Kanisa Katoliki libadili mtazamo kuhusu jinsi linavyowatendea Mapadre na Watawa

Binafsi nimesomea Katoke Seminary kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita. Nikiwa mtu niliyeishi ndani ya mfumo wa Kanisa Katoliki, ninaweza kusema kwa ukweli kuwa kanisa hili limejipanga vizuri sana katika idara na utendaji wake. Hata hivyo, bado kuna changamoto kubwa katika namna linavyowatendea Mapadre na Watawa wake.

Kumekuwa na taarifa na tuhuma kwamba baadhi ya Mapadre wanapitia msongo mkubwa wa maisha unaowasukuma kuchukua hatua kali kama kujiteka, kujidhuru au hata kujiua. Ingawa binafsi sina imani kubwa na vyombo vya dola kama jeshi la polisi, kwa kuzingatia falsafa na mifumo ya kanisa, ninaona kuna chembe ya ukweli katika matukio hayo.

Kibinadamu, mtu ameumbwa na asili ya kutaka kumiliki—iwe ni fedha, nyumba, mali au familia. Ni vigumu sana kwa binadamu kukana kabisa asili hii. Hata mnyama kama mbwa anatambua sahani yake na hawezi kuruhusu mwingine kula chakula chake; sembuse binadamu. Kwa hiyo, ni changamoto kubwa kumlazimisha Padre kuishi maisha yasiyo na umiliki wowote—bila fedha, mali, wala mwenza.

Shinikizo la maisha hayo linaweza kuwapelekea baadhi ya Mapadre na Watawa kukopa kwa siri, kushindwa kulipa, na hatimaye kupata msongo wa mawazo, shinikizo la damu, au kufikia hatua mbaya ya kujidhuru.

Kimsingi, mwanaume au mwanamke aliyekomaa kisaikolojia na kimwili hawezi kuishi bila mwenza au bila kushiriki tendo la ndoa—hilo ni hitaji la kiasili, si udhaifu. Kwa hiyo, naamini iwapo Mapadre na Watawa wangepewa uhuru wa kumiliki mali binafsi na kuwa na wenza, wangeishi kwa amani zaidi, na utii wao kwa kanisa ungeongezeka marView attachment 3490237
Acha upuuzi! Kwani useja kwa mapadre umeanza leo! Kwani kuna mtu anamg'ang'ania akawe Padre?
 
Sio Kila tukio jeshi linakimbilia kusema mtu kajiteka?? Refer issues ya yule padri mwingine SERIKALI kupitia jeshi ikasema Kuna biashara ya online alipo gundua katapelika..
Refer issue ya ABDUL NONDO,
Hilo siwezi kuuthibitisha ila kusema ukweli kanisa katoliki Lina falsafa ambazo zinapinga nature na hii Kwa miaka hii itawasumbua sana na watapata matukio mengi.
Ni Bora Vatican iketi warekebishe baadhi ya vifungu
 
Acha upuuzi! Kwani useja kwa mapadre umeanza leo! Kwani kuna mtu anamg'ang'ania akawe Padre?
Upadre haujaanza Leo ila kumbuka falsafa ya kanisa katoliki unapinga nature, Kwa Karne hii watapata matukio mengi
Kumbuka huyu ni Padre wa pili anakutwa na tukio hili.
Kuna matukio ya ulawiti
Kuna tukio la ushirikina huko Bukoba Padre alifadhili genge la kumuua mtoto mwenye zeruzeru
 
Ni kweli jeshi lina makando kando, lkn katika hili nadhan wanasema ukweli, tatizo tu kuweka public hizi taarifa wamemkosea sana padri.
Ni kama wamezidi kumzalilisha jambo ambalo litazidi kumletea depression.
 
Namjua paroko mmoja huko kusini anamke na mtoto, huyu mtoto anamuita baba yake "Babu" ila kwa hakika ni baba yake mzazi. Na Bado wanaishi pamoja mpaka Leo.
Mimi nina cousin yangu amezaa na padri watoto zaidi ya watatu. Na watoto walipokuwa wadogo walikuwa wanamuita babu, ila saivi wanamuita baba tu.
 
Binafsi nimesomea Katoke Seminary kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita. Nikiwa mtu niliyeishi ndani ya mfumo wa Kanisa Katoliki, ninaweza kusema kwa ukweli kuwa kanisa hili limejipanga vizuri sana katika idara na utendaji wake. Hata hivyo, bado kuna changamoto kubwa katika namna linavyowatendea Mapadre na Watawa wake.

Kumekuwa na taarifa na tuhuma kwamba baadhi ya Mapadre wanapitia msongo mkubwa wa maisha unaowasukuma kuchukua hatua kali kama kujiteka, kujidhuru au hata kujiua. Ingawa binafsi sina imani kubwa na vyombo vya dola kama jeshi la polisi, kwa kuzingatia falsafa na mifumo ya kanisa, ninaona kuna chembe ya ukweli katika matukio hayo.

Kibinadamu, mtu ameumbwa na asili ya kutaka kumiliki—iwe ni fedha, nyumba, mali au familia. Ni vigumu sana kwa binadamu kukana kabisa asili hii. Hata mnyama kama mbwa anatambua sahani yake na hawezi kuruhusu mwingine kula chakula chake; sembuse binadamu. Kwa hiyo, ni changamoto kubwa kumlazimisha Padre kuishi maisha yasiyo na umiliki wowote—bila fedha, mali, wala mwenza.

Shinikizo la maisha hayo linaweza kuwapelekea baadhi ya Mapadre na Watawa kukopa kwa siri, kushindwa kulipa, na hatimaye kupata msongo wa mawazo, shinikizo la damu, au kufikia hatua mbaya ya kujidhuru.

Kimsingi, mwanaume au mwanamke aliyekomaa kisaikolojia na kimwili hawezi kuishi bila mwenza au bila kushiriki tendo la ndoa—hilo ni hitaji la kiasili, si udhaifu. Kwa hiyo, naamini iwapo Mapadre na Watawa wangepewa uhuru wa kumiliki mali binafsi na kuwa na wenza, wangeishi kwa amani zaidi, na utii wao kwa kanisa ungeongezeka marView attachment 3490237
Mtazamo wako unahukumu pasipo kuangazia upande wa pili.. tusubiri tamko la padri na askofu wake.

Binafsi padri Nikata namfahamu fika sidhani na siamini yaliyotamkwa na rpc
 
Hata mimi nimepitia kwenye shule zao, miaka mingi iliyiopita. Siku zote nimekuwa muwazi kuhusu maisha ya Maaskofu, Mapadre, na Watawa wa kiume na wa kike wa Kanisa Katoliki!

Waachane na maisha ya useja! Kwa sababu ni wachache tu kati yao ndiyo wanayaishi hayo maisha. Wengi wamekuwa wakifanya uzinzi kimya kimya!

Yaani kiufupi Kanisa Katoliki hata kama ni kongwe kuliko Makanisa yote duniani; bado hawazuiliwi kubadilisha aina yao ya maisha. Maaskofu na Mapadre waruhusiwe kuoa kama ilivyo kwa Makatekista! Mwisho wa mwezi walipwe posho kutokana na sadaka tunazotoa, pamoja na uwekezaji wa miradi mbalimbali.

Maisha ya kuishi useja, kutokumiliki mali au familia; kiukweli yana changamoto nyingi za kisaikolojia. Na wanaoshindwa kuyaishi hayo maisha ndiyo utawakuta wana vimada na watoto wao pembeni! Wana biashara zao binafsi, nk.

Mabadiliko kiukweli hayakwepeki.
Kwa hiyo unamaanisha kabisa hilo linahitaji Reforms?
 
Unaweza kutusababishia majanga tukihoji mambo kadhaa kuhusu kujiteka na depression za mapadri wa kanisa Katoliki.
Mfano: Kwanini huo msongo wa kufikia kujiteka ujitokeze sasa na siyo miaka mingine? Kumbuka kanisa limeanza miaka zaidi ya 2000 kufuata sheria yao ya nadhiri ya useja na kutomiliki mali binafsi.
Kesi za uzinzi wa watawa tumezisikia toka miaka hiyo. Kwanini msongo na kujiteka iwe Sasa?
 
Hilo siwezi kuuthibitisha ila kusema ukweli kanisa katoliki Lina falsafa ambazo zinapinga nature na hii Kwa miaka hii itawasumbua sana na watapata matukio mengi.
Ni Bora Vatican iketi warekebishe baadhi ya vifungu
Screenshot_20251018-124310.png
 
Mtazamo wako unahukumu pasipo kuangazia upande wa pili.. tusubiri tamko la padri na askofu wake.

Binafsi padri Nikata namfahamu fika sidhani na siamini yaliyotamkwa na rpc
Sio suala la Padre Nikita tu
Kuna Padre huko Mbeya na askofu alithibitisha alikuwa na madeni, na msongo wa Mawazo.
Kuna kesi za ulawiti nyingi.
Kuna tukio la ushirikina huko Bukoba Padre alifadhili genge la kumuua mtoto mwenye zeruzeru
 
Nimekwambia suala la kufanya ngono Kwa mtu aliyekamilika kibaolojia ni la laZima na huwezi kulipinga ni sawa na kusema watu wakae Kwa kutumia kichwa na sio makalio
Moja ndio maana nimekwambia sitaki kulizungumzia celibacy hapa na nimejikita kwenye mali nadhani nimesema hilo tangia mwanzo kabisa na kuhusu hao Mapadre kutokufanya Ngono kuna Mapadre wanajulikana na wana watoto (ila kama nilivyosema hapa najikita kwenye mali
Kumiliki Mali na kaubinafsi ndo asili ya viumbe hai sio binadamu tu, hili halitaki utake au usitake
Ndio maana nikasema hujui unachoongelea wewe kumiliki material things kwako huenda ndio ikawa alfa na omega mwingine kujitoa na nafsi yake kuona kwamba imeweza kutangaza neno (kazi ya Mungu) ndio kumiliki kwenyewe; kila mtu ana matamanio yake usiangalie vitu kwa macho ya nafsi yako au unachopenda wewe - Mwingine kuwa Father na ku-make a difference ndio anashukuru ndio maana kuina Monks kwao material things anajiona amepungua
Kutoa maoni si jambo baya, usiseme kama unaona hutaki utoke RC, nyie ndo wale tukidai katiba ya nchi mnatwambia tuhamie Burundi
Kuzaliwa umezaliwa Tanzania hii ni nchi yako kwahio huwezi kuambiwa uhame Kanisa umelikuta na Kanuni zake kama unaona hazifai mbona rahisi tu unatoka kama wewe ulivyotoka - Ukizingatia kumiliki vitu ni nani anakuchangia ? Kama ni masikini ambaye hana kitu alafu wewe unataka kumiliki huo ndio unaitwa unayonyaji na utapeli
 
Sio suala la Padre Nikita tu
Kuna Padre huko Mbeya na askofu alithibitisha alikuwa na madeni, na msongo wa Mawazo.
Kuna kesi za ulawiti nyingi.
Kuna tukio la ushirikina huko Bukoba Padre alifadhili genge la kumuua mtoto mwenye zeruzeru
Suala la kuoa au rugusa ya umiliki na uwezo binafsi wakujitawala hauepushi madeni, ulawiti au makosa mengine ya kimaadili...

Kuna mashehe wanaruhusiwa kuoa Hadi wake wanne na wanajitawala binafsi kiuchumi na mambo mengine..
hujawahi sikia wamebaka, wanna madeni, msongo wa mawazo, ulawiti na ubakaji n.k ?!
 
Moja ndio maana nimekwambia sitaki kulizungumzia celibacy hapa na nimejikita kwenye mali nadhani nimesema hilo tangia mwanzo kabisa na kuhusu hao Mapadre kutokufanya Ngono kuna Mapadre wanajulikana na wana watoto (ila kama nilivyosema hapa najikita kwenye mali

Ndio maana nikasema hujui unachoongelea wewe kumiliki material things kwako huenda ndio ikawa alfa na omega mwingine kujitoa na nafsi yake kuona kwamba imeweza kutangaza neno (kazi ya Mungu) ndio kumiliki kwenyewe; kila mtu ana matamanio yake usiangalie vitu kwa macho ya nafsi yako au unachopenda wewe - Mwingine kuwa Father na ku-make a difference ndio anashukuru ndio maana kuina Monks kwao material things anajiona amepungua

Kuzaliwa umezaliwa Tanzania hii ni nchi yako kwahio huwezi kuambiwa uhame Kanisa umelikuta na Kanuni zake kama unaona hazifai mbona rahisi tu unatoka kama wewe ulivyotoka - Ukizingatia kumiliki vitu ni nani anakuchangia ? Kama ni masikini ambaye hana kitu alafu wewe unataka kumiliki huo ndio unaitwa unayonyaji na utapeli
Naheshimu mtazamo wako Mkuu
 
Suala la kuoa au rugusa ya umiliki na uwezo binafsi wakujitawala hauepushi madeni, ulawiti au makosa mengine ya kimaadili...

Kuna mashehe wanaruhusiwa kuoa Hadi wake wanne na wanajitawala binafsi kiuchumi na mambo mengine..
hujawahi sikia wamebaka, wanna madeni, msongo wa mawazo, ulawiti na ubakaji n.k ?!
Hata kama baadhi ya viongozi wa dini wanafanya maovu wakiwa na uhuru wa ndoa au mali, hilo haliwezi kuwa hoja ya Kanisa Katoliki kupinga asili ya kibinadamu. Binadamu ameumbwa na mwili, nafsi na roho; anahitaji uhuru wa kibiolojia, kisaikolojia na umiliki. Kufutilia mbali uhuru huu kunapingana na uumbaji na utu wake.
 
Namjua paroko mmoja huko kusini anamke na mtoto, huyu mtoto anamuita baba yake "Babu" ila kwa hakika ni baba yake mzazi. Na Bado wanaishi pamoja mpaka Leo.
Ukienda Jimbo Katoliki la Mahenge na Ifakara, kuna Mapadre wengi tu wana familia na biashara zao binafsi. Achilia mbali maisha ya ulevi na ufuska uliokothiri kwa baadhi ya Mapadre na Watawa.

Haya mambo yanavyozidi kutamalaki, yanachangia wapinzani wetu kuendelea kututupia mawe kila wanapo jikwaa.
 
Kwa hiyo unamaanisha kabisa hilo linahitaji Reforms?
Huu mjadala haujadiliwi na sisi tu. Ni karibia dunia nzima. Ni vile tu Kanisa liwamua kuweka pamba masikioni. Ila mabadiliko hayakwepeki siku zijazo.

Kinyume na hapo, wapinzani wataendelea kujichukulia pointi za bure mara zote yatakapo tokea matukio tatanishi yanayo wahusu Mapadre na Watawa wetu.
 
Nguvu ya kanisa katoliki ipo kwenye sera yake ya useja,kanisa likiachana na useja nakuhakikishia ndio itakua mwisho wake.

A man with family is a weak man,waroma sio wajinga kama wewe wanajua nini wanafanya na kama mtu hawezi endana na kiapo hicho hajalazimishwa.

We endelea kulomba wanawake na kuwa na familia hakuna alokulazimisha ila jua your a weak man na taasisi kubwa kama ya RC haihitaji weak men.
 
Back
Top Bottom