Kariakoo, Dar: Kumetokea ujambazi wa kutisha mtaa wa Lindi na Livingstone muda huu, Polisi mpo wapi?

Kariakoo, Dar: Kumetokea ujambazi wa kutisha mtaa wa Lindi na Livingstone muda huu, Polisi mpo wapi?

Kuna bodaboda mbili zilipita speed kwenda uelekeo wa mtaa wa Lindi na Livingstone, kumbe bwana walikuwa wanamkimbiza mhindi aliyekuwa kwenye bodaboda nyingine ya mbele akiwa na begi mgongoni, inasemekena ni mauzo ya dukani, basi nikasikia puuu, kugeuka nikaona ile bodaboda ya mhindi ipo chini, na zile bodaboda zilizomgonga mmoja wao akashuka na kuanza kukata mikono ya begi kwa kisu, mhindi akang’ang’ani begi, maumivu ya kisu yalipozidi mhindi akaachia begi, jamaa akapanda kwenye pikipiki wakaamsha, halafu eti watu wanaangalia tu, mi nilitaka kwenda ila nikaona wale jamaa ili mibisu yao sio ya kitoto, wameanza kuondoka watu ndio wanajidai kuwakimbiza, wakatikomea kupitia pale kona ya Azam, livingstone pale.

Hadi sasa hali ni tete, polisi wawahi hapo kuchukua maelelezo.

========================
Halafu Nimekumbuka, hilo tukio limetokea mbele ya CCTV camera za duka la ‘New Tahery stores’ na ‘D&S Lab equipements’ mtaa wa Lindi, Polisi wakazitizame zile footage wanaweza kuwaona wale majambazi wakati wanakimbizana’ , wacheki footage time ya kuanzia muda nimepost hii thread kurudi nyuma, ni pembeni ya ile nguzo ndio walipomgalagaza mhindi, mbele ya duka la ‘New tahery stores’.
Hii wazungu kitaalamu wanaita, "going back to square A".
 
Dawa ni pikipiki zisiruhusiwe ingia kkoo. Iwe marufuku kabisa kasoro za delivery, zenye delivery kit
ukisema uzuie pikipiki kuingia kkoo unafeli kwakua wapo wamiliki wa biashara wana tumia pikipiki kama usafiri wapo watu wanajiingizia kipato cha msingi ni jamii kukataa uhalifu na kua na ushirikiano tatizo kkoo linakuja pale tukio linatokea huwez saidia kwakua ukiacha biashara yako bas ukirud hamna kitu
 
Yaani raia mmeshindwa zuia uhalifu, halafu unauliza mahali polisi walipo!!

Unajua kuwa polisi mmoja anahudumia idadi ya watu wangapi?
haiondoi udhaif wa polis
 
Dar utauawa mbele za watu hakuna atakayekusaidia.
Nilikuta ajali mbaya watu wamegongwa na gari na kurushwa mtaroni na wanavuja damu kama kuku aliyechinjwa na wakilia kuomba msaada lkn hakuna aliyesogea zaidi wanapiga picha tu na midume kibao imezunguka.

Ndipo nilipojitosa kuwatoa mtaroni na kuwafunga majeraha yao huku wengine wakishangaa tu hadi nilipowafokea sana ...akajitokeza jamaa mmoja akanisaidia kuwanyanyua.

Wakazi wa Dar ni wa ajabu sana
Umenikumbusha riwaya ya kisa cha Chonya wa Chilonwa [emoji23] [emoji23] hongera sana mkuu
 
Yaani raia mmeshindwa zuia uhalifu, halafu unauliza mahali polisi walipo!!

Unajua kuwa polisi mmoja anahudumia idadi ya watu wangapi?

Aisee wizi kariakoo umeanza kupamba moto

Leo kuna jamaa amenyang’anywa simu mbele ya ofisi ya transporter amehangaika kumkimbiza mwenyewe

Watu wako busy na mambo yao

Hao ndo wana daslam
 
Pole sana kwa huyo aliyeibiwa....

Dar es Salaam ukishindwa kujitetea basi imekula kwako,,,, huu Mji hakuna anayejali...

Labda tu mambo ya umbea ndio wapo mstari wa mbele.
Ila mimi huwa nashindwa kuwaelewa watu wanaoporwa fedha karne hii ambapo kama ni mfanyabiashara kuna lipa namba kwa mitandao yote, mawakala wa benk zote wamejaa kila hatua mbili, hasa mijini, sasa ni kwa nini usubiri mpaka mauzo yafikie milioni 50??
 
Polisi wakisikia Chadema inakutana hawachukui hata sekunde kumi kufika
 
ukisema uzuie pikipiki kuingia kkoo unafeli kwakua wapo wamiliki wa biashara wana tumia pikipiki kama usafiri wapo watu wanajiingizia kipato cha msingi ni jamii kukataa uhalifu na kua na ushirikiano tatizo kkoo linakuja pale tukio linatokea huwez saidia kwakua ukiacha biashara yako bas ukirud hamna kitu
Hakuna haja ya kuzuia pikipiki,
Hivi watu wa Kariakoo wameshindwa hata kutumia fimbo za fagio na mfanowe kuwagalagaza hao wahuni?
 
Ahsante broohh...barikiwa Kwa uzalendo wakooo
 
Back
Top Bottom