Kanisa la Tanzania linapitia kipindi kigumu sana. Mungu alinusuru

Watumishi wameitwa kuhubiri uchemi kibiblia? Mbona unatupiga fix jamani? Hao hao watumishi walioitwa kuhubiri uchumi wakitaka gari la kutembea wanaomba mchango kwa waumini na waumini wakitaka gari wanaambiwa waombewe na mhubiri aliyewaomba mchango. Kwa nini yeye mhubiri asiombe gari kwa njia ya maombi?
Ungekuwa wa kambi hii ungejua ninachomaanisha hakuna mtu aliyekilimia kila kitu kwenye ufalme wa Mungu, Mungu amegawa vipawa tofauti ili kuukamilisha mwili wa Kristo
 
Hiyo namba 3, waumini tuko imara sana. Maana michango yote tunayochanga ni kwa ajili ya kulitegemeza Kanisa la Mungu.

Halafu ifikie wakati tuwe wakweli! Hakuna binadamu asiyeishi katika Jumuiya! Sasa kama wewe jumuiya yako ni ya wavuta bangi, inakuwaje tena unataka uzikwe na jumuiya nyingine?
wewe nadhani huujui ukristo wa kweli au unaujua lakini hujitambui. Mungu akusaidie na akubariki ukae vizuri kwenye neno lake na uujue ukweli.

Je, Kama hutoi michango kwenye jumuiya na makanisani lakini unahudhuria misa zote ina maana wewe unaishi na kusali na wavuta bangi? maana nimeshuhudia marehemu anagomewa kufanyiwa sala kabla ya maziko kwasababu alikuwa sio mtoaji zaka.

Je kama mtu hatoi michango kanisani na kwenye jumuiya lakini analisha kituo cha mayatima kwa zaidi ya mwaka mzima na hajamwambia mtu, hiyo sio sadaka? na anaishi na jumuiya ya wavuta bangi?

Kumbuka ukimnyooshea mwenzako kidole, vidole vitatu kati ya vinne vilovyobaki, vinakua vimekuelekea wewe.

binadamu hatuna mamlaka ya kuhukumu, mamlaka hayo anayo Mungu pekee. Sisi wajibu wetu ni kutoa huduma na kupeana faraja wakati wa mapito yetu hapa duniani.

Hao wavuta bangi unaowadharau kwa taarifa yako ni watu muhimu kukupita hata wewe kwenye jamii. Wao ndio wanaofanya kazi zote za hatari ambazo wewe huwezi kuzifanya hapo mtaani kwako.

1. wao ndio wanazibua vyoo vyako vikiziba hapo nyumbani kwako.

2. Kama unafuga hapo nyumbani, mifugo ikifa, wao ndio utawaita kuja kuzoa iyo mizoga na kuichimbia na kuifukia.

3. Ukiwe na sherehe hapo kwako, wao ndio utawaita kukuchinjia mbuzi. Alafu kwa roho ya uchoyo uliyonayo, utaishia kuwapa kwato tu wakale na familia zao

4. Wao ndio wanakulinda usiku wakati wewe umelala unakoroma. Alafu mwisho wa mwezi unachangia buku tano ya ulinzi wa sungu sungu, tena unautoa kwa mbinde, huku ukilalamika lawama ambazo hazina kichwa wala miguu.

5. Wao ndio watabeba jeneza lako siku ukifa maana mabishoo wenzako watasimama pembeni tu na suti zao na miwani meusi wakiangalia na kuweka mapozi ya picha, baadae watupie insta.

6. Wao hao hao ndio watafunga maturubai nyumbani kwako siku ukifa maana mabishoo wenzako watakua wametulia kivulini wanapiga story na selfie za kutosha.

7. Wavuta bangi hao hao ndio watakusaidia kubadili tairi ya ki passo chako cha mkopo siku ukipata pancha kitaani kwako.

Hizo ni baadhi tu, zipo nyingi sana.

Sasa we jiulize kati ya wavuta bangi na wewe nani ana manufaa hapo mtaani? nani anaishi kikristu zaidi? wewe au wao? maana ukristu wa kweli unaonekana kwenye matendo yako!
 
Yesu alikuja kutuokoa na dhambi na SI kuhukumu,hivyo huduma ya kikanisa ni ya Kila mtu bila kuhukumu.kumtenga mtu tena akiwa mfu SI sawa,yesu alitufundishe tusilipize .
Kwa akili za kawaida unaweza ukawa na hoja ila ukiingia upande wa imani still ikawa hoja mfu,kwanini nasema hivi?

Wakati nikiwa mzima wa afya na akili zangu timamu nazulula mtaani sikuwahi kuwa interested na mambo ya Kanisa,wala kukusanyika na wenzangu kusali nao japo kwa saa moja ndani ya wiki leo nakufa wewe unajikusanya na watu wako unabeba maiti yangu unaenda kuilazimisha ikamkiri Mungu unadhani ni sawa?kwa hiyo Mungu kupitia wewe ambaye na wewe una dhambi zako ataisikiliza sala yako kuliko ile ambayo ilibidi nimuombe mimi wakati bado nikiwa hai?

Kanisa siyo sehemu ya kufanya unafiki kama unataka ibada ianzishe wewe kwenye maisha yako ukiwa bado hai ili siku ukifa watakaobaki wakaikamilishe kwenye safari yako ya mwisho.
 
Ungekuwa wa kambi hii ungejua ninachomaanisha hakuna mtu aliyekilimia kila kitu kwenye ufalme wa Mungu, Mungu amegawa vipawa tofauti ili kuukamilisha mwili wa Kristo
Mahibiri kama haya yanatumiwa na hao matapeli kupiga watu. Eti mtu ana kipawa cha kuombea watu wapate magari halafu yeye mwenyewe anaomba achangiwe kununua gari yake!
 
wewe nadhani huujui ukristo wa kweli au unaujua lakini hujitambui. Mungu akusaidie na akubariki ukae vizuri kwenye neno lake na uujue ukweli.

Je, Kama hutoi michango kwenye jumuiya na makanisani lakini unahudhuria misa zote ina maana wewe unaishi na kusali na wavuta bangi? maana nimeshuhudia marehemu anagomewa kufanyiwa sala kabla ya maziko kwasababu alikuwa sio mtoaji zaka.
Siku zote tunapojadili hili jambo kuna point huwa tunai-miss.

Kila taasisi ina sheria na taratibu zake,Jumuiya siyo sehemu ya kukusanya michango (hoja ya wale wanaozipinga)bali ni sehemu kwanza ya kusali na pia kuratibu mambo mbalimbali ya waumini.

Hoja kwamba mtu unalisha kituo cha yatima huku unahudhuria Kanisani swali litakuja kwanini ibada yako usiianze na wenzako mtaani kama sheria na taratibu za Kanisa zinavyosema?
 
Siku zote tunapojadili hili jambo kuna point huwa tunai-miss.

Kila taasisi ina sheria na taratibu zake,Jumuiya siyo sehemu ya kukusanya michango (hoja ya wale wanaozipinga)bali ni sehemu kwanza ya kusali na pia kuratibu mambo mbalimbali ya waumini.

Hoja kwamba mtu unalisha kituo cha yatima huku unahudhuria Kanisani swali litakuja kwanini ibada yako usiianze na wenzako mtaani?
na kwanini unichagulie mahali pa kutoa sadaka yangu? kwa mamlaka gani uliyonayo?
 
Calonga soma uelewe usisome ili ujibu au lengo lako unataka kuupeleka mjadala unakoona wewe kunakufaa?

Ktk andiko langu kuna sehemu nimesema muumini lazima atoe sadaka kama hana?au kwamba kama una sadaka lazima ukaitoe Kanisani au kwenye Jumuiya?
 
Huu ni uzushi na ujinga na Uzindaki wa kiwango Cha juu, hakuna ibada kwenye spiritual world isiyoambatana na sadaka ndo maana kwenye ibada yeyote Ile sadaka ni muhimu ili kufanya upatanisho kwenye spiritual
Mleta mada hakusema sadaka zisitolewe alichosema yeye ni mafundisho kuhusu sadaka kuchukua sehemu kubwa ya mahubiri.

Hao kina mwamposa ndiyo habari za acha dhambi sijui usizini au saidia maskini wameachana nazo wanachosisitiza wao ni toa toa toa utabarikiwa hawana lingine.
 
Mwakasege naye amechachamaa na masomo ya sadaka mwanzo mwisho, mfano semina ya Mbeya (26-30 Oct, 2022) somo ni sadaka tu hakuna kingine.
Sasa ataenezaje neno la Mungu pasipo sadaka? Mahema yanayofungwa , viti vinavyotumika unafikiri Hela inatoka wap? Bado kusafirisha vifaa mkoa Hadi mkoa Kwa ajili ya mikutano, Bado watumishi wale na wanywe walau maji. Huoni vyote hivyo vinahitaji pesa? Bado pesa za kurusha matangazo Ili neno la Mungu lisikike. Hujalazimishwa kutoa ni hiari ya mtu.

Sent from my M2004J19C using JamiiForums mobile app
 
wewe nadhani huujui ukristo wa kweli au unaujua lakini hujitambui. Mungu akusaidie na akubariki ukae vizuri kwenye neno lake na uujue ukweli.

Je, Kama hutoi michango kwenye jumuiya na makanisani lakini unahudhuria misa zote ina maana wewe unaishi na kusali na wavuta bangi? maana nimeshuhudia marehemu anagomewa kufanyiwa sala kabla ya maziko kwasababu alikuwa sio mtoaji zaka.

Je kama mtu hatoi michango kanisani na kwenye jumuiya lakini analisha kituo cha mayatima kwa zaidi ya mwaka mzima na hajamwambia mtu, hiyo sio sadaka? na anaishi na jumuiya ya wavuta bangi?

Kumbuka ukimnyooshea mwenzako kidole, vidole vitatu kati ya vinne vilovyobaki, vinakua vimekuelekea wewe.

binadamu hatuna mamlaka ya kuhukumu, mamlaka hayo anayo Mungu pekee. Sisi wajibu wetu ni kutoa huduma na kupeana faraja wakati wa mapito yetu hapa duniani.

Hao wavuta bangi unaowadharau kwa taarifa yako ni watu muhimu kukupita hata wewe kwenye jamii. Wao ndio wanaofanya kazi zote za hatari ambazo wewe huwezi kuzifanya hapo mtaani kwako.

1. wao ndio wanazibua vyoo vyako vikiziba hapo nyumbani kwako.

2. Kama unafuga hapo nyumbani, mifugo ikifa, wao ndio utawaita kuja kuzoa iyo mizoga na kuichimbia na kuifukia.

3. Ukiwe na sherehe hapo kwako, wao ndio utawaita kukuchinjia mbuzi. Alafu kwa roho ya uchoyo uliyonayo, utaishia kuwapa kwato tu wakale na familia zao

4. Wao ndio wanakulinda usiku wakati wewe umelala unakoroma. Alafu mwisho wa mwezi unachangia buku tano ya ulinzi wa sungu sungu, tena unautoa kwa mbinde, huku ukilalamika lawama ambazo hazina kichwa wala miguu.

5. Wao ndio watabeba jeneza lako siku ukifa maana mabishoo wenzako watasimama pembeni tu na suti zao na miwani meusi wakiangalia na kuweka mapozi ya picha, baadae watupie insta.

6. Wao hao hao ndio watafunga maturubai nyumbani kwako siku ukifa maana mabishoo wenzako watakua wametulia kivulini wanapiga story na selfie za kutosha.

7. Wavuta bangi hao hao ndio watakusaidia kubadili tairi ya ki passo chako cha mkopo siku ukipata pancha kitaani kwako.

Hizo ni baadhi tu, zipo nyingi sana.

Sasa we jiulize kati ya wavuta bangi na wewe nani ana manufaa hapo mtaani? nani anaishi kikristu zaidi? wewe au wao? maana ukristu wa kweli unaonekana kwenye matendo yako!
Mimi nimetolea mfano! Wewe sasa ndiyo umeuvalia njuga! Basi sawa. Naheshimu mawazo yako.
 
Hiyo namba 3, waumini tuko imara sana. Maana michango yote tunayochanga ni kwa ajili ya kulitegemeza Kanisa la Mungu.

Halafu ifikie wakati tuwe wakweli! Hakuna binadamu asiyeishi katika Jumuiya! Sasa kama wewe jumuiya yako ni ya wavuta bangi, inakuwaje tena unataka uzikwe na jumuiya nyingine?
Mkuu ifike mahali kanisa liishi kwa kutosheka na sadaka zetu maana haiwezekani kila misa na ibada ninayohudhuria natoa sadaka halafu eti wakitak kunenga nyumba ya Padre wanakuja tena kudai fedha za ujenzi. Mfano ni sisi waumini wao kupitia ujira tunaoupata kwa kazi zetu za kila siku tunatenga bajeti ya chakula, kusomesha mavazi na mambo mengine ya maendeleo pasipo kutegemea kupitisha bakuli kwa watu wengine.
Kwahiyo ifike mahali kanisa litambue na liishi kwa kutegemea sadaka na sio kutulundikia michango waumini, kama kuna mambo mengine wasiwe na haraka waende taratibu kwa chanzo hicho kikuu cha mapato.
Hali ilivyo sasa waamini wamerundikana kwenye nyumba za kupanga huku watumishi wa kanisa wakiishi kifahari

Sent from my TECNO KC6 using JamiiForums mobile app
 
Sasa usipomjengea nyumba Padre wako kupitia hicho kidogo unachotoa! Atamjengea nani? Halafu unaposema watumishi wa Kanisa wanaishi kifahari, una maana gani!

Ulitaka walale nje, watembee kwa muguu kuja kukupa huduma ya kiroho, wale vyakula vichafu ili waumwe matumbo na kushindwa kuendesha ibada/misa!!

Mimi ninachofahamu, hiyo michango ni ya hiyari! Na ukiona inakukwaza, hamia Kanisa/dhehebu lingine ambalo halina hiyo michango. Kulalamika tu pasipo kuchukua hatua, haitakusaidia kitu.
 
Eti mgogo na kimaro wanaiga staili ya wa pentekoste kuhubiri, ungekuwa unajua historia ya injili ungejua muhubiri aliyezaa upentekoste alikuwa Martin Luther mluteri usingeandika ulivyoandika,na ungejua kategori za watumishi wanavyoitwa usingehukumu watumishi kirejareja hivyo wapo watumishi wameitwa kuhubiri uchumi kibiblia kwa hiyo mostly watahubiri katika mlengo huo,n.k

Tofautisha upentekoste na Protestant. Upentekoste wa Sasa ulianza 1900's kwenye uhamsho wa Azusa kule marekani. Na muasisi ws vuguvugu la upentekoste ni mmarekani mweusi mch William Seymour.
 
Huu ni uzushi na ujinga na Uzindaki wa kiwango Cha juu, hakuna ibada kwenye spiritual world isiyoambatana na sadaka ndo maana kwenye ibada yeyote Ile sadaka ni muhimu ili kufanya upatanisho kwenye spiritual

Ukienda kwa waganga wa kienyeji lazima utoe sadaka ni ili wafanye upatanisho kwenye ulimwengu wa Roho

Sadaka inatumika na miungu kukamata mioyo yao ni mjinga pekee anayepinga sadaka, kama hutaki sadaka ni vizuri ukaachana na mambo ya kiroho

Mungu alishatoa sadaka yake ya mwana wake wa pekee kwa ajili ya mwanadamu. Hivyo anachohitaji Ni moyo wako zaidi uwe kwake sadaka ni ziada.
 
Tofautisha upentekoste na Protestant. Upentekoste wa Sasa ulianza 1900's kwenye uhamsho wa Azusa kule marekani. Na muasisi ws vuguvugu la upentekoste ni mmarekani mweusi mch William Seymour.
Mimi sizungumzii uprotestant nazungumzia injili yenye kuambatana na madhihirisho ya matendo ya Roho mtakatifu ambayo imebatizwa jina la upentekoste
 
Mungu alishatoa sadaka yake ya mwana wake wa pekee kwa ajili ya mwanadamu. Hivyo anachohitaji Ni moyo wako zaidi uwe kwake sadaka ni ziada.
Hujui unachoongea sadaka ya damu ya YESU ni mbadala wa sadaka za damu za wanyama ambazo zilikua zinatumika kufanya upatanisho kwenye ulimwengu wa Roho

Sadaka kama dhabihu, zaka, malimbuko, shukrani, mbegu ziko pale pale
 
Mimi nadhani ktk bandiko lako hoja #3 ihusuyo RC ungeitoa maana mimi binafsi nachangia Kanisa na taasisi zake hata nikiwa nje ya Kanisa au jumuiya,pia hakuna kitu kinaitwa "kama huna hela hupewi huduma za kikanisa”

Najua wewe siyo RC ila kama unaijua Radio Maria huwa kuna mchango wa kuiwezesha(maana haina matangazo yoyote ya kibiashara so ada yake pamoja na mishahara ya wafanyakazi inatoka kwetu sisi waamini) mwaka huu inatakiwa zaidi ya 1bill ambayo wasikilizaji tunaichanga tukiwa hata hatujuani,imani hakuna kulazimishana kama wewe huko uliko unalazimishwa ni wewe usituweke wote kwenye kundi moja
Huyu kaamua tu kupotosha, hiyo siyo changamoto ya RC,
 
Hujui unachoongea sadaka ya damu ya YESU ni mbadala wa sadaka za damu za wanyama ambazo zilikua zinatumika kufanya upatanisho kwenye ulimwengu wa Roho

Sadaka kama dhabihu, zaka, malimbuko, shukrani, mbegu ziko pale pale
Mungu gani tena wakati tushaambiwa yesu ni mungu?
 
Back
Top Bottom