu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, Padri Charles Kitima amesema kuwa ndani ya miezi miwili iliyopita zaidi ya mapadri 25, masista na manesi 60 na wenyeviti wawili wa Baraza la Walei wamefariki dunia kwa sababu mbalimbali ikiwemo changamoto ya upumuaji..​
Ina maana waliokufa wote hawakuwajibika?
 
Umepotoka ndugu!
Unamkufuru Mungu, wala huna shukrani. Unaukataa hadharani uponyaji wa Mungu dhidi ya korona kwa Taifa letu. Kwa kufanya hivyo unaiita laana ya corona katika maisha yako nanyumba yako mwenyewe!! Usije kutafuta mchawi utakapoona corona inakutafuna.
Kuacha kufanya vipimo na kutoa takwimu sia uponyaji. Btw ugonjwa unaoitwa changamoto ya upumuaji ni ugonjwa gani huo? Kwa vile ugonjwa huo uko Tz pekee, tumeshataarifu WHO ili kuwe na mkakati wa kidunia wa kuudhibiti?
 
Mimi najua kuwa nina pumzi ya Mungu. Pamoja na udhaifu wangu mwingine wote wa kibinadamu, bado nina Roho wa Mungu. Ni aheri niishi hata bila hata ya kuwa mjumbe wa serikali ya mtaa kuliko kuukubali ushetani.

Jiwe yeye, ana ujasiri mkubwa. Ana uwezo wa kuishi na shetani moyoni mwake, na akatenda matakwa ya shetani kama walivyofanya kwenye uchaguzi, akadhulumu kwa kuiba kura kama alivyofanya, na mengine maovu mengi kama ya kuua, kuteka watu, kuwapoteza watu, akaufurahia uovu huo hata bila ya kuumizwa na dhamira yake kwa sababu dhamira yake ilikwishakufa.
Mungu akubariki. Amina.
 


Katibu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, Padri Charles Kitima amesema kuwa ndani ya miezi miwili iliyopita zaidi ya mapadri 25, masista na manesi 60 na wenyeviti wawili wa Baraza la Walei wamefariki dunia kwa sababu mbalimbali ikiwemo changamoto ya upumuaji.

Ameongeza kuwa vifo vinaendelea na kuwataka Watanzania kuendelea kuchukua tahadhari na kuacha mzaha katika katika suala zima la Corona.

Huyu Mungu si hirizi, anataka kila binadamu awajibike na atumie uwezo wake kufikiri. Corona ipo, unaambiwa chukua tahadhari unasema mimi nasali. Mungu wetu anataka watu wawajibike, si kusema tu, tunasali - Ameongeza Padri Charles Kitima


Watanzania ni wakati sasa tuwe wasikilizaji wazuri wa taarifa maelekezo yanayotolewa na viongozi wetu wa Serikali
Tunaambiwa tujikinge basi tufanye hivyo lakini tunakumbushwa Mungu anasikia hivyo tuwe na Imani nae kwani yeye ndiye muumba wetu
 
Mwendo wa kukata motooo unaendelea duh
MPAKA KWENYE BARAZA UWIII
 
Back
Top Bottom