Kanisa Katoliki lapoteza Mapadri 25 na Watawa 60 kwa tatizo la upumuaji ndani ya miezi miwili

Kanisa Katoliki lapoteza Mapadri 25 na Watawa 60 kwa tatizo la upumuaji ndani ya miezi miwili

Inasikitisha sana kwa kanisa kutoa kauli kama hii...Hii dini hapa imesimama kama taasisi na wala siyo kuongozi wa kiroho...Kanisa katoliki haliamini katika abortion na wala family planning je hiyo siyo science? Au science inakuwa valid pale ambapo interests zako zimelalia?...
Na kila siku wanaimba Yesu alikufa kwa ajili ya dhambi zetu leo wamemgeuka. Huyu kitime ma boss wake nikishawashtukia kitambo wana agenda ya upinzani tena iliyo sugu. Boss wake yeye hata sina mashaka nae maana ukabila ni jadi ya atokako.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Acha kutisha watu wanaotimiza wajibu wao kwa nchi na kwa Mungu.

Nyinyii ndio mnaostahili kuwajibika kwa maisha yanayopotea ovyo kwa upotoshaji wenu kupitia imani zenu za kishirikina.
Huo anaofanya Kitime siyo wajibu wake ni wajibu wa viongozi wa Nchi. Yeye atangaze kanisani lock down watu wasiende makanisani tuone ataishije bila sadaka.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Mapadre25 watawa 60 so tuliambiwa corona Inauwa Wanaume zaidi au hii ya South Africa imegeuza kibao
Poleni sana wale wote mliopoteza Ndugu na jamaa na marafiki
Kwa uwiano wa mapadre vs masister ndani kanisa katoliki.vifo vya mapadre ni vingi mno kwa uwiano.mapadre ni wachache ktk Kila Jimbo kuliko masister
 
Mapadre25 watawa 60 so tuliambiwa corona Inauwa Wanaume zaidi au hii ya South Africa imegeuza kibao
Poleni sana wale wote mliopoteza Ndugu na jamaa na marafiki
Kwa nini hatujiulizi - iweje mataifa yaliyo kubali baadhi ya raia wake kufanyiwa majaribio ya chanjo za Oxford, ndio mataifa hayo hayo yaliyo kumbwa na aina mpya hatarishi ya ugonjwa wa COVID-21 - hii inaleta picha gani?

Jana nilishangaa sana nilipo wasikia wataalamu wa immunology wa huko Ulaya na Merikani wakisema kwamba variant mpya ina uwezo mkubwa wa kukwepa/by pass kinga ya mwili - hivi inaingia akilini kwamba virusi hivi vime mutate tu ili vikwepe kinga ya mwili au kuna wataalamu wenye ajenda zao za siri ndio wame chezea virus hivi ili viwe more virulent - wanafanya hivo baada ya kuona COVID-19 haiwui Waafrika wengi kama mkewe Bill Gates alivyo tabiria Bara la Afrika kwamba ugonjwa huu ungetuuwa kama nzinge!!

Tukumbuke kwamba mfuko wa Bill Gates na mkewe ndio wanafadhili Big Pharma Companies zinazo zalisha chanjo, wana sayansi wa makampuni hayo wana uwezo mkubwa wa kutekeleza kile mfadhili wao anacho wa-instruct wafanye - moja wapo ikiwa ni kutujia na variant mpya ya virus kama plan "B" wakiwa na lengo la kuzifanya Nchi/Mataifa yapate taharuki mwisho wa siku Serikali zao zilazimike kununua chanjo za Bill Gates fasta maana hazitakuwa na jinsi/lakufanya tuk Afrika zitaingizwa batch ya chanjo zenye malengo ya ku- depopulate gracefully Bara la Afrika kwa kupitia chanjo zao kuingilia mfumo wa uzazi wa akina mama,pia chanjo hizo zitaongezewa/rutubishwa na vichocheo vya kufanya kinga ya mwili ku-over react na allergies za kawaida tu mfano mafua nawbaadhi ya vyakula watu wataanza kudhulika na wengine kufariki kutokana na vifo vyenye utata na haitakuwa rahisi kukumbuka kwamba madhala hayo yanatokana na chanjo tulizo chanjwa miezi/miaka iliyo pita .

Sasa ukweli huu niliyo utaja hapo juu ndio unamfanya Rais wetu JPM akatae kuingiza nchini chanjo zenye utata mkubwa, hivi sasa kuna baadhi ya Watanzania wana mbeza beza kutokana na aidha na uelewa wao mdogo kuhusu kinga ya mwili inavyo fanya kazi inapo pata boost kupitia chanjo,na bila shaka anajua utofauti wa chanjo zinazo zalishwa kupitia conventional method ya kutumia attenuated virus,pia anajuwa vile vile mbinu za hivi karibuni ambazo zinatumia njia ya kijinetiki (mRNA) zinazo tumika na predominantly nchi za magharibi kuzalisha chanjo za corona, ukweli ni kwamba no knows for certain njia hii ya kijinetiki inaweza kusababishi madhala gani ya short na long term kwa wale watakao kubali kuchanjwa kwa chanjo zinazotokana na mRNA - sasa JPM akikataa Watanzania kugeuzwa ma Guinea Ping mnamuona mbaya - JPM hajakataza watu wanao taka kwenda nchi nyingine kudungwa chanjo - nendeni Kenya, Afrika Kusini, Ghana na Ivory Coast mkisha chanjwa tupatie mrejesho baada ya miezi sita/mwaka kupita - mtakuja kukumbuka busara za JPM alipo toa tahadhali kubwa kwa Watanzania kuhusu chanjo hizi zenye utata.

FYI wanajeshi wengi wa huko Merikani wamekataa kuchanjwa chanjo ambazo hazijawahi kufanyiwa tafiti na majaribio ya kutosha, Dunia ikajiridhisha kwamba chanjo hizo ni salama na hazikukimbizwa kuingizwa sokoni na Big Pharma Companies kwa lengo la kupiga hela ndefu wakishirikiana na WHO na Bill Gates na mkewe. Tukubali kwamba JPM ana kalama ya kuona mbali. Hayo ni maoni yangu.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Peleka hukoo hayo mambo yako ya ushirikina.

Mnamsingizia Mungu na imani kwa misimamo ya ajabu ajabu ambayo haina mantiki bali kujitwalia utukufu nyimgi wenyewe huku watanzania wakizidi kupukutika..
Hata watu wote wakikataa, ukweli utabaki kuwa Tanzania tuliponywa na Mungu dhidi ya Corona!! Mungu apishe mbali!! Tanzania tulionja tu harufu ya corona, hata sasa tunasikia harufu tu ya corona.

Mungu apishe mbali!! Kama Mungu angeruhusu sasa watanzania tukinywee kikombe cha corona kama jinsi walivyokinywea mataifa mengine ya ulaya, Marekani na Marekani ya kusini, hapo ndipo watu wangetambua kuwa kumbe Mungu alikuwa ametuhifadhi Sana.

Ni sawa na mtoto wa tajiri aliyepewa chai ya maziwa lakini bahati mbaya kitafunwa kikawa hakipo! Huyo mtoto akalalamika Sana kuwa atashinda njaa wakati ana uhakika wa chakula cha mchana na Cha jioni!! Siku baba yake akifilisika akawa anashindia chai ya rangi hadi saa mbili usiku ndipo ale ugali na maharage chukuchuku, ndipo atatambua kuwa kumbe hata siku alipopata chai ya maziwa bila kitafunwa walikuwa na maisha mazuri mno.

Watanzania nawasihi tusikufuru!! Maana sisi si bora Sana kuliko mataifa ambako wanakufa kwa mamia na maelfu kwa siku moja! Ni rehema za Mungu tu na ambazo tunazifumbia macho tusizione! Mungu naomba utusamehe.

Mungu naomba uwasamehe wote wanaoukataa uponyaji wako uliotupatia watanzania kwa kuwa hawajui walitendalo.

Inashangaza sana!! Corona imeua mamilioni ya watu duniani, aliyebaki mzima bado hatambui kuwa ni Mungu amemponya.

Mwanadamu anaweza kuwa kiumbe wa ajabu sana!! Japo ana pumzi ya uhai lakini hajui atoaye uhai huo.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Shetani ni wa ajabu sana. Ni mwenye hila. Ana uwezo wa kuleta tatizo na kisha akajidai analeta suluhisho. Wengi wasio na macho ya rohoni wamenaswa na hila zake hizi.


YESU NI BWANA NA MWOKOZI
 
Tumsifu yesu kristu, umeona muongozo mpya wa ibada au haujauona?
Si wanataka tuige hatua walizochukua wazungu na wamarekani? Wawatangazie waumini wao kujifanyia lockdown na makanisa yafungwe, maana huko ulaya yamefungwa!! Tuone kama watalifanya hilo! thubutu!! bila sadaka wakale polisi!! hapo watajitoa kabisa ufahamu!!
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Hii taarifa kuna media wanaiogopa. Wengine wata edit edit tu [emoji41]

Millard kaweka vipande tu! Hata Instagram hajapost itakuwa bado anasikilizia.Hatuwezi kuisaidia jamii namna hii. Inafikia viongozi wa juu kiroho wanatoa maagizo bado tunayaogopa tunataka ashuke Mungu?
Hao ni viongozi wa dini si viongozi wa kiroho! sikiliza tena hiyo clip! Hawana ubavu wa kuthubutu kujiita viongozi wa kiroho!! Hawamwamini kabisa Mungu wala nguvu zake! Hawa ndio biblia ilisema Wana mfano wa utakuwa lakini wakizikana nguvu zake!!! Hawana lolote hao.

Ukweli ni kuwa Mungu alituponya na corona mwaka jana na atatuponya na corona mwaka huu pia!! Tuliishinda corona mwaka jana kwa kumwomba na kumtanguliza Mungu, hali kadhalika anatuponya mwaka huu maana tumemwomba na kumtanguliza Mungu.

Shetani na vibaraka wake wanajitahidi kwa nguvu zote kuupinga na kuufumbia macho uponyaji huu mkuu wa Mungu kuwa Taifa letu lakini wameshindwa vibaya.

Nathamini uhai wa kila mmoja, lakini ni nini vifo vya hawa mapadri wachache na masista ukilinganisha na makumi elfu ya mapadri na masista waliokufa na corona duniani kote hasa Italia? Hata sasa Bwana ametusaidia!
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Hivi hawa maaskofu kama wako serious kwanini wasifunge kabisa makanisa? Kwani kuna mtu atawazuia?
Nakuunga mkono! Si wanataka tuige wanavyofanya Ulaya? Ulaya makanisa yamefungwa!! Na wao wayafunge kama wako serious!! Namshauri Rais Magufuli awaagize kufunga makanisa yao ili kuepusha mapadri na masista kufa kwao korona, tuone kama hawataomba poo!!!!!
 
Shule ulienda kufanya ko nini ?! Kama Padri amezungumzia kanisa lake . Siyo takwimu za nchi kama Tz . Hivi ukiwa mfuasi wa u dictator na u communist lazima uwe hamnazo ?!

Hakuna sheria inayomzuia kuzungumzia watu walio chini yake. By the way u communist & u dictator haujawahi kuitoa nchi yeyoe mrisi [emoji107]. mbingunikwetu
Si wafunge hayo makanisa yao ili kuwanusuru mapadri na masista na corona? Si ulaya walifunga!! Kama wanataka kuiga wazungu kwa kutoa takwimu, si waive na kufunga makanisa yao? Wana ubavu wa kufanya hivyo? Hapo hakuna kitu zaidi ya unafiki!!
 
Acha kudanganya watu na upotoshaji. Mbona mnafanya propaganda za kishamba namna hiyo?

Mnataka kuachive nini? Wewe hujatoa takwimu halafu unajilinganisha na aliyetoa! Hakunaga kitu ya namna hiyo. Mnamdanganya nani? THE OBVIOUS CAN NOT BE PROVED!
Takwimu hazisaidii, ndio maana haijawasaidia wamarekani. Badala yake takwimu huleta hofu na taharuki tu!!
 
Si wafunge hayo makanisa yao ili kuwanusuru mapadri na masista na corona? Si ulaya walifunga!! Kama wanataka kuiga wazungu kwa kutoa takwimu, si waive na kufunga makanisa yao? Wana ubavu wa kufanya hivyo? Hapo hakuna kitu zaidi ya unafiki!!
Kabisa mkuu! Tunaunga mkono wito wao wa kuchukua thadhali, lakini hii ya kujaribu kutuonesha kama kuna mtu hawajibiki wakati wao wana mamlaka ya kufunga hayo makanisa na kunusuru mapadri wao inashangaza sana.

Shida ni sadaka watatoa wapi?

Yani ningekuwa mimi Magu, ningepiga ban misa kwa miezi 3 tu uone kama hawajaenda kupiga magoti.
 
Kanisa limepoteza Imani hivyo wanavuna walichopanda.

Tunasahau hata wimbi la Kwanza hatukulishinda kwa nguvu zetu.

Petro alianza kuzama majini baada ya kupoteza imani.
Corona haikuwahi kwisha msidanganywe na dereva wenu kipofu wakati yeye kupata chanjo ya mchina kimyakimya
 
Watu wanahisi kwasababu bible haijajikita sna kweny historia ya mwili bali imani basi wanahisi zamani walikuwa maroboti ya Mungu hawaugui wala hawana dawa. Mungu kaweka dawa kwenye miti why is that? Kwann watu wake wanaenda hospital na wanapona? Mungu aliposema kuwa ukiwa na imani ndogo kama chembe ya haladari(kama sikosei neno) utaamisha mlima doesn't mean umuombe ahamishe mlima kweli bila sababu kwasababu atakuona mpumbavu uliopofuka. Sijui kama tunamkosea kwahili tunaomba tusamehewe atujaze imani na amani kati yetu.
... wanashanagza sana. Mwenye Biblia yake anaema; "wenye afya hawahitaji tabibu, bali wenye kuugua ndio wanaomhitaji.” Mt. 9:12. Huduma za hospitali/matibabu zilikuwepo tangu kale na hata Bwana Yesu mwenyewe alizitambua. Halafu wanatokea wendawazimu wachache kupuuza matibabu ya kisayansi kwa gonjwa hili sijui wana ajenda gani na maisha yetu.
 
Bora anatumika kusema ukweli kwa wanaogopa kuusema , kuliko mtu anayetumika kusema hali shwari wakati sio shwari
 
Ni upumbavu wa hali ya juu kumtaka Mungu akulinde huku wewe hufanyi chochote...
Hayo ni ya kwako. Hakuna hata siku moja viongozi wa serikali wamesema tusifanye chochote! Hivi una macho au hauna? Una masikio au hauna? Tulichokifanya ni kumtanguliza Mungu mbele ndipo mambo ya tahadhari kama kunawa mikono na kuvaa barakoa yafuate? Acha uongo!!

Si kwamba Tanzania hatujafanya chochote, Ila tukimtanguliza Mungu KABLA ya kufanya chochote, na hiyo imetulipa, ndio maana bado upo hai!! Laiti ungekuwa unaishi Marekani waliotanguliza "kufanya chochote" na Mungu kumwacha nyuma labda ungekuwa umeshakufa na corona!! Moe Mungu utukufu!!
 
Ametueleza kuwa corona ipo na inaua. Sijajua sijui mtanzania gani hajui Kama corona ipo. Hata huku shamba tunajua...
Hata mimi nimesikitika sana alipofikia kusema MUNGU siyo hilizi!! Nimeumia sana kusikia haya maneno yakitoka kinywani mwa padre msomi tena doctor wa fALSAFA NA THEOLOJIA.

MUNGU ULIYE HAI UWASAMEHE.Nimeona niandika haya japo moyo wangu utulie, CORONA inabeba ufahamu wa watu wasio wagonjwa je wagonjwa wana hali gani sasa duuuu
 
Hao ni viongozi wa dini si viongozi wa kiroho! sikiliza tena hiyo clip! Hawana ubavu wa kuthubutu kujiita viongozi wa kiroho!! Hawamwamini kabisa Mungu wala nguvu zake! Hawa ndio biblia ulisema Wana mfano wa utakuwa lakini wakizikana nguvu zake!!! Hawana lolote hao...
Baba padre akirudia kuisikiliza hiyo clip atatamani kuiondoa kwenye mitandao, lakini haina jinsi Historia ameaindika itabaki
 
Back
Top Bottom