@ngara24Tusubirie maoni ya ngara24 sasa
Kenyoko!.. kwahiyo unaaminisha watu ya kwamba padre alijiteka?!Binafsi nimesomea Katoke Seminary kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita. Nikiwa mtu niliyeishi ndani ya mfumo wa Kanisa Katoliki, ninaweza kusema kwa ukweli kuwa kanisa hili limejipanga vizuri sana katika idara na utendaji wake. Hata hivyo, bado kuna changamoto kubwa katika namna linavyowatendea Mapadre na Watawa wake.
Kumekuwa na taarifa na tuhuma kwamba baadhi ya Mapadre wanapitia msongo mkubwa wa maisha unaowasukuma kuchukua hatua kali kama kujiteka, kujidhuru au hata kujiua. Ingawa binafsi sina imani kubwa na vyombo vya dola kama jeshi la polisi, kwa kuzingatia falsafa na mifumo ya kanisa, ninaona kuna chembe ya ukweli katika matukio hayo.
Kibinadamu, mtu ameumbwa na asili ya kutaka kumiliki—iwe ni fedha, nyumba, mali au familia. Ni vigumu sana kwa binadamu kukana kabisa asili hii. Hata mnyama kama mbwa anatambua sahani yake na hawezi kuruhusu mwingine kula chakula chake; sembuse binadamu. Kwa hiyo, ni changamoto kubwa kumlazimisha Padre kuishi maisha yasiyo na umiliki wowote—bila fedha, mali, wala mwenza.
Shinikizo la maisha hayo linaweza kuwapelekea baadhi ya Mapadre na Watawa kukopa kwa siri, kushindwa kulipa, na hatimaye kupata msongo wa mawazo, shinikizo la damu, au kufikia hatua mbaya ya kujidhuru.
Kimsingi, mwanaume au mwanamke aliyekomaa kisaikolojia na kimwili hawezi kuishi bila mwenza au bila kushiriki tendo la ndoa—hilo ni hitaji la kiasili, si udhaifu. Kwa hiyo, naamini iwapo Mapadre na Watawa wangepewa uhuru wa kumiliki mali binafsi na kuwa na wenza, wangeishi kwa amani zaidi, na utii wao kwa kanisa ungeongezeka marView attachment 3490237
Ngono ni hitaji la msingi la kila mtu aliye timamu kibaolojia wala sio uhuni au uasiHata mimi nimepitia kwenye shule zao, miaka mingi iliyiopita. Siku zote nimekuwa muwazi kuhusu maisha ya Maaskofu, Mapadre, na Watawa wa kiume na wa kike wa Kanisa Katoliki!
Waachane na maisha ya useja! Kwa sababu ni wachache tu kati yao ndiyo wanayaishi hayo maisha. Wengi wamekuwa wakifanya uzinzi kimya kimya!
Yaani kiufupi Kanisa Katoliki hata kama ni kongwe kuliko Makanisa yote duniani; bado hawazuiliwi kubadilisha aina yao ya maisha. Maaskofu na Mapadre waruhusiwe kuoa kama ilivyo kwa Makatekista! Mwisho wa mwezi walipwe posho kutokana na sadaka tunazotoa, pamoja na uwekezaji wa miradi mbalimbali.
Maisha ya kuishi useja, kutokumiliki mali au familia; kiukweli yana changamoto nyingi za kisaikolojia. Na wanaoshindwa kuyaishi hayo maisha ndiyo utawakuta wana vimada na watoto wao pembeni! Wana biashara zao binafsi, nk.
Mabadiliko kiukweli hayakwepeki.
Naungana na wewe huko ni kupinga natureNdo mjue sasa kua huo ukatoliki ni imani ya watu wa huko roma na sio dini hivi dini kweli inaweza kumkataza mtu asioe wala asiolewe huku ni kupingana na maumbile haiwezekani abadani asilani haiwezekani
N
Kweli mkuu samahani kwa kutoka nje ya mada kidogo 🙏Uzi haujazungumzia uislam au udini
utamu kama ule utanyimaje wakati ni hitaji la kibayojia?Hata mimi nimepitia kwenye shule zao, miaka mingi iliyiopita. Siku zote nimekuwa muwazi kuhusu maisha ya Maaskofu, Mapadre, na Watawa wa kiume na wa kike wa Kanisa Katoliki!