Kapteni Ibrahim Traore adai nchi haiwezi kuendelea ikiwa katika mfumo wa demokrasia

Ikiwa wameshindwa kuondoa umasikini basi hawana positive impact

Barabara
Madaraja

Hata wakoloni walijenga is bullshit kuwasifu viongozi wa Africa ambao wamekuwa wakiliibia Taifa na kujilimbikizia mali
Bila Magufuli tusingekuwa na AIR TANZANIA, SGR na Stigler's Gauge bila kusahau DART na viwanda vingine alivyovianzisha na hapo mzee wa watu katawala tu kwa miaka mitano tu.

Bila Kagame pengine Rwanda ingeshuhudia Genocide nyingine na isingekuwa na jeshi imara la kuwachachafya wanajeshi wakongo.
 
Bila kusahau daraja la kigongo busisi, daraja la mwalimu Nyerere, flyover za kutosha na ujenzi wa ukuta wa Tanzanite .
 

Rwanda Mimi nimekaa na nimeenda Sana

Tanzania nimekaa

Viongozi wa Africa ukiachana na kuwa akili ndogo bado wamekuwa wakiliibia Taifa

Mfano huyo jamaa aliyekuwa anajenga madaraja alijitengenezea mirija ya upigaji mingi Sana


Ukija kwa kagame the same


Ndo maana wanakuwa waoga kuachia madaraka kwakuwa wanaogopa wakitoka madarakani wataingizwa nyuma ya nondo


Hata Cccm wapo tayari waue watu na sio kuachia nji

Kwakuwa wanajua wizi wao
 
Bila kusahau daraja la kigongo busisi, daraja la mwalimu Nyerere, flyover za kutosha na ujenzi wa ukuta wa Tanzanite .
Ndio alifanya kazi nzuri

Je umefanya mambo mazuri Kama haya Ila unaogopa uchaguzi unaiba kura

Tazama uchaguzi wa 2020 alivyojitia aibu


Hapo ndo ujue demokrasia mnaiogopa kwakuwa nyie ni wezi wa kura na Mali za umma.

Mtu ambaye sio mwizi na anafanya maendeleo ya kweli hawezi kugangania madaraka au kupora uchaguzi.
 
Wapi Magufuli kaiba? Hiyo AIR TANZANIA angeamua si angeiandikisha katika jina lake awe anaimiliki yeye?

Na hiyo Rwanda inapiga hatua kila kukicha hata Currency yake hatuifikii.
 
Wapi Magufuli kaiba? Hiyo AIR TANZANIA angeamua si angeiandikisha katika jina lake awe anaimiliki yeye?

Na hiyo Rwanda inapiga hatua kila kukicha hata Currency yake hatuifikii.
Je hizo Mali zake mahoteli ya kiahari ni mishahara tu?
 
Uganda, Rwanda,Tanzania za kidikteta zina maendelea gani?
 
Kwahiyo watu kama Mao ze Dong na Lenin Putin walikuwa wanaiba mali za umma kwakuwa walikuwa wanang'ang'ania madaraka?

Nakubali tumeshuhudia maditactor yasiyojielewa kama Mobutu ila ili nchi iendelee inabidi atokee kiongozi anayejielewa. Na mara nyingi viongozi hawa hawapatikani na kuwa maintained kwa demokrasia.
 
Waafrika wengi mnapenda mijeledi kama punda, na huyu ndivyo anavyotaka kuwapiga.

Na ni sawa tu, kwa sababu ndiyo mnavyopenda.

Hiyo nayo ni demokrasia pia.
Akishindwa huo mfumo wake atakuja kwenye demokrasia
 
Kuna Paul Biya wa Cameroon, halafu kuna Teodoro Nguema wa Equatoria Guinea ambaye yuko madarani tangu mwaka 1982 na pia kuna Faure Gnassignbe wa Togo ambaye alirithi uraisi kutoka kwa baba yake Ginassignbe Eyadema aliyeitawala Togo kwa miaka 46.

Hao watatu ndio madikteta haswa yaani utawala wao ni ule wa kidikteta kiasi kwamba hata wanainchi wenyewe hawawataki, ila huwezi ukaskia wakiongelewa mara kwa mara kwa na media za mabeberu, kwa sababu udikteta wao hauthiri chochote interests za mabeberu, wanaumizwa na udikteta wao ni wanainchi wao, mfano kama hiyo familia ya Ginassgnbe imeshalalamikiwa sana na wapinzani wa kisiasa nchini Togo nafikiri kwa huo ukanda wao ndio wana wafungwa wengi wa kisiasa, lakini hizo serikali za magharibi zimeweka pamba maskioni, na badala yake zinakomaa na watu kama Traore.

Wapenzi wa demokrasia wa afrika huwa ni vibaraka wa mabeberu wako kwa ajili ya kulinda interests zao wakitumia demokrasia kama camoufrage tu.
 
UKo sahihi na yuko sahihi. Demokrasia inatumika kwa tija katika mazingira yenye watu wenye sifa kuu 2 muhim.
1. WELL KNOWLEDGEABLE
2. WELL INFORMED
(sikupata kiswahili chake kwa haraka)
Ndio maana mifano ya scandnavian countries inaleta maana.
Kwa africa na Asia, demokrasia inatumika kama silaha ya ubeberu.
 
Nikweli kabisa demokrasia ni kichaka cha kurudisha Nyuma maendeleo.

Hakuna nchi zilizoendelea kwa kutumia democracy Bali Udictator.

Mfano ni nchi ya Libya ni nchi iliyokua na maendeleo makubwa chini ya utawala wa bwana Gadafy.

Wananchi walidanganyw a juu ya Mapinduzi ya kuleta utawala wa democracy sasa tuwaulizw Ile democracy waliokua wanaishabikia imewapa maendeleo?
 
Hakika....

Ni CCM tu ndiyo inayopambana na mifumo ya kibeberu ndani yake na nje yake....huko nje wanaanzia hawa MAKUWADI wa ubeberu na ukolonimamboleo akina Tundu Lissu na Chadema yao.....
 
Jumuiya ya Francophone iliwasakama kina Traore kisa mapinduzi lakini kina Mamadou Doumbiya hawakuambiwa chochote na yule Mahamat Idris Deby wa Chad ndo kabisa kuna media ya mabeberu ilandika Ufaransa imesapoti mapinduzi nchini kwake. Sasa unajiuliza kwa nini kina Traore wasakamwe lakini wengine wakifanya mapinduzi wapewe sapoti kabisaa. Jiongeze
 
Walichokipigania wamefanikiwa kwa kweli....wana maendeleo ya KUKOSA MAJI SAFI huku kila vitongoji vikijaa vikundi vya waasi na magaidi.....
 
Halafu muda si mrefu wenzake humo kwenye hicho kijeshi chao [more so kikundi tu cha wanamgambo wenye silaha na si jeshi proper] watamfurusha [kumpindua] au watataka kumfurusha.

Ni suala la muda tu.
Mpaka sasa hivi Capt. Traore amesha survive coup attempts zaidi ya 31 na amesurvive assasination attempts nne.

Kwa hiyo yeye mwenyewe analijua hilo ndio maana kila dk anayoishi yuko tayari kimamapambano... na of course kwa historia ya taifa la Burkinafaso yeye mwenyewe anajua uongozi wake hautakuwa na mwisho tofauti na wa watangulizi wake akina Zerbo,Jean Baptiste,Sankara,Campaore na huyu wa karibuni Damiba.
 
Doumbiya huyu huyu ambaye alikuwa ni ASKARI wa Ufaransa kule Ufaransa ?!!

Idriss Derby huyu huyu kipenzi cha wafaransa ?!!

UKUWADI wa ubeberu....
 
Usisumbuke kuumiza kichwa, mfano mzuri unao hapo Libya. Unaionaje Libya ya sasa ya kidemokrasia na ile ya kimapinduzi chini ya Ghadafi? Ingawa this is not always the case
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…