Kanisa Katoliki libadili mtazamo kuhusu jinsi linavyowatendea Mapadre na Watawa

Kanisa Katoliki libadili mtazamo kuhusu jinsi linavyowatendea Mapadre na Watawa

Attachments

  • Screenshot_20251018-132751_WhatsApp.jpg
    Screenshot_20251018-132751_WhatsApp.jpg
    247.9 KB · Views: 18
Binafsi nimesomea Katoke Seminary kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita. Nikiwa mtu niliyeishi ndani ya mfumo wa Kanisa Katoliki, ninaweza kusema kwa ukweli kuwa kanisa hili limejipanga vizuri sana katika idara na utendaji wake. Hata hivyo, bado kuna changamoto kubwa katika namna linavyowatendea Mapadre na Watawa wake.

Kumekuwa na taarifa na tuhuma kwamba baadhi ya Mapadre wanapitia msongo mkubwa wa maisha unaowasukuma kuchukua hatua kali kama kujiteka, kujidhuru au hata kujiua. Ingawa binafsi sina imani kubwa na vyombo vya dola kama jeshi la polisi, kwa kuzingatia falsafa na mifumo ya kanisa, ninaona kuna chembe ya ukweli katika matukio hayo.

Kibinadamu, mtu ameumbwa na asili ya kutaka kumiliki—iwe ni fedha, nyumba, mali au familia. Ni vigumu sana kwa binadamu kukana kabisa asili hii. Hata mnyama kama mbwa anatambua sahani yake na hawezi kuruhusu mwingine kula chakula chake; sembuse binadamu. Kwa hiyo, ni changamoto kubwa kumlazimisha Padre kuishi maisha yasiyo na umiliki wowote—bila fedha, mali, wala mwenza.

Shinikizo la maisha hayo linaweza kuwapelekea baadhi ya Mapadre na Watawa kukopa kwa siri, kushindwa kulipa, na hatimaye kupata msongo wa mawazo, shinikizo la damu, au kufikia hatua mbaya ya kujidhuru.

Kimsingi, mwanaume au mwanamke aliyekomaa kisaikolojia na kimwili hawezi kuishi bila mwenza au bila kushiriki tendo la ndoa—hilo ni hitaji la kiasili, si udhaifu. Kwa hiyo, naamini iwapo Mapadre na Watawa wangepewa uhuru wa kumiliki mali binafsi na kuwa na wenza, wangeishi kwa amani zaidi, na utii wao kwa kanisa ungeongezeka marView attachment 3490237
Kuingia upadre ni hiari na si amri. Kabla ya kuingia wanatambua yote hayo na wanakubali.
Lakini pia hulazimishwi kuwa padri maisha yako yote ukiona upwiru umekuzidi sepa tu kama Dr. Slaa anakula zake maisha bila bugudha.
 
Kuingia upadre ni hiari na si amri. Kabla ya kuingia wanatambua yote hayo na wanakubali.
Lakini pia hulazimishwi kuwa padri maisha yako yote ukiona upwiru umekuzidi sepa tu kama Dr. Slaa anakula zake maisha bila bugudha.
Upwiru hauvumiliki Mkuu
Kusepa sio suluhu
Kila mwanaume aliyekamilika kibaolojia anahitaji papuchi angalau mara 3 Kwa wiki
 
Upwiru hauvumiliki Mkuu
Kusepa sio suluhu
Kila mwanaume aliyekamilika kibaolojia anahitaji papuchi angalau mara 3 Kwa wiki
Waache kuwa mapadri maana hawajalazimishwa ni kiherehere chao wenyewe
 
Back
Top Bottom