Kariakoo hakuna machimbo tena, kwa atakayepuuza sitaongea tena

Kariakoo hakuna machimbo tena, kwa atakayepuuza sitaongea tena

Bro hujui how things work. Biashara zote dunian zinafanyika online na wakat mwingine huwez kuwa na watu wote online so unakuta una mawinga kama 50 kila mtu ana wafuasi elfu 4 tuseme na wanakuja dukan kupiga picha kuposti so ndani ya nusu saa kila Winga anakuja huyu anataka pcs 30 huyu kumi huyu 20 na wanakuja kuchukua mizigo kupelekea wateja huko walipo so yeye anapata cha juu na wewe unapata chochote kitu. Ndivyo mfumo wa biashara ulivyo dunian lazima awepo mtu wa kati anaerahisisha kazi zako ziaende. Kwa mtu ambae amesafir anajua hasa viwandani. Biashara ni agent mzee. Na hiyo ya dukan kusubirishwa ni kawaida kkoo mi tangu naanza biashara vijana wanafanya hivyo miaka hiyo we umestuka leo na hata wagen wanajua. Kwa mfano mimi biashara yangu ni groups za whatsp za wateja wangu kutoka congo zambia Zimbabwe kenya malawi Rwanda Burundi comoro msumbiji nk. So mzigo ukitoka natoa sampo store narusha kwenye whatsp kila mtu anaweka order humo humo kutoka hizo nchi na wanaingiza mizigo kwenye account yako unawatumia mizigo yao. Simpo mzee life ishabadilika kaka. Mimi naweza kuuza mizigo nikiwa hukuhuku china ikawafuata wateja walipo na wakaniingizia mpunga wangu kwenye account tu. So usikariri maisha mzee pinduka maisha na yenyewe yanavyopinduka waache wenye kibarua cha kulaumu walaumu kila mtu apigane vita vyake. Ukiona umestuka ujue kuna mwingine ni mtaji, biashara ni mchezo wa sanaa kuna wakati unafungwa na kuna wakat unafunga.
Mtu wa kati anaweza akawepo ila Kwa staha kidogo
Sasa hapo Kariakoo
Unafika mteja unazongwa kama nzi kwenye mzoga

Hata ule utulivu na kuaminika kuwa wanaokuuzia ni halisi unapotea
Nyie wenye maduka wapangeni mawinga wenu, wasiwe kama wapiga debe stend
 
Mpango mzima ni Maduka ya HOMECITY.
Na bado ile China ndogo pale Ubungo terminal ikikamilika wafanyabiashara makanjanja mtanyooka tu days are numbered.
Sijui kwa nini mnajidanganya na hako kasehemu kadogo kiasi hiko. Kariakoo Kuna Kila biashara ambazo zimesambaa hakuna sehemu inayoweza ku_match ukubwa wa Kariakoo. Cha msingi ni kutafuta taratibu na kutokuwa na papara. Mimi mwenyewe nanunua vitu vyangu Kariakoo na Kila baada ya muda nagundua duka zenye nafuu ambazo sikuzijua hapo mwanzo hapo hapo Kariakoo.
 
Nilishangaa bei ya vifaa vya jikoni kama jiko, fridge, oven nk mlimani city iko sawa na kariakoo, sasa si bora twende mlimani tu unapigwa kiyoyozi, hamna mawinga aka nzi wa chooni hakuna hofu ya kuibiwa wala harufu za vikwapa na midomo🙊
 
Very interesting. Ina maana wafanyabiashara halali wa Kariakoo ni mateka kwa mawinga?Hapa mpuuzi ni nani.
Ukitaka kwenda mbali lazima uwe fala kwenye mambo flan flan. Ni kama vile unavyotaka kuuza eneo unakuwa kwa muda mbele ya madalali mambo yako yaende. Usipojifunza kunyenyekea bro sahau kufika mbali nakuhakikishia utabakia tu kumiliki nyumba mbili tatu ukienda mbali utajenga hoteli au kumiliki apartment utajidanganya we ni tajiri. Mzee jifunze walipokosea waliokutangulia utafika mbali. Mi winga ndio wananipangia cha kuweka order kiwandani na mzigo ukifika fasta unaisha nataka nini sasa.

Kuitwa boss tajiri mwenye duka cjui mkuu hizo mambo ni upuuzi umetupumbaza wengi.

We jichanganye nao nakuhakikishia utakula mema ya nchi. Mfano mdogo.

Kuna winga mimi tulifikia mahali nikawafungulia maduka tunagawana kwenye faida baada ya mtaji wangu kurudi.

Mzee the sky is your limit ni wewe tu.
 
Umasikin ni mbaya sana aisee. Nyie ndio mkiona mtu kanunua range rover mnamlaumu kwa kununua gari inayotumia mafuta. Mzee ukiona unanunua kitu kwa kubagain ujue hali yako ni mbaya pambana mkuu.
Wengi wetu sisi WaTz ni mafukara tumetofautiana TU viwango vya ufukara wetu. Mimi nanunua kiatu mtumba, wewe utanunua gari mtumba Wakati nguo mtumba au kiatu mtumba hununui kamwe.
 
Kwani nyie wenzetu mnaenda Kariakoo na Ilala ipi? Kwa suala la mtumba hasa viatu na sandals kwa sasa biashara imekuwa ngumu mno hapo Karume sababu mtumba sasa hivi hautoki kama zamani na unaotoka kuna watu wana pesa ya kutosha wanahifadhiwa waje kununua kwa bei ya juu kidogo na wao wakauze kwa bei kubwq! Electronics mjomba umepuyanga, uliza detailcally uoneshwe maduka ya kununua braza.

Usitukane wote kwa sababu ulikwamishwa na maduka mawili au matatu.
 
Mtu wa kati anaweza akawepo ila Kwa staha kidogo
Sasa hapo Kariakoo
Unafika mteja unazongwa kama nzi kwenye mzoga

Hata ule utulivu na kuaminika kuwa wanaokuuzia ni halisi unapotea
Nyie wenye maduka wapangeni mawinga wenu, wasiwe kama wapiga debe stend
Ukitaka utulivu nenda mwenge ucje huku changanyiken mkuu. We hujafika pratunam Thailand wewe uone huo mziki au indra pradesh India pale. Ukitaka kutoka hapo chini ni kama kupigana jihad mzee huitaji utulivu zaid ya umakin tu.
 
Kariakoo kila unaekutana nae usimuamini..

Hao wafanya biashara wenyewe hawana uhakika wa bei zao🤔

Unamuuliza bei ya bidhaa (mf. Kiatu) bei gani anakwambia 40k ukighairi ukitaka kuondoka utamsikia anashusha bei tena utaskia 'basi lipia 35k boss'😁

Ukirudi kuongea nae unachkua kwa 10k. 😂😂😂
Yeah!... muhimu usiogope ku-bargain
 
Mi
Usijisumbue kwenda kariakoo kununua mzigo ukidhani Kuna bei nafuu
Kariakoo wamejaa wajanja na madalali tu
Unaweza ingia kwenye duka ukamkuta mwenye duka ukamuuliza bei akakuelekeza uongee na vijana wake wakuumize
Nyie watu situka Kariakoo hakufai kabisa, mawinga wameharibu uaminifu
Matajiri wanauchukulia wateja kama wajinga, wanajua kuwa mtaenda tu
Sasa naomba niwape machimbo mapya Kwa Dar

1. Kwa wale wa electronics nenda Tegeta pale Kibo complex utapata bei ambayo Kariakoo haipo

Pia nenda Mbagala rangi Tatu utapata electronics zote, kuanzia Tv, simu, cable

2. Nguo nenda Mwenge au Makumbusho

3. Mitumba
Usijaribu kwenda Karume au Ilala tena
Kwa mitumba ya bei nafuu, mabalo za rejareja nenda Tandika, Temeke, Tandale na Mwenge

Kanda ya ziwa, machimbo yapo Katoro

Kwa machimbo mengine, tujaribu ku share.
Ila chonde chonde kariakoo utaishia kupandiliwa na kupigwa bei ya maana
Kariakoo nilikuwepo Jana, nikahairisha kuchukua mzigo kisa mawinga
mimi nikishasikia anamuita mtu naondoka sitaki ujinga shwaini mxiuuu
 
Wengine wetu sisi WaTz ni mafukara tumetofautiana TU viwango vya ufukara wetu. Mimi nanunua kiatu mtumba, wewe utanunua gari mtumba Wakati kiatu mtumba hununui.
Kimsingi sisi watz sio masikin mkuu. Ni hatujajua tu how things work na pia tuna ujamaa sana umetupumbaza. Wewe kama mshikaji unaweza ukawa huna kitu ukaja kwangu nikakutoa na ten nk. Hapo Dar life inaweza kukushinda ukarud kijijin mzee akakupa eneo ukalima life likaenda. Kwa wenzetu usipofanya kaz tena kwa nidhamu uchomoke imekula kwako. Hakuna wa kukupa hata mia na hakuna kijijin pa kwenda unabaki kuwa homeless mjin. Na ndio maana wageni wakija hapa wanatoka. Sisi hatuna tofauti na wale wazulu wa south Africa. Wao ni kucheza na kuimba hawataki kaz ni starehe tu ila ukija mgen ukifanikiwa hawataki. Sisi hatuna tofauti sana na wao
 
Usijisumbue kwenda kariakoo kununua mzigo ukidhani Kuna bei nafuu
Kariakoo wamejaa wajanja na madalali tu
Unaweza ingia kwenye duka ukamkuta mwenye duka ukamuuliza bei akakuelekeza uongee na vijana wake wakuumize
Nyie watu situka Kariakoo hakufai kabisa, mawinga wameharibu uaminifu
Matajiri wanauchukulia wateja kama wajinga, wanajua kuwa mtaenda tu
Sasa naomba niwape machimbo mapya Kwa Dar

1. Kwa wale wa electronics nenda Tegeta pale Kibo complex utapata bei ambayo Kariakoo haipo

Pia nenda Mbagala rangi Tatu utapata electronics zote, kuanzia Tv, simu, cable

2. Nguo nenda Mwenge au Makumbusho

3. Mitumba
Usijaribu kwenda Karume au Ilala tena
Kwa mitumba ya bei nafuu, mabalo za rejareja nenda Tandika, Temeke, Tandale na Mwenge

Kanda ya ziwa, machimbo yapo Katoro

Kwa machimbo mengine, tujaribu ku share.
Ila chonde chonde kariakoo utaishia kupandiliwa na kupigwa bei ya maana
Kariakoo nilikuwepo Jana, nikahairisha kuchukua mzigo kisa mawinga
Kuna siku nilikuta mashuka tandika bei kitonga,niliyakusanya kama yote,kufika home nilipomuambia Wife bei niliyonunulia,siku ya pili tulirudi wote kuyakusanya tena,tandika ipewe maua yake,kikubwa wangese mawinga wasiende kupaharibu,soko la ilala lilikua zuri sana kwa jeans za mtumba ila now ni ghari mno,jeans za bei rahisi ukiiotea kwa wale wanaotembeza mkononi
 
Back
Top Bottom