ngara23
JF-Expert Member
- Aug 31, 2019
- 16,871
- 39,881
Binafsi nimesomea Katoke Seminary kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita. Nikiwa mtu niliyeishi ndani ya mfumo wa Kanisa Katoliki, ninaweza kusema kwa ukweli kuwa kanisa hili limejipanga vizuri sana katika idara na utendaji wake. Hata hivyo, bado kuna changamoto kubwa katika namna linavyowatendea Mapadre na Watawa wake.
Kumekuwa na taarifa na tuhuma kwamba baadhi ya Mapadre wanapitia msongo mkubwa wa maisha unaowasukuma kuchukua hatua kali kama kujiteka, kujidhuru au hata kujiua. Ingawa binafsi sina imani kubwa na vyombo vya dola kama jeshi la polisi, kwa kuzingatia falsafa na mifumo ya kanisa, ninaona kuna chembe ya ukweli katika matukio hayo.
Kibinadamu, mtu ameumbwa na asili ya kutaka kumiliki—iwe ni fedha, nyumba, mali au familia. Ni vigumu sana kwa binadamu kukana kabisa asili hii. Hata mnyama kama mbwa anatambua sahani yake na hawezi kuruhusu mwingine kula chakula chake; sembuse binadamu. Kwa hiyo, ni changamoto kubwa kumlazimisha Padre kuishi maisha yasiyo na umiliki wowote—bila fedha, mali, wala mwenza.
Shinikizo la maisha hayo linaweza kuwapelekea baadhi ya Mapadre na Watawa kukopa kwa siri, kushindwa kulipa, na hatimaye kupata msongo wa mawazo, shinikizo la damu, au kufikia hatua mbaya ya kujidhuru.
Kimsingi, mwanaume au mwanamke aliyekomaa kisaikolojia na kimwili hawezi kuishi bila mwenza au bila kushiriki tendo la ndoa—hilo ni hitaji la kiasili, si udhaifu. Kwa hiyo, naamini iwapo Mapadre na Watawa wangepewa uhuru wa kumiliki mali binafsi na kuwa na wenza, wangeishi kwa amani zaidi, na utii wao kwa kanisa ungeongezeka mar