Kariakoo, Dar: Kumetokea ujambazi wa kutisha mtaa wa Lindi na Livingstone muda huu, Polisi mpo wapi?

Kariakoo, Dar: Kumetokea ujambazi wa kutisha mtaa wa Lindi na Livingstone muda huu, Polisi mpo wapi?

Duuuh yaani watu wamekimbia watu walioshika visu? Je wangeshika BOMBA watu si wangeenda kukasimamia FAYA?
 
Kuna bodaboda mbili zilipita speed kwenda uelekeo wa mtaa wa Lindi na Livingstone, kumbe bwana walikuwa wanamkimbiza mhindi aliyekuwa kwenye bodaboda nyingine ya mbele akiwa na begi mgongoni, inasemekena ni mauzo ya dukani, basi nikasikia puuu, kugeuka nikaona ile bodaboda ya mhindi ipo chini, na zile bodaboda zilizomgonga mmoja wao akashuka na kuanza kukata mikono ya begi kwa kisu, mhindi akang’ang’ani begi, maumivu ya kisu yalipozidi mhindi akaachia begi, jamaa akapanda kwenye pikipiki wakaamsha, halafu eti watu wanaangalia tu, mi nilitaka kwenda ila nikaona wale jamaa ili mibisu yao sio ya kitoto, wameanza kuondoka watu ndio wanajidai kuwakimbiza, wakatikomea kupitia pale kona ya Azam, livingstone pale.

Hadi sasa hali ni tete, polisi wawahi hapo kuchukua maelelezo.

========================
Halafu Nimekumbuka, hilo tukio limetokea mbele ya CCTV camera za duka la ‘New Tahery stores’ na ‘D&S Lab equipements’ mtaa wa Lindi, Polisi wakazitizame zile footage wanaweza kuwaona wale majambazi wakati wanakimbizana’ , wacheki footage time ya kuanzia muda nimepost hii thread kurudi nyuma, ni pembeni ya ile nguzo ndio walipomgalagaza mhindi, mbele ya duka la ‘New tahery stores’.
Kila mmoja atamkumbuka jiwe Kwa style yake , sa hv likikukuta unakufa nalo mwenyewe
 
wazaz kuwa watz km wengine hainifany nisiseme udhaifu wa raia wa hii nchi hii , naunga mkoj hoja kuwa watz hamna tofaut na wapuuz wengine kwny ulimwng huu
Unatumia wifi ya Chama gani?
Coz mmekua kama mazombie,
 
Hicho kisa kiliniumiza moyo sana, baada ya kutoa huduma ya kwanza niliondoka hadi walipo traffic na kuwajulisha lkn walifika nao kwa kuchelewa kwa taarifa nilizozipata baada ya kufuatilia kesho yake.

Siku hiyo nilishindwa kula
Walifariki?
 
Dar utauawa mbele za watu hakuna atakayekusaidia.

Nilikuta ajali mbaya watu wamegongwa na gari na kurushwa mtaroni na wanavuja damu kama kuku aliyechinjwa na wakilia kuomba msaada lkn hakuna aliyesogea zaidi wanapiga picha tu na midume kibao imezunguka.

Ndipo nilipojitosa kuwatoa mtaroni na kuwafunga majeraha yao huku wengine wakishangaa tu hadi nilipowafokea sana, akajitokeza jamaa mmoja akanisaidia kuwanyanyua.

Wakazi wa Dar ni wa ajabu sana.
Watu wa Dar ni waoga sana. Sijui Yana tabia gani
 
hao wahindi Wana hela.
Kuna mzee alikuwa anahadithia Kuna ndugu yake NI mlinzi alikuwa analinda kwa wahindi Sasa siku moja usiku anaingia lindoni anakuta funguo za kamati la hela zipo juu na wenyewe hawapo.kufungua akakuta maburungutu ya hela za kutosha.akachukua milioni 15 akazificha.alivyokuwa mjinga zile funguo akaziacha pale pale mezani.
Kesho mabosi wanakuja wanakuta funguo zipo mezani wanaangalia Kuna wizi umetokea.
Mlinzi akakamatwa akapelekwa mahakamani akala miaka yake 6.na hela akarudisha
 
Kariakoo Kuna ujinga mwingi sana usije ukafikiri siku ukikutana na wezi utasaidiwa Kama unaweza pambana mwenyewe.
Nilishuhudia gari lililobeba tv likiibiwa tv moja kwenye foleni njia ya kuingia Somali street na watu wanaangalia huku wanacheka.ikaja boda boda ikambeba yule mwizi hao wakasepa
Yaani anabeba hela hata ngumi hajui
Bila pistol Sibebi hela mimi
 
Back
Top Bottom