Kanisa Katoliki mnazingua, michango imekuwa kero

Kanisa Katoliki mnazingua, michango imekuwa kero

Michango ya kanisa ukitoa kwa moyo kadiri uwezavyo bila manung'uniko kuna baraka nyingi sana.
Ningeweza kutoa shuhuda nyingi hapa, ila si sawia kadiri ya desturi zetu wakatoliki.
Sadaka ya kweli ni ile inayouma, japo mtoaji hupaswi kulalama njia nzima
Hebu hudhuria kanisani ujionee michango kama utitiri
 
Sasa si bora huku bongo, njooo huku Monrovia uone watu wanavyolazimishwa muchango
 
Solution ni kuacha kutoaa hiyo michango tu, kwani umelazimishwa?

Kingine, mapadre waache na wakome kutoa vitisho vya kishamba kishamba Kwa waumini,

Matangazo ni mengi na marefu ambayo mengi ni useless,

Mahubiri yawe mafupi yenye kumjenga mtu kiimani na kiroho, sio kila mahubiri lazima waongelee kuhusu hela,

Tusikubali mambo ya kijinga kijinga kanisani, padre yupo kwàajili ya waumini, sio waumini kwàajili ya padre.

Kama hutaki kutoa huduma toka na upote parokiani kwetu,
umejileta wewe mwenyewe parokiani kwetu,ni wajibu wako kutupatia huduma.

Sisi Waumini kama tukipendezwa tunaweza tukachanga chochote kitu, lakini sio lazima.
Umeongea kitemi
 
Huku kwetu Paroko alianza kutupagia kiwango kila jumuiya, tukamuitikia tu. Ikifika ktk utekelezaji tunapeleka tulichokipata kata kama 70,000. Basi anakasirika

Akaanza kufoka na kututishia kwa maandiko. Tukamwambia yeye hana majukumu, pia asitupangie ktk utoaji. Maisha ya waamini n magumu sana. Wapo wanakula milo miwili tu. Yeye hajawahi kugawa hata mche wa sabuni kwa kaya maskini.

Sisi tumeamua kutoa sadaka, zaka na mavuno basi. Tena kila mmoja kuamua si kumpangia ktk utoaji.

Katika kikao cha halmashauri Paroko alipewa ukweli tu, ajue pia hali ya kiimani ya waamini wake kama anavyojua kaya zisizotoa michango.

Wakatoliki ifike wakati tauche unafiki wa kufukia makosa. Tuache yasemwe turekebishe. Jamaa amesema baadhi wanamwandama kwa maneno makali. Sio namna nzuri ya kutatua ama kutetea taasisi.
duuh safi mkuu naona umeamua kujivika mabomu kwa maslahi ya wengi
 
duuh safi mkuu naona umeamua kujivika mabomu kwa maslahi ya wengi
Kosa wanalofanya ni kutozingatia saikolojia,kipato na muda.Wangekuwa wanapopiga harambee isichukuwe muda mrefu na kufanya kama mashindano unachosha akili ya za watu.kuhusu muda wasiambatanishe michango mingi muhimu wakati mmoja.mf kama kuna michango ya ujenzi wa parokia wasimame na hili hadi liishe ndipo waanze lingine.Ila zaka ni wajibu kila mmoja atalipa kwa wakati wake .kuhusu kipato unakuta michango sawa hata haanagaliwi mgane mwenye hali ngumu walau wangempunguzia huyu.Mwisho kwa nyongeza wafanye sensa ya waumini kwenye jumuiya ili wakinuwa idadi michango iliyoratibiwa vizuri igawanywe kulingana na sensa.Vinginevyo itakuwa watoaji ni wale wale kila siku hatimaye wanakata tamaa.
 
Mnashindwa wapi kusoma saikolojia za watu.Yani kunapokuwa na matukio ya komunyo ya kwanza au kupaimara mnawakamua waumini michango hadi wanachukia dini.

Halafu siku ya tukio la komunyo bado tena wanakamuliwa wazazi kupitia harambee tena siyo tu kuwahusisha wanaume katoliki na wanawake katoliki bali wanaitwa watoto wanapangwa mbele na kuitwa kila mzazi aje kumgombowa mtoto, halitoshi mama aliyesuka vizuri anapelekewa kikapu.

Acheni kuwadhalilisha wazazi kama alibakiwa na buku 2 hatimaye anashindwa hata kukodi boda. Michango ya ujenzi ina utaratibu wake haya mengine ni unyanyasaji.
Ofisi zipo Kaka, katoe maoni
 
Mkuu mbona huko afadhari?
Njoo kwenye madhehebu ya kilokole sasa!
Utajuta!
 
Back
Top Bottom