Hiyo namba 3, waumini tuko imara sana. Maana michango yote tunayochanga ni kwa ajili ya kulitegemeza Kanisa la Mungu.
Halafu ifikie wakati tuwe wakweli! Hakuna binadamu asiyeishi katika Jumuiya! Sasa kama wewe jumuiya yako ni ya wavuta bangi, inakuwaje tena unataka uzikwe na jumuiya nyingine?
wewe nadhani huujui ukristo wa kweli au unaujua lakini hujitambui. Mungu akusaidie na akubariki ukae vizuri kwenye neno lake na uujue ukweli.
Je, Kama hutoi michango kwenye jumuiya na makanisani lakini unahudhuria misa zote ina maana wewe unaishi na kusali na wavuta bangi? maana nimeshuhudia marehemu anagomewa kufanyiwa sala kabla ya maziko kwasababu alikuwa sio mtoaji zaka.
Je kama mtu hatoi michango kanisani na kwenye jumuiya lakini analisha kituo cha mayatima kwa zaidi ya mwaka mzima na hajamwambia mtu, hiyo sio sadaka? na anaishi na jumuiya ya wavuta bangi?
Kumbuka ukimnyooshea mwenzako kidole, vidole vitatu kati ya vinne vilovyobaki, vinakua vimekuelekea wewe.
binadamu hatuna mamlaka ya kuhukumu, mamlaka hayo anayo Mungu pekee. Sisi wajibu wetu ni kutoa huduma na kupeana faraja wakati wa mapito yetu hapa duniani.
Hao wavuta bangi unaowadharau kwa taarifa yako ni watu muhimu kukupita hata wewe kwenye jamii. Wao ndio wanaofanya kazi zote za hatari ambazo wewe huwezi kuzifanya hapo mtaani kwako.
1. wao ndio wanazibua vyoo vyako vikiziba hapo nyumbani kwako.
2. Kama unafuga hapo nyumbani, mifugo ikifa, wao ndio utawaita kuja kuzoa iyo mizoga na kuichimbia na kuifukia.
3. Ukiwe na sherehe hapo kwako, wao ndio utawaita kukuchinjia mbuzi. Alafu kwa roho ya uchoyo uliyonayo, utaishia kuwapa kwato tu wakale na familia zao
4. Wao ndio wanakulinda usiku wakati wewe umelala unakoroma. Alafu mwisho wa mwezi unachangia buku tano ya ulinzi wa sungu sungu, tena unautoa kwa mbinde, huku ukilalamika lawama ambazo hazina kichwa wala miguu.
5. Wao ndio watabeba jeneza lako siku ukifa maana mabishoo wenzako watasimama pembeni tu na suti zao na miwani meusi wakiangalia na kuweka mapozi ya picha, baadae watupie insta.
6. Wao hao hao ndio watafunga maturubai nyumbani kwako siku ukifa maana mabishoo wenzako watakua wametulia kivulini wanapiga story na selfie za kutosha.
7. Wavuta bangi hao hao ndio watakusaidia kubadili tairi ya ki passo chako cha mkopo siku ukipata pancha kitaani kwako.
Hizo ni baadhi tu, zipo nyingi sana.
Sasa we jiulize kati ya wavuta bangi na wewe nani ana manufaa hapo mtaani? nani anaishi kikristu zaidi? wewe au wao? maana ukristu wa kweli unaonekana kwenye matendo yako!