Kanisa la Tanzania linapitia kipindi kigumu sana. Mungu alinusuru

Point no 4, Refer sadaka aloitoa Mungu kumtoa Yesu Kristo, Ibrahimu kumtoa Isaka. Hivyo basi huoni ya kuwa Mungu mwenyewe ndio muanzilishi wa Sadaka???

Sadaka ni divine invitation, Kamsome Kornelio, Dorcas na Daudi.
Sadaka ya Yesu Kristo msalabani (sacrifice) haifanani kamwe na fedha na mali. Huku ni kuudharau msalaba.

Ibrahimu na Isaka ilikuwa unabii wa Kristo msalabani.

Mwanzo 22:2
Akasema, Umchukue mwanao, mwana wako wa pekee, umpendaye, Isaka, ukaende zako mpaka nchi ya Moria, ukamtoe sadaka ya kuteketezwa huko juu ya mlima mmojawapo nitakaokuambia
.

Kristo ni mwana wa pekee wa Mungu. Huyu ni kwangu mpendwa wangu niliyependezwa naye. Sawa huwezi kusema fedha ni nwanao mpendwa uliyependezwa naye kwa sababu maandiko yamekataza kupenda mali. Habari za kuambiana utoe sadaka inayokuumiza, yaani mali, ni uongo.

Kama matoleo (weweumeita sadaka) ni divine invitation basi tufanyacho ni BRIBING GOD.
 
Ondoa Hapo namba 3 umekosea.Tunaona shule hospitali vyuo n.k vyote hivi vinatoa huduma katika jamii wakati huo mapadre si watu matajiri kama ilivyo kwa wengine na injili inahubiriwa kama kawaida.
Usilolijua...Kuna padre ameangusha ghorofa karibu na kibanda changu
 
Jambo lingine la msingi ndugu zangu katika Bwana..

Tumefika tulipo fika kwasababu hatuakisi upendo.. tunatazama utoaji wa sadaka na kutaka kuwa wakamilifu lakini tukumbuke upendo..
 

Attachments

  • Screenshot_20221029-064458.png
    26.6 KB · Views: 2
  • Screenshot_20221029-064558.png
    24 KB · Views: 5
  • Screenshot_20221029-064910.png
    27.3 KB · Views: 2
Pia udini.. naongea Kila mara hamna dini inayookoa mtu ..Ukristo sio dini, shida inaanza tunapolazimisha Ukristo uwe dini.. lazima ufanye hivi upate majibu, lazima ufanye hivi uwe mtakatifu.. mambo ya kujitakasa takasa
 
Umuombe Mungu yupi huyo? You are doomed.
 
Kanisa ni jumuiya huru, uwe na mchango au usiwe nao, uwe na hela au usiwe nayo, ubaya ulioposasa huku RC tunapeana mpaka risiti za michango ya jumuiya...hizo ni sadaka hapa panaboa sana.
Michango imewaweka pembeni wakristo wasikini!
Michango ndiyo inayompaa tenda za ujenzi na usambazaji wa huduma muhimi nanilii hapa Arusha....
Nasema bila michango bado watu tutatoa kwa moyo....
 
Ondoa Hapo namba 3 umekosea.Tunaona shule hospitali vyuo n.k vyote hivi vinatoa huduma katika jamii wakati huo mapadre si watu matajiri kama ilivyo kwa wengine na injili inahubiriwa kama kawaida.
Kama kuna kitu sintokuja kurudia kutoa ni mchango wa kujenga mradi wa kanisa!! Iwe ni hospitali, shule, hotel, au gesti hausi, SITOI, kkkt arusha ilinipa somo.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Hiyo namba 3 sio changamoto ya RC kuyumbisha kanisa, amekwepa kusrma changamoto za ukweli, uzinzi wa mapadri na mauaji kanisani tena mauaji ya mapadri ni changamoto kubwa sana huko RC
 
Tumsifu Yesu Kristo Tate Mkuu

Watu wanasahau kwamba makanisa na misikiti inaendeshwa kwa sadaka na kutoa sadaka ni maelekezo ya Mungu bila shurti
RC changamoto yao kubwa kwasasa ni uzinzi wa mapadri, pia mauaji ya mapadri kanisani na hakuna kesi inafikirisha sana
 
Kanisa linapita nyakati ngumu sana. Nyakati hizi sisi akina baba tusiposimama kuijua imani vema na kuongoza familia badala ya kuwaachia wanawake mambo ya imani utaangamiza familia yako kama si leo ni kesho!

Ukristo umevurugwa sana sana! Makanisa mama yaliyokuwa nguzo nayo yanapigwa mawimbi ya nguvu! Walokole ndio wamevurugwa kiasi cha kutisha! Tuliombee Kanisa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…