Kariakoo, Dar: Kumetokea ujambazi wa kutisha mtaa wa Lindi na Livingstone muda huu, Polisi mpo wapi?

Kariakoo, Dar: Kumetokea ujambazi wa kutisha mtaa wa Lindi na Livingstone muda huu, Polisi mpo wapi?

Kumsaidia hapo ilitakiwa mtu uwe na bastola pekee uwashoot wale majambazi na si kuwasogelea!
 
Asilimia 90 ya watu unaowaona karikakoo ni vibaka, waporaji, wezi wa mifukoni, na matapeli......katika hali kama hiyo ni ngumu sana kusaidia uhalifu......ukiona wanakusaidia ujue kuna fursa ya wao kuiba......ndio maana wanaweza kukutetea ukiibiwa simu alafu unajikuta mwisho huna pochi.........

Asilimia kubwa watu wanawajua wezi wote.....Kwa kifupi karikakoo ni jamhuri ya vibaka, wezi na majambazi..........

Unaweza ukajitoa kusaidia kumbe waliokuzunguka ni wezi wenzie ukazurika..........

Niliwahi kusaidia Binti mmoja aliyekuwa anaibiwa pochi lake...... katika watu waliokuja kunisaidia kukabiliana na wale vibaka na mimi wakaniibia simu yangu......mpaka leo sithubutu kusaidia...
 
Haukuokota ata elfu kumi tano?maana ile pesa ilikua mingi hatari
Huwaga naogopa sana kujisogeza karibu na matukio makubwa,hua najificha kabisa , nakumbuka Yule binti aliyepigwa risasi pale kituoni Morocco na majambazi kisa alisimama tu kituoni wao walikua wanakimbia baada ya kufanya tukio
 
Ungepiga hata picha hiyo bodaboda ya majambazi polisi wapate pakuanzia kufanya uchunguzi sasa nyie mlikaa tu kuangalia afu unakuja kupigia kelele polisi kwani walikuwepo kwenye tukio
 
Kabla kuwala
Kuna bodaboda mbili zilipita speed kwenda uelekeo wa mtaa wa Lindi na Livingstone, kumbe bwana walikuwa wanamkimbiza mhindi aliyekuwa kwenye bodaboda nyingine ya mbele akiwa na begi mgongoni, inasemekena ni mauzo ya dukani.

Basi nikasikia puuu, kugeuka nikaona ile bodaboda ya Mhindi ipo chini, na zile bodaboda zilizomgonga mmoja wao akashuka na kuanza kukata mikono ya begi kwa kisu, mhindi akang’ang’ani begi, maumivu ya kisu yalipozidi Mhindi akaachia begi, jamaa akapanda kwenye pikipiki wakaamsha, halafu eti watu wanaangalia tu.

Mi nilitaka kwenda ila nikaona wale jamaa ile mibisu yao sio ya kitoto, wameanza kuondoka watu ndio wanajidai kuwakimbiza, wakatokomea kupitia pale kona ya Azam, Livingstone pale.

Hadi sasa hali ni tete, polisi wawahi hapo kuchukua maelelezo.

======================

Halafu Nimekumbuka, hilo tukio limetokea mbele ya CCTV camera za duka la ‘New Tahery stores’ na ‘D&S Lab equipements’ mtaa wa Lindi, Polisi wakazitizame zile footage wanaweza kuwaona wale majambazi wakati wanakimbizana’ , wacheki footage time ya kuanzia muda nimepost hii thread kurudi nyuma, ni pembeni ya ile nguzo ndio walipomgalagaza mhindi, mbele ya duka la ‘New Tahery Stores’.
Kabla kuwalaumu polisi anza na raia.Mitaa kama ya Kariakoo na Gerezani ni aibu kwa jambazi kumuibia mtu na akakimbia muda wa mcha.Foleni kama zile lazima washikwe hata wakiwa na SMG. nI dalili ya upungufu wa imani.
Polisi wakiienda waanze kuwashika majirani na wapita njia wote walioshuhudia tukio hilo isipokuwa wewe uliyetoa taarifa.
 
Unatembea na hela nying kweny beg afu huna hata bastola?huo nao ni uzembe mwngine
 
Hao wangapi anaowahudumia si pamoja na huyo?
Au hao wangapi ni wale maalumu?

Jamaa(wapo hapo karibu) wanashindwa kudhibiti wezi wakitaraji polisi(wapo mbali pasi taarifa) ndio wafanye kazi hiyo
 
Camera 540mil duh
Na wapo over ibil ina maana kwa wastan camera 1 watu 2 kweli wameamua
Kwa security wako vizuri ndio wanaongoza kwa kufunga cctv duniani
Na sisi ifike mahali basi vyuo vikuu vijana watengeneze jamani
Hata kukopi hatuwezi haha
 
Wahindi wanajibagua sana,kupiga kelele za" wezi au majambazi",ili kupata msaada wa waswahili na hilo bado awataki!
 
Yaani raia mmeshindwa zuia uhalifu, halafu unauliza mahali polisi walipo!!

Unajua kuwa polisi mmoja anahudumia idadi ya watu wangapi?
Wanaume wa Dar bana, mtu ana kisu unaogopa hata kumpopoa mawe.
 
Back
Top Bottom